Fei TotoFei Toto
  • Unbeaten 19 Azam F.C NBC Premier League 2025/26
  • Feisal Salum ni King of Asisti ndani ya Tanzania Premier League akiwa amefikisha 7
  • Mechi 10 Azam FC wamepata sare kwenye msimamo nafasi ya 3

Unbeaten 19 Azam F.C NBC Premier League 2025/26 chini ya Kocha Mkuu, Florent Ibenge. Matokeo ya mchezo uliopita hivi punde Azam FC 3-0 JKT Tanzania. Huu ulikuwa ni mchezo wa 19 kwenye ligi uliochezwa Uwanja wa Azam Complex. Wanafikia rekodi ya Yanga SC ambayo nayo imecheza imechi 19 bila kupoteza.

SOMA TAARIFA HII: Azam FC Unbeaten 18 NBC Premier League 2025/26 | Yaikimbizia rekodi ya Yanga SC ligi kuu

Aviator game promotional banner featuring a red propeller plane and a jackpot of 800,000,000.

Unbeaten 19 Azam F.C NBC Premier League

Unbeaten 19 Azam F.C NBC Premier League
Feisal Salum kiungo mshambuliaji wa Azam FC: Source: Azam FC.

Wamefikisha Unbeaten 19 Azam F.C NBC Premier League 2025/26. Hii inatokana na kiwango kuendelea kuwa bora kwenye mechi za ushindani. Licha ya kutofungwa wanaongoza kwa kupata sare nyingi ambazo ni 10. Kwenye mechi 19 ushindi ni mechi 9 pekee.

SOMA HII: Yanga SC ina Unbeaten 27 CRDB Federation Cup | Mataji miaka minne mfululizo

Aviator game promotional banner featuring a red propeller plane and a jackpot of 800,000,000.

Matokeo ya Azam FC NBC Premier League 2025/26

TareheMechiMatokeo
17 Apr 2026Azam FC vs JKT Tanzania3-0
09 Apr 2026Mbeya City vs Azam FC0-0
05 Apr 2026Azam FC vs Simba SC0-0
01 Apr 2026Singida Black Stars vs Azam FC1-2
19 Mar 2026Mashujaa FC vs Azam FC0-0
15 Mar 2026Azam FC vs Yanga SC0-0
11 Mar 2026Dodoma Jiji FC vs Azam FC0-3
05 Mar 2026Tanzania Prisons vs Azam FC0-0
02 Mar 2026Pamba Jiji FC vs Azam FC2-2
25 Feb 2026Azam FC vs Mtibwa Sugar3-0
22 Feb 2026KMC FC vs Azam FC0-2
29 Jan 2026Azam FC vs TRA United2-0
20 Jan 2026Azam FC vs Fountain Gate0-0
17 Jan 2026Azam FC vs Coastal Union3-0
07 Dec 2025Simba SC vs Azam FC0-2
03 Dec 2025Azam FC vs Singida Black Stars0-0
09 Nov 2025Namungo FC vs Azam FC1-1
01 Oct 2025JKT Tanzania vs Azam FC1-1
24 Sep 2025Azam FC vs Mbeya City2-0

Ushindi mkubwa Azam FC NBC Premier League

Unbeaten 19 Azam F.C NBC Premier League
Idd Nado nyota wa Azam FC kwenye mchezo dhidi ya JKT Tanzania. Source: Azam FC.

Azam FC imepata ushindi mkubwa kwenye mechi 4. Katika mechi hizo walipata ushindi wa magoli 3-0 bila kuruhusu kufungwa. Kipa namba moja ni Aishi Manula aliyesajiliwa hapo akitokea kikosi cha Simba SC 2024/25.

TareheMechiMatokeo
17 Apr 2026Azam FC vs JKT Tanzania3-0
11 Mar 2026Dodoma Jiji FC vs Azam FC0-3
25 Feb 2026Azam FC vs Mtibwa Sugar3-0
17 Jan 2026Azam FC vs Coastal Union3-0

Feisal Salum King of Asisti

Kiungo mshambuliaji wa Azam FC, Feisal Salum ni King of Asisti NBC Premier League akiwa amefikisha 7. Mbali na kutengeneza pasi kwa wengine amefunga magoli 7. Jumla amehusika katika magoli 14 kati ya 26 yaliyofungwa na timu hiyo iliyo nafasi ya 3 kwenye msimamo.

SOMA HII: Ubingwa unanukia Yanga SC: Wananchi pengo la Pointi 8 kileleni, Simba SC, Azam FC hali tete!

Hitimisho

Unbeaten 19 Azam F.C NBC Premier League ndani ya 2025/26. Msimu wa 2013/14 Azam F.C ilitwaa taji la Ligi Kuu Tanzania Bara bila kupoteza mchezo. Rekodi hiyo itafikiwa kwa mara nyingine? Endelea kufuatilia SportPesa Blog kwa taarifa na matokeo zaidi.

Share this: