Real Madrid Vs BarcelonaReal Madrid Vs Barcelona
  • Barcelona vs Real Madrid ni El Clasico yamoto itakayopigwa kesho Jumapili.
  • Mchezo huu utakaopigwa Uwanja wa Camp Nou, unakuja kipindi ambacho, inaelezwa hali sio nzuri kwenye kambi ya Real Madrid.
  • Hii ni baada ya kuvuja kwa taarifa kuwa kumetokea ugomvi mkubwa kati ya baadhi ya mastaa wa timu hiyo, huku kiungo Aurelien Tchouameni na nahodha Federico Valverde wakiripotiwa kupigana na kuumizana.
  • Ikumbukwe kuwa ikiwa Barcelona watashinda basi, mchezo huu utaamua ubingwa wa La Liga.

Barcelona vs Real Madrid mechi kali ya El Clasico itakayopigwa kesho Jumapili. Mechi hii itakayopigwa Uwanja wa Camp Nou, inakuja kipindi ambacho inaelezwa hali sio nzuri kwenye kambi ya Real Madrid. Hii ni baada ya kuvuja kwa taarifa kuwa kumetokea ugomvi mkubwa kati ya baadhi ya mastaa wa timu hiyo, huku kiungo Aurelien Tchouameni na nahodha Federico Valverde wakiripotiwa kupigana na kuumizana. Mechi hii pia itaamua ubingwa wa La Liga ikiwa Barcelona wataibuka na ushindi.

Fuatilia mwenendo wote wa mashindano ya UEFA Champions League 2025/26; Ratiba, matokeo, mechi, magoli na habari za papo kwa papo kupitia SportPesa Blog.

Unataka kushinda mamilioni? Unaweza kushinda mpaka Shilingi Milioni 800 na SportPesa

Wengi tayari wamevuna mamilioni kupitia mchezo wa Kindege yaani ‘Aviator’ ya SportPesa. Wewe unasubiri nini? Nafasi ni yako cheza Aviator na kushinda mpaka Shilingi Milioni 800 sasa kwa kubonyeza picha hii chini.

SportPesa Aviator Challenge

Aviator: Paisha kindege ujishindie mpaka zaidi ya Milioni 800,000,000

Barcelona vs Real Madrid h2h

Real Madrid 3-2 Barcelona: Goals and highlights - LaLiga 23/24
Real Madrid 3-2 Barcelona: Goals and highlights – LaLiga 23/24

Timu hizi zimekutana katika michezo 263 ya mashindano rasmi, ambapo Real Madrid wameshinda mechi 106 na Barcelona wameshinda mechi 105. Mechi 52 katika mikutano yao ziliisha kwa matokeo ya sare. Mabao 883 yamefungwa katika idadi hiyo ya mechi, ambapo Real Madrid wamefunga mabao 447 na Barcelona wakifunga mabao 436.

SOMA HII PIA: Barcelona vs Real Madrid El Clasico ya 261 kinawaka leo: H2H, Vikosi, Uchambuzi, Utabiri

Vikosi vinavyotarajiwa kuanza Barcelona vs Real Madrid

Barcelona

Kipa: J Garcia

Walinzi: Kounde, Cubarsi, Martin, Cancelo

Viungo: E Garcia, Pedri, Rashford, Gavi, Fermin

Mshambuliaji: Lewandowski

Real Madrid

Kipa: Courtois

Walinzi: Alexander-Arnold, Rudiger, Huijsen, F Garcia

Viungo: Camavinga, Tchouameni, Pitarch, Bellingham

Washambuliaji: Vinicius, Mbappe

Taarifa za timu

Raphinha na ubingwa
Raphinha na ubingwa

Barcelona wako kileleni mwa msimamo wa La Liga kwa tofauti ya pointi 11 dhidi ya Real Madrid walio nafasi ya pili, ikiwa watashinda leo watatangazwa rasmi mabingwa. Kwenye La Liga Barcelona wamefanikiwa kushinda mechi 29, sare 1 na kupoteza mechi 4 pekee kati ya michezo 34. Takwimu zinaonyesha kuwa, wameibuka na ushindi katika mechi zao 10 zilizopita za La Liga.

Mchezo wa mwisho baina ya timu hizi kukutana uliopigwa 11/1/2026 kwenye fainali ya Spanish Super Cup, Barcelona walishinda mabao 3-2. Kabla ya hapo, Real Madrid waliichapa Barcelona 2-1 kwenye mchezo wa mzunguko wa 1 wa La Liga uliochezwa Oktoba, 2025. Katika mechi 6 zilizopita za timu hizi kwenye mashindano yote, Barcelona wameshinda 5. Barcelona watatamani kutangaza ubingwa mbele ya mahasimu wao wa jadi, lakini hata wakipoteza bado watabaki kileleni. Tofauti ya itapungua hadi pointi 8 huku kukiwa na mechi 3 pekee zilizobaki.

SOMA HII ZAIDI: Barcelona VS Real Madrid-El Clásico ya kombe la Mfalme.

Sakata la Aurelien Tchouameni vs Federico Valverde

Barcelona vs Real Madrid (-)
Barcelona vs Real Madrid

Kwa upande wa Real Madrid, wiki hii imekuwa na sintofahamu baada ya nahodha Federico Valverde, kuhusika kwenye ugomvi na kiungo Aurelien Tchouameni. Valverde alipelekwa hospitali kutokana na tukio hilo, ambapo ameripotiwa kupata majeraha ya Kichwa. Majeraha hayo yanatarajiwa kumuweka nje kwa takribani wiki mbili. Wakati hayo yakiendelea inaelezwa kuwa mshambuliaji, Kylian Mbappe anadaiwa kuwa na mahusiano yasiyo mazuri na baadhi ya wachezaji wenzake.

Hali ya majeruhi

Barcelona

Wenyeji watamkosa nyota wao chipukizi, Lamine Yamal ambaye atakosekana hadi mwisho wa msimu, kutokana na majeraha ya misuli ya nyuma ya paja. Hata hivyo, beki Andreas Christensen amerejea mazoezini baada ya kupona jeraha la goti. Kocha Hansi Flick ana maamuzi kadhaa muhimu ya kufanya kuhusu kikosi chake, huku Eric Garcia akitajwa kuweza kucheza kiungo pamoja na Pedri na Gavi.

Fermin Lopez anatarajiwa kuanza, huku Marcus Rashford na Robert Lewandowski pia wakipewa nafasi kikosini. Raphinha ambaye amepona majeraha, huenda akaanzia benchi. Hii ni kama sehemu ya kuchukua tahadhari.

Real Madrid

Rodrygo baada ya upasuaji
Rodrygo baada ya upasuaji

Kwa upande wa Real Madrid, Valverde hatakuwepo kutokana na majeraha aliyopata kwenye ugomvi huo, lakini Tchouameni hajafungiwa hivyo anaweza kuanza mchezo. Golikipa Thibaut Courtois pamoja na Mbappe wamethibitishwa kuwa fiti, baada ya kuwa na matatizo ya kiafya hivi karibuni. Hata hivyo, Rodrygo, Arda Guler, Eder Militao, Dani Carvajal na Ferland Mendy wote wameondolewa kwenye mchezo huu kutokana na majeraha.

SOMA HII PIA: BARCELONA VS REAL MADRID 26/4/2025, USO KWA USO FAINALI COPA DEL REY

Utabiri na hitimisho

Barcelona vs Real Madrid ni mchezo unaotajwa kuwa dabi maarufu zaidi duniani. Licha ya mambo ya nje ya Uwanja yanayoripotiwa kwa sasa, lakini mchezo huu unasalia kuwa mchezo mgumu. Mchezo huu unatabiriwa kuisha kwa sare kama kila timu itacheza kwa ubora unaotarajiwa, na kusaka matokeo muhimu.

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.