- Yanga SC vs Singida Black Stars ni mechi inayokwenda kuamua hatima ya ubingwa wa Ligi Kuu Bara (NBC Premier League), msimu huu.
- Mechi hii inatarajiwa kupigwa Ijumaa 22/5/2026, katika Uwanja wa KMC.
- Yanga SC wataingia katika mchezo huu huku wakiendelea kupokea presha kubwa, kutoka kwa watani zao Simba SC walio nafasi ya pili.
- Mara ya mwisho timu hizi kukutana matokeo yalikuwa Singida Big Stars 0-3 Yanga SC.
Vita ya ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara (NBC Premier League), itaendelea tena Ijumaa 22/5/2026, ambapo ratiba inaonyesha Yanga SC vs Singida Black Stars. Yanga SC ambao ndio mbingwa watetezi, itakuwa kibaruani kutetea ubingwa katika Uwanja wa KMC. Yanga SC wataingia katika mchezo huu huku wakiendelea kupokea presha kubwa, kutoka kwa watani zao Simba SC walio nafasi ya pili. Makala hii inakuchambulia baadhi yamambo muhimu, kuelekea mchezo huo.
Fuatilia mwenendo wote wa mashindano ya Ligi Kuu ya NBC 2025/26; Ratiba, matokeo, mechi, magoli na habari za papo kwa papo kupitia SportPesa Blog.
Je, unataka kushinda mamilioni? Unaweza kushinda mpaka Shilingi Milioni 800 na SportPesa
Wengi tayari wamevuna mamilioni kupitia mchezo wa Kindege yaani ‘Aviator’ ya SportPesa. Wewe unasubiri nini? Nafasi ni yako cheza Aviator na kushinda mpaka Shilingi Milioni 800 sasa kwa kubonyeza picha hii chini.

Aviator: Paisha kindege ushinde mpaka zaidi ya 800,000,000.
Yanga SC vs Singida Big Stars h2h

Katika michezo 9 zilizopita ambazo timu hizi zimekutana katika michuano mbalimbali Yanga SC wameshinda mechi 7, Singida Black Stars wao wameshinda mechi 2 tu. Hakuna matokeo ya sare katika michezo hiyo 9 iliyopita. Hii inafanya mchezo wa Ijumaa kuwa muhimu sana. Jedwali lifuatalo linaelezea takwimu hizi kwa ufupi.
| Tarehe | Mashindano | Mechi | Matokeo |
|---|---|---|---|
| 05/03/2026 | NBC Premier League | Singida Black Stars dhidi ya Yanga SC | 0-3 (Ushindi wa Yanga) |
| 29/06/2025 | CRDB Federation Cup Fainali | Yanga SC dhidi ya Singida Black Stars | 2-0 (Ushindi wa Yanga) |
| 17/02/2025 | NBC Premier League | Yanga SC dhidi ya Singida Black Stars | 2-1 (Ushindi wa Yanga) |
| 30/10/2024 | NBC Premier League | Singida Black Stars dhidi ya Yanga SC | 0-1 (Ushindi wa Yanga) |
| 11/03/2024 | NBC Premier League | Yanga SC dhidi ya Singida Black Stars | 5-0 (Ushindi wa Yanga) |
| 04/10/2023 | NBC Premier League | Singida Black Stars dhidi ya Yanga SC | 2-1 (Ushindi wa Singida Black Stars) |
| 16/01/2023 | NBC Premier League | Yanga SC dhidi ya Singida Black Stars | 1-0 (Ushindi wa Yanga) |
| 29/11/2022 | NBC Premier League | Singida Black Stars dhidi ya Yanga SC | 2-1 (Ushindi wa Singida Black Stars) |
SOMA HII PIA: Yanga SC vs Singida Black Stars Fainali CRDB, Baada ya kuiua Simba Yanga yafanya umafia mzito Zanzibar
Yanga SC, Singida Black Stars wanasemaje?
Yanga SC

Akizungumzia mchezo huo, Kocha mkuu wa Yanga SC, Abdi Hamid Moalin amesema: “Tumefanya maandalizi ya kutosha kuelekea mchezo huu, tunafahamu kuwa hauwezi kuwa mchezo rahisi kwa kuzingatia nafasi ya wapinzani. Tumwaandaa wachezaji kisaikolojia na kimwili, kuhakikisha wanacheza katika ubora na kupelekea matokeo ya ushindi. Ligi ni ngumu katika mechi chache zilizobaki, hivyo ni lazima tuhakikishe hatuangushi pointi.”
SOM HII ZAIDI: Yanga SC 2-0 Singida Black Stars fainali ya kibabe/ Mataji matano yakusanywa 2024/25/ Magoli na takwimu
Singida Black Stars
Naye Msemaji wa Singida Big Stars, Massanza JR amesema: “Katika siku za karibuni hatujawa na matokeo mazuri na maneno mengi yanasemwa juu yetu. Ikumbukwe walewale waliokuwa wanaidharau Azam FC na kuipa lawama, ndio wale wale wanaiombea mema siku hizi. Walewale waliodhani Coastal Union FC haijiwezi na kuipuuza, ndio walewale hawana la kusema juu yao zama hizi.
“Walewale walioichafua Dodoma Jiji FC kwa kuiita majina yote mabaya, ndio wale wale wanaoisifia kwa kila aina ya pambio leo hii. Walewale wenye makasiriko na Singida BS na kuitweza, ipo siku watachutama na kuipigia saluti. Wanaokudharau siku moja watakusalimia kwa heshima. Ijumaa kutakuwa na mechi kubwa.”
Hitimisho

Yanga SC vs Singida Black Stars ni mechi muhimu katika kuamua vita ya ubingwa msimu huu. Yanga SC wana presha kubwa kufuatia kasi ya watani zao Simba SC walio kwenye nafasi ya pili. Singida nao baada ya kuwa na nyakati ngumu katika siku za karibuni, wanatamani kufanya vizuri na kurejea kasi yao. Mechi ya Ijumaa inasubiriwa kwa hamu kuona nani amejipanga vizuri kuhakikisha anapata pointi 3 muhimu.
SOMA HII ZAIDI: Simba SC 1-3 Singida Black Stars Mei 31: Magoli yote nusu fainali CRDB Cup, H2H, Fainali Yanga SC vs Singida Black Stars

