Ni Mashujaa FC vs Simba SC NBC Premier League 2025/26 mchezo unaofuata kwenye ratiba. H2H katika mechi 5 walizokutana Sokwe hajapata ushindi huku mnyama akiwa hajapoteza kwenye ligi. Msimu huu Mashujaa FC imekutana mara moja na Simba SC ikipoteza kwa kufungwa magoli 2-0. Mei 14, 2026 wababe hawa wanakutana Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma saa 10:15 jioni.
SOMA HII: Mashujaa FC: Muhtasari, Ratiba, Matokeo, Kikosi, Usajili, Takwimu, na Msimamo wa Ligi
Je, Unataka kushinda pesa? Cheza ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa
Ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege kupitia kampuni bora ya kubashiri ya SportPesa. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

Mashujaa FC vs Simba SC NBC Premier League 2025/26

Hatumwi mtoto dukani Mashujaa FC vs Simba SC NBC Premier League kutokana na kila timu kupambania malengo. Wenyeji wanapiga hesabu kumaliza ligi ndani ya 5 na kuvunja rekodi yakutoshinda mbele ya mnyama. Wageni wanapiga hesabu kuongeza vita kuwania ubingwa dhidi ya Yanga SC. Hili linaongeza ugumu ndani ya dakika 90.
H2H Mashujaa FC vs Simba SC NBC Premier League
| Tarehe | Mechi | Matokeo |
|---|---|---|
| 03/02/2023 | Mashujaa FC vs Simba SC | 0-1 |
| 15/03/2024 | Simba SC vs Mashujaa FC | 2-0 |
| 01/11/2024 | Mashujaa FC vs Simba SC | 0-1 |
| 02/05/2025 | Simba SC vs Mashujaa FC | 2-1 |
| 29/01/2026 | Simba SC vs Mashujaa FC | 2-0 |
Msimamo wa ligi Mashujaa FC vs Simba SC
| Timu | Nafasi | Mechi | Pointi | Ushindi | Sare | Vipigo | Magoli yaliyofungwa |
|---|---|---|---|---|---|---|---|
| Mashujaa FC | 9 | 22 | 26 | 5 | 11 | 6 | 11 |
| Simba SC | 2 | 22 | 49 | 14 | 7 | 1 | 39 |
Mnyama yupo nafasi ya pili kwenye msimamo. Mchezo mmoja amepoteza kati ya 22 anakutana na Mashujaa FC ambao wamepoteza mechi 6. Nani kuibuka na ushindi Lake Tangayika?
SOMA HII: Simba SC vs Mashujaa FC, mwenye kisu kikali kula nyama dakika 90

Maoni ya makocha Mashujaa FC vs Simba SC
Julio, Kocha Mkuu wa Mashujaa FC amesema wamejipanga kupata pointi tatu mbele ya Simba SC. Kocha huyo ameongeza kuwa hawatambui wachezaji wa timu pinzani anaamini atakutana nao uwanjani. Aliongeza kuwa hakuna timu ambayo ni nyepesi kwenye ligi.
“Sijui kuhusu wachezaji wa Simba SC kwa kuwa sijawahi kuhudhuria mazoezi yao. Ambacho ninatambua tutakutana uwanjani kusaka pointi tatu. Wachezaji wapo tayari na tunaamini utakuwa ni mchezo wenye ushindani.
Seleman Matola, kocha msaidizi wa Simba SC amesema wamefanya maandalizi kwa mchezo huo. Ameongeza kwamba licha ya ugumu wa ratiba wapo tayari kuwakabili Mashujaa FC. Matola amewaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi uwanjan.
“Tumefanya maandalizi mazuri kuwakabili Mashujaa FC. Tunatambua kwamba hautakuwa mchezo mwepesi. Kila timu inahitaji ushindi hivyo tutapambana kupata matokeo mazuri,”.
SOMA HII: Simba SC 2-0 Mashujaa FC Ligi Kuu Bara NBC: Mnyama afufuka! Highlits,Matokeo, Ratiba
Hitimisho
Mashujaa FC vs Simba SC NBC Premier League 2025/26 kupigwa ugenini, Kigoma mwisho wa reli. Hii ni lala salama kwenye mechi za ligi. Ni vita ya kumsaka bingwa na timu ambazo zitashuka daraja. Je Mashujaa FC wataonyesha ushujaa mbele ya mnyama? Endelea kufuatilia SportPesa Blog kwa taarifa na matokeo zaidi.

