- Ramadhan Salum Chobwedo kumalizana na Simba SC?
- Chobwedo alisajiliwa na TRA United katika dirisha dogo akitokea KenGold
- Umri wake ni miaka 26 raia wa Tanzania ambaye anapenda kuvaa jezi namba 11
- Ahmed Ally Meneja wa Idara ya Habari Simba SC ataja sifa za kiungo TRA United
Anaitwa Ramadhan Salum Chobwedo mwenye miaka 26 kiungo wa TRA United anatajwa kuwa katika rada za Simba SC. Mchezaji huyo wa zamani wa KenGold amekuwa kwenye ubora katika mechi za hivi karibuni. Kutokana na uwezo huo tetesi zimekuwa zinamtaja kuhitajika na timu kubwa.
SOMA HII: Man of The Match Yanga SC 2025/26 | Dube anaongoza | Depu, Pacome, Maxi na Mudathiri tuzo
Cheza na ushinde sasa na ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa hivi
Hujashinda na kindege cha SportPesa? Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Bashiri na SportPesa uvune mkwanja sasa hivi.

Ramadhan Salum Chobwedo kumalizana na Simba SC?

Tetesi zinaeleza kwamba Ramadhan Salum Chobwedo kumalizana na Simba SC kwa ajili ya msimu ujao. Ni dau la milioni 180 linatajwa kuwekwa mezani kukamilisha usajili wake. Ikumbukwe kwamba mchezaji bado ana mkataba na TRA United hivyo mabosi wa msimbazi wanatakiwa kuvunja mkataba huo.
Mbali na Simba SC kutajwa kuwania saini yake Yanga SC wamekuwa wakitajwa. Pia Singida Black Stars hawa mwanzoni kabisa jicho lao linatajwa lilitua kwa kiungo huyo. Je kwa wababe hawa nani atainasa saini yake? Endelea kufuatilia SportPesa Blog kwa taarifa zaidi.
SOMA HII: TRA United yaibana mbavu Yanga SC NBC Premier League/ Highlights, statics, standings

Msikie Ahmed Ally kuhusu Chobwedo
Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari Simba SC ameweka wazi kuwa Chobwedo ni mchezaji hatari. Alibainisha kwamba amemfuatilia kwa ukaribu na kuona uwezo wake akiwa na mali. Aliongeza kwamba wanaouliza kuhusu usajili watapata majibu wakati ukifika.
“TRA United wana mchezaji mmoja anaitwa Chobwedo huyu ni mtu hatari akiwa na mali. Nimemuona kwenye michezo kadhaa, ana balaa. Unajua ana upara akishachemka unaona kabisa jasho la kazi linapita pale ni mchezaji mzuri tunamheshimu,”.
Orodha ya wachezaji walioongeza mikataba Msimbazi

Yusuph Kagoma
Yusuph Kagoma ni kiungo mkabaji mwenye miaka 29. Amejiunga na Simba SC akitokea Fountain Gate alipokuwa msimu wa 2023/24. Aliwahi kucheza Geita Gold 2023/24.
Awali kabla ya kusajiliwa na Simba SC alikuwa anatajwa kuwa katika rada za Yanga SC. Sakata lake la kusaini Yanga SC lilizuia gumzo na mwisho mchezaji akasalia Msimbazi.
Kutokana na kiwango bora anachoonyesha akiwa uwanjani, Machi 8,2026 aliongeza kandarasi nyingine. Hivyo bado ataendelea kusalia ndani ya kikosi cha Simba SC baada ya kuongeza kandarasi ya miaka miwili hadi 2028.
Mbali na kukaba ana uwezo wakufunga magoli. Katika mchezo wa Simba SC 3-0 TRA United, Kagoma alifunga goli moja. Magoli mengine yalifungwa na Seleman Mwalimu na Neo Maema.
Rushine De Reuck
Rushine De Reuck ni beki wa kati alipendekezwa na Fadlu Davids aliyekuwa kocha wa Simba SC 2024/25. Ana miaka 30. Ni raia wa Afrika Kusini ameongeza kandarasi ya mkataba wa mwaka mmoja mpaka 2027.
Beki huyo alijiunga na Simba SC akitokea Mamelodi Sundowns. Ni chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Steve Barker. Katika mchezo dhidi ya TRA United alichaguliwa kuwa mchezaji bora ikiwa ni tuzo yake ya 3.
Marchi 8 2026 taarifa rasmi ya kuongeza mkataba wake ilikuwa wazi. Baada ya mechi 14 safu ya ulinzi iliruhusu magoli. Ni pointi 31 imekusanya ikiwa nafasi ya pili kwenye msimamo.
Kauli ya Rushine unyamani
“Nimefurahi kuendelea kuwa ndani ya kikosi cha Simba SC. Bado tutaendelea kushirikiana na wachezaji ili kupata matokeo. Mashabiki waendelee kuwa nasi,”.
Ellie Mpanzu

Winga Ellie Mpanzu ni raia wa DRC Congo alikuwa anatajwa kuwa katika rada za Yanga SC. Ametengeneza jumla ya pasi 5 za magoli. Alifunga goli la ushindi mchezo dhidi ya Singida Black Stars akitokea benchi.
Machi 23,2026 taarifa zilitolewa kuhusu mkataba wake. Rais wa Simba SC, Mohammed Dewji alihusika kwa asilimia kubwa kufanikisha jambo hilo. Ni miaka wa miaka miwili Mpanzu alisaini.
SOMA HII: Fountain Gate (0) vs Simba SC (3) NBC Premier League | Highlights, goal score, H2H
Hitimisho
Ramadhan Salum Chobwedo ni jina ambalo linatajwa mitaa ya Kariakoo. Kwenye mchezo dhidi ya Yanga SC kiungo huyu alitwaa tuzo ya Man of the Match. Dhidi ya mnyama aliwavuruga mabeki mwanzo mwisho.

