Yanga SC na maajabu 2025/26 | Matokeo ya hivi punde, wafungaji na msimamo NBC Premier League

ByLunyamadizo Mlyuka

April 8, 2026
TRA United kiboko ya vigogo NBC Premier LeagueYahya MudathirYahya Mudathir
  • Pamba Jiji FC imeikabili Yanga SC Jumatano, Aprili 8 2026 ikipoteza kwa kufungwa magoli 3-0.
  • Yanga SC na maajabu 2025/26 NBC Premier League inaifukuzia unbeaten ya mechi 49.
  • Allan Okello ametoa hat trick ya asisti Uwanja wa CCM Kirumba, Mudathir afunga magoli mawili.
  • Msimamo na wafungaji wa hivi punde NBC Premier tumekusogezea hapa

Yanga SC na maajabu 2025/26 kwenye upatakinaji matokeo mechi 18 mfululizo haijafungwa NBC Premier League. Matokeo ya Aprili 8, 2026 Pamba Jiji FC 0-3 Yanga SC yanaonyesha mfanano na matokeo mzunguko wa kwanza ilipokuwa Yanga SC 3-0 Pamba Jiji FC. Wananchi wametoka kushinda magoli 3-0 Tanzania Prisons, Uwanja wa KMC Complex.

SOMA HII: Djigui Diarra wa Yanga SC amefungiwa mechi 3 na TPLB | Mechi atakazokosekana, waamuzi wafungiwa

Paisha Kindege cha SportPesa uvune mamilioni sasa hivi

Muda ni sasa kushinda mamilioni ukicheza mchezo wa Aviator. Ni rahisi sana kwa kila rubani kuvuna mamilioni. Cheza sasa upate mgao wako bila chenga ni rahisi sana

Sportpesa Aviator Rain Free Bets- Mil

Yanga SC na maajabu 2025/26 mechi 18 mfululizo

Yanga SC haijafungwa 2025/26
Mudathir Yahya kiungo wa Yanga SC.

Ni Yanga SC na maajabu 2025/26 ikicheza mechi ngumu bila kupoteza katika mechi za ushindani. Hapa tunakuletea matokeo ya hivi punde na wafunganji katika timu hiyo. Ikumbukwe kwamba hawa ni mabingwa mara 31 NBC Premier League.

Wanaifukuzia rekodi ya unbeaten 49 waliyoiandika kwa misimu mitatu. Hiyo ilianza 2020-21, 21-22 na ilivunjwa 2022/23 kwa kufungwa 2-1 na Ihefu ilikuwa Novemba 29, 2022. Je msimu huu itavunjwa na nani?

Wafungaji Pamba Jiji FC 0-3 Yanga SC

Wakati ubao wa CCM Kirumba, Aprili 8, 2026 ukisoma Pamba Jiji FC 0-3 Yanga SC, Yona Amos alianza langoni. Mudathir Yahya alifunga magoli mawili dakika ya 8 na 34. Maxi Nzengeli alifunga goli moja dakika ya 66. Pasi za magoli zilitengenezwa na Allen Okello.

Matokeo ya Yanga SC 2025/26

Haya hapa matokeo ya mechi zote za Yanga SC NBC Premier League. Pedro Goncalves ni Kocha Mkuu. Kipa namba moja ni Djigui Diarra.

Tarehe Timu (H) Matokeo Timu (A)
Aprili 8, 2026 Pamba Jiji FC   Yanga SC
April 4, 2026 Yanga SC 3-0   Tanzania Prisons
March 21, 2026 Mtibwa Sugar 1-1   Yanga SC
March 18, 2026 TRA United 0-0   Yanga SC
March 15, 2026 Azam FC 0-0   Yanga SC
March 12, 2026 Tanzania Prisons 0-1   Yanga SC
March 5, 2026 Singida Black Stars 0-3   Yanga SC
March 1, 2026 Yanga SC 0-0   Simba SC
Feb 25, 2026 Yanga SC 5-0   JKT Tanzania
Feb 22, 2026 Namungo FC 0-1   Yanga SC
Jan 27, 2026 Yanga SC 3-1 Dodoma Jiji  
Jan 19, 2026 Yanga SC 6-0   Mashujaa
Dec 7, 2025 Coastal Union 0-1   Yanga SC
Dec 4, 2025 Yanga SC 2-0   Fountain Gate
Nov 9, 2025 Yanga SC 4-1 KMC  
Oktoba 28, 2025 Yanga SC 2-0 Mtibwa Sugar  
Sep 30, 2025 Mbeya City 0-0   Yanga SC
Sep 24, 2025 Yanga SC 3-0   Pamba Jiji FC

SOMA HII: Wachezaji wanne wa Yanga SC warejea kazini | Taarifa mpya kuhusu Depu, ratiba 2025/26

cropped-Sportpesa-Aviator-Rain-Free-Bets-Mil-jpg- jpeg

Msimamo wa NBC Premier League 2025/26

Yanga SC haijafungwa 2025/26
Allan Okello kiungo wa Yanga SC 2025/26.

 Msimamo wa NBC Premier League uliobereshwa hivi punde. Yanga SC wanaongoza ligi na pointi 44. Pamba Jiji FC nafasi ya 6 kwenye msimamo.

POS MP W D L PTS
Yanga SC 18 13 5 0 44
Simba SC 16 10 5 1 35
3. Azam FC 17 8 9 0 33
4. JKT Tanzania 18 7 8 3 29
5.Singida Black Stars 18 8 4 6 28
6.Pamba Jiji FC 18 6 8 4 26
7.Dodoma Jiji FC 18 6 6 6 24
8. TRA United 17 6 5 6 23
9.Mtibwa Sugar 18 5 8 5 23
10.Namungo FC 18 5 7 6 22
11.Mashujaa FC 18 4 8 6 20
12.Mbeya City 17 4 4 9 16
13.Coastal Union 18 3 7 8 16
14.Fountain Gate 17 4 4 9 16
15.Tanzania Prisons 18 3 4 11 13
16. KMC FC 18 2 2 14 8

SOMA HII: Yanga SC Unbeaten NBC Premier League 2025/26: Haya hapa Matokeo yote na rekodi za Wananchi msimu huu, Azam hawavumi lakini wamo

Hitimisho

Yanga SC na maajabu 2025/26 na imefungwa magoli machache ambayo ni 3. Azam FC inafuatia ikiwa imecheza mechi 17 bila kupoteza msimu huu. Simba SC imepoteza mchezo mmoja ilikuwa dhidi ya Azam FC.

Share this: