Yanga SC kufungwa bado NBCDube na Pacome
  • Yanga SC kufungwa bado NBC Premier League mchezo wowote 2025/26
  • Matokeo ya kichapo cha TRA United 4-1 Azam FC yametibua rekodi
  • Ramadhan Salum Chobwedo afunga goli mbele ya matajiri Uwanja wa Sheikh Amri Abeid

Yanga SC kufungwa bado NBC Premier League 2025/26. Hii ni baada ya ubao wa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid kusoma TRA United 4-1 Azam FC. Ushindi wa wakusanya mapato unavunja rekodi ya matajiri kucheza mechi 21 bila kupoteza.

Je, bado hujashinda mamilioni ya aviator ‘Kindege’ cha SportPesa? Cheza ushinde mamilioni sasa

Changamka! sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

SOMA HII: Unbeaten 19 Azam F.C NBC Premier League | Yanga SC rekodi zinadunda

Aviator game promotional banner featuring a red propeller plane and a jackpot of 800,000,000.

Yanga SC kufungwa bado NBC Premier League mechi 21

Yanga SC kufungwa bado NBC
Air Manula Arusha

Ipo wazi Yanga SC kufungwa bado NBC Premier League baada ya kucheza mechi 21 bila kudondosha pointi tatu. Rekodi ya matajiri wa Dar Azam FC imevunjwa Arusha na vijana wa TRA United. Mei 8, 2026 vijana wa Chamanzi walipokea kichapo kutoka kwa wakusanya mapato.

Magoli kwenye mchezo huo yalifungwa na Ally Ng’anzi dakika ya 19, Ammy Mapaka alifunga mawili dakika ya 41 na 43 huku goli moja likifungwa na Ramadhan Salum Chobwedo. Goli pekee la Azam FC lilifungwa na Jephte Kitambala dakika ya 6.

Licha ya Azam FC kuanza kufunga mapema walikwama kulinda ushindi huo. Hiki ni kipigo kikubwa kwa waoka mikate hao kupigwa ndani ya msimu wa 2025/26. TRA United inaandika rekodi kuwa timu ya kwanza kuifunga Azam FC.

SOMA HII: Yanga SC Unbeaten NBC Premier League 2025/26: Haya hapa Matokeo yote na rekodi za Wananchi msimu huu, Azam hawavumi lakini wamo

Aviator game promotional banner featuring a red propeller plane and a jackpot of 800,000,000.

Je Yanga SC watadunda na rekodi yao?

Yanga SC kufungwa bado NBC
Ahamid Moallin

Mabingwa watetezi Yanga SC wanatarajiwa kucheza mchezo wa 22 leo dhidi ya Coastal Union. Je watadunda na rekodi yao ama itavunjwa. Ikumbukwe kwamba ndani ya ligi zilibaki timu mbili ambazo hazijapoteza baada ya mechi 21 ilikuwa ni Azam FC na Yanga SC.

Ikumbukwe kwamba Yanga SC imetoka kuachana na kocha mwezi huu. Pedro Goncalves aliyekuwa kocha mikoba yake ipo mikononi mwa Ahmid Moallin ambaye atakuwa mpaka mwisho wa msimu 2025/26. Timu hiyo inapambania kutetea taji ililotwaa 2024/25.

TRA United wameleta mshtuko mkubwa NBC Premier League

Mara baada ya mchezoTRA United wameleta mshtuko mkubwa kwa kutibua rekodi tamu ya Azam FC. Mwanzo mchezo ulionekana kuwa upande wa wageni mwisho wenyeji wakawa kwenye utawala. Mfungaji wa magoli mawili Ammy alichaguliwa kuwa Man of the Match.

SOMA HII: Yanga SC na maajabu 2025/26 | Matokeo ya hivi punde, wafungaji na msimamo NBC Premier League

Hitimisho

Yanga SC kufungwa bado NBC Premier licha ya kumtimua Pedro Goncalves Mei 6, 2026 kwenye benchi la ufundi. Mabingwa hao watetezi wanakibarua cha kusaka pointi tatu dhidi ya Coastal Union, Uwanja wa KMC Complex. Rekodi itatibuliwa ama itaendelea kudunda? Endelea kufuatilia Blog ya SportPesa.

Share this: