Simba SC vs Tanzania Prisons | Ratiba, matokeo, msimamo, NBC Premier League, utabiri, Livescore, h2h, na Habari za timu
- Simba SC vs Tanzania Prisons moto utawaka kesho Jumapili 10/5/2026, ni katika mfululizo wa mechi za Ligi Kuu Bara (NBC Premier League).
- Kwa mara ya kwanza msimu huu Simba SC watatumia Uwanja wa KMC Complex, kama uwanja wao wa nyumbani.
- Hii ni mara baada ya muda mrefu, kutumia Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo.
- Ikumbukwe mara ya mwisho timu hizo kukutana matokeo yalikuwa Tanzania Prisons 0-2 Simba SC tarehe 22/2/2026.
Simba SC vs Tanzania Prisons kitawaka kesho Jumapili 10/5/2026, ni katika mfululizo wa mechi za Ligi Kuu Bara (NBC Premier League). Mechi hii itapigwa kwenye Uwanja wa KMC, ambapo hii inakuwa mara ya kwanza msimu huu kwa Simba SC kutumia uwanja huo kama uwanja wao wa nyumbani. Hii ni mara baada ya muda mrefu, kutumia Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo. Ikumbukwe mara ya mwisho timu hizo kukutana matokeo yalikuwa Tanzania Prisons 0-2 Simba SC tarehe 22/2/2026.
Fuatilia mwenendo wote wa mashindano ya Ligi Kuu Bara ‘NBC Premier League’ 2025/26; Ratiba, matokeo, mechi, magoli na habari za papo kwa papo kupitia SportPesa Blog.
Je, unataka kushinda mamilioni? Unaweza kushinda mpaka Shilingi Milioni 800 na SportPesa
Wengi tayari wamevuna mamilioni kupitia mchezo wa Kindege yaani ‘Aviator’ ya SportPesa. Wewe unasubiri nini? Nafasi ni yako cheza Aviator na kushinda mpaka Shilingi Milioni 800 sasa kwa kubonyeza picha hii chini.

Aviator: Paisha kindege ushinde mpaka zaidi ya 800,000,000.
Simba SC vs Tanzania Prisons h2h

Timu hizi zimekutana katika mechi 28 za ushindani, ambapo Simba SC wameshinda mechi 18, na Tanzania Prisons wameshinda mechi 6. Mechi 4 katika mikutano yao ziliisha kwa matokeo ya sare. Mchezo huu ni muhimu kwa Simba SC katika kuimarisha dhamira yao ya kupambana na Yanga SC, katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu Bara.
SOMA HII PIA: Ratiba ya Simba SC NBC Premier League 2025/26 ni moto | Msimamo, Mzizima Dabi, Kariakoo Dabi
Simba kwenye nafasi ya 2 msimamo wa Ligi Kuu Bara (NBC Premier League)
Mpaka sasa Simba SC wanakamatia nafasi ya 2 kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara (NBC Premier League), hii ni baada ya kukusanya pointi 46 katika michezo 21. Simba SC imeshinda mechi 13, sare mechi 7 na kupoteza mechi moja tu. Katika michezo hiyo Simba imefunga mabao 35 na kuruhusu mabao 9 tu. Hii inaelezewa na jedwali lifuatalo;
| Nafasi | Timu | Mechi | Ushindi | Sare | Vipigo | Magoli ya Kufunga/Kufungwa | Tofauti ya Magoli | Pointi |
|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
| 1 | Young Africans | 21 | 15 | 6 | 0 | 47:5 | +42 | 51 |
| 2 | Simba | 21 | 13 | 7 | 1 | 35:9 | +26 | 46 |
| 3 | Azam | 22 | 11 | 10 | 1 | 31:9 | +22 | 43 |
| 4 | Singida Black Stars | 22 | 10 | 5 | 7 | 29:23 | +6 | 35 |
| 5 | TRA United | 22 | 9 | 6 | 7 | 27:20 | +7 | 33 |
| 6 | JKT Tanzania | 21 | 8 | 8 | 5 | 21:21 | 0 | 32 |
| 7 | Pamba | 21 | 7 | 8 | 6 | 22:22 | 0 | 29 |
| 8 | Dodoma Jiji | 21 | 7 | 7 | 7 | 19:21 | -2 | 28 |
| 9 | Mashujaa | 22 | 5 | 11 | 6 | 11:17 | -6 | 26 |
| 10 | Namungo | 22 | 5 | 9 | 8 | 17:23 | -6 | 24 |
| 11 | Mtibwa Sugar | 22 | 5 | 8 | 9 | 16:29 | -13 | 23 |
| 12 | Coastal Union | 22 | 5 | 7 | 10 | 20:27 | -7 | 22 |
| 13 | Fountain Gate | 21 | 6 | 4 | 11 | 14:30 | -16 | 22 |
| 14 | Mbeya City | 21 | 5 | 6 | 10 | 18:31 | -13 | 21 |
| 15 | Tanzania Prisons | 21 | 3 | 5 | 13 | 11:28 | -17 | 14 |
| 16 | Kinondoni MC | 21 | 2 | 3 | 16 | 8:32 | -24 | 9 |
Ratiba ya mechi 5 zijazo za Simba SC
Zimesalia mechi chache kumaliza msimu huu wa 2025/26, na hapa chini ni jedwali la Ratiba ya Simba ya mechi zilizosalia. Kila mechi hapa inabeba pointi 3 muhimu katika vita ya ubingwa wa ligi. Simba SC wanataka kushinda ubingwa huu baada ya kushuhudia watani wao wakiubeba misimu 4 mfululizo.
| Tarehe | Muda | Mechi |
|---|---|---|
| 10 Mei 2026 | 19:00 | Simba vs Tanzania Prisons |
| 14 Mei 2026 | 16:15 | Mashujaa vs Simba |
| 21 Mei 2026 | 18:30 | Coastal Union vs Simba |
| 24 Mei 2026 | 18:15 | Simba vs Dodoma Jiji |
| 14 Juni 2026 | 19:00 | Simba vs Pamba |
| 18 Juni 2026 | 16:00 | Mbeya City vs Simba |
| 24 Juni 2026 | 16:00 | Mtibwa Sugar vs Simba |
| 27 Juni 2026 | 16:00 | Simba vs Singida Black Stars |
| 30 Juni 2026 | 16:00 | Simba vs Kinondoni MC |
SOMA HII ZAIDI: Mzizima Dabi yaiachia maumivu Simba SC 2025/26 | Highlights, msimamo, h2h, ratiba mechi zijazo
Simba SC vs Tanzania Prisons makocha wanasemaje?
Simba SC

Akizungumzia mchezo huo kocha Msaidizi wa Simba SC, Seleman Matola amesema: “Hatuiangalii Prisons katika nafasi waliyopo, tunaangalia Prisons tunapokutana nao wanatupa mchezo wa namna gani. Mchezo kati yetu haujawahi kuwa mwepesi, hii ni kutokana na ubora walionao. Lakini malengo yetu ni kuchukua pointi 3 muhimu.”
Tanzania Prisons
Naye Kocha wa Tanzania Prisons, Shadrack Nsajigwa amesema: “Kikosi cha timu yetu kipo kamili na tayari kuwakabili Simba SC kutokana na maandalizi tuliyofanya. Tumeusoma ubora wa mpizani wetu na tupo tayari kuzipigania alama tatu muhimu. Tunazitaka pointi hizi ili kuzidi kujiimarisha kwenye enezo zuri la msimamo.”
SOMA HII PIA: Simba SC vs Coastal Union NBC Premier League Aprili 2, 2026 | H2H, msimamo, live score
Kuhusu Simba SC kuhamia Uwanja wa KMC Complex

Uongozi wa Simba SC alhamisi hii 7/5/2026 walitangaza rasmi kurejea Uwanja wa KMC. Simba SC wamerejea Uwanja wa KMC, baada ya muda mrefu msimu kutumia Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo. Akizungumzia uamuzi huo, Kocha Matola amesema kusema timu yao imehamia KMC Complex kwa kuwa uwanja Meja Jenerali Isamuhyo unaonekana kuzidiwa na uharibifu wa eneo la kuchezea.
Hitimisho

Simba SC vs Tanzania Prisons ni mchezo ambao umekuwa ukitoa upinzani mkubwa, mara zote wanapokutana. Simba SC wanaingia katika mchezo huu wakiwa kwenye fomu nzuri, hii ni baada ya kuichapa JKT Tanzania bao 1-0. Kama Simba SC wataibuka na ushindi katika mchezo huu, watakuwa wamefikisha pengo la pointi 9 dhidi ya Azam walio nafasi ya 3.

