- Kocha mpya Yanga SC ni nani? Hili ndio swali kubwa kwa wadau wa soka na hasa mashabiki wa Yanga SC.
- Hii ni baada ya siku moja tu, tangu uongozi wa timu hiyo ulipotangaza kumfuta kazi aliyekuwa kocha wao mkuu, Pedro Goncalves.
- Kocha Goncalves aliyempokea kijiti cha kocha, Roman Folz, alifutwa kazi muda mfupi baada ya kuwaongoza Wananchi kupata matokeo ya KMC 0-1 Yanga SC.
- Majina mbalimbali tayari yamehusishwa kuchukua mikoba ya wa kocha mpya Yanga SC akiwemo kocha, João Paulo Mota Maria na Makala hii inamchambua kocha huyo.
Nani kuwa kocha mpya Yanga SC? Hili ndilo swali kubwa miongoni mwa wadau wa soka na hasa mashabiki wa Yanga SC. Hii inakuja ikiwa ni siku moja tu, imepita tangu uongozi wa timu hiyo ulipotangaza kumfuta kazi aliyekuwa kocha wao mkuu, Pedro Goncalves. Kocha huyo aliyempokea kijiti kocha, Roman Folz, alifutwa kazi muda mfupi baada ya kuiongoza timu hiyo kupata matokeo ya KMC 0-1 Yanga SC. Majina mbalimbali tayari yamehusishwa kuwa kocha mkuu mpya, akiwemo kocha João Paulo Mota Maria.
Fuatilia mwenendo wote wa mashindano ya Ligi Kuu Bara ‘NBC Premier League’ 2025/26; Ratiba, matokeo, mechi, magoli na habari za papo kwa papo kupitia SportPesa Blog.
Je, unataka kushinda mamilioni? Unaweza kushinda mpaka Shilingi Milioni 800 na SportPesa
Wengi tayari wamevuna mamilioni kupitia mchezo wa Kindege yaani ‘Aviator’ ya SportPesa. Wewe unasubiri nini? Nafasi ni yako cheza Aviator na kushinda mpaka Shilingi Milioni 800 sasa kwa kubonyeza picha hii chini.

Aviator: Paisha kindege ushinde mpaka zaidi ya 800,000,000.
Kocha mpya Yanga SC ni João Mota? Je, Joao Mota ni nani?

Jina lake kamili ni João Paulo Mota Maria, ni mzaliwa wa Portugal Lisboa, nchini Ureno ambapo alizaliwa tarehe 16/09/1966, hii inamfanya sasa kuwa na umri wa miaka 59. Kocha huyu ana wastani wa 0.64 kufundisha timu. Kocha huyu anapendelea zaidi soka lenye balansi ya kulinda na kushambulia, ambapo hupendelea mfumo wa 4-2-3-1. Kocha huyu anasimamiwa na taasisi ya uwakala ya Arab Africano na kwa sasa anafundisha kikosi cha Al Ittihad inayoshiriki Ligi daraja la pili Falme za kiarabu UAE, ambayo alijiunga nayo tarehe 22/9/2025.
SOMA HII PIA: Romain Folz kocha mpya Yanga SC mwenye CV kubwa | Wachezaji wenye uhakika 2025/26
Historia yake kisoka

Kocha Joao Mota kama ilivyo kwa makocha wengine, naye amepata nafasi ya kucheza soka katika ngazi mbalimbali. Timu yake ya mwisho ya klabu kuichezea ni Lagoa ya Ureno, japo timu aliyoichezea mechi nyingi zaidi ni União Madeira ya jukuhuko Ureno. Rasmi alistaafu kucheza soka tarehe 01/04/2000. Jedwali hilli linaonyesha historia ya timu alizowahi kucheza kocha huyo, enzi ya ujana wake;
| Msimu | Tarehe | Klabu Aliyoondoka | Klabu Aliyojiunga | Aina ya Uhamisho |
|---|---|---|---|---|
| 1999/2000 | 01 Aprili 2000 | Lagoa | Kustaafu Soka | Kustaafu |
| 1999/2000 | 01 Julai 1999 | Beja | Lagoa | Uhamisho wa Bure |
| 1998/1999 | 01 Julai 1998 | Câmara Lobos | Beja | Uhamisho wa Bure |
| 1995/1996 | 01 Julai 1995 | Torreense | Câmara Lobos | Uhamisho wa Bure |
| 1993/1994 | 01 Julai 1993 | Montijo | Torreense | Uhamisho wa Bure |
| 1992/1993 | 01 Julai 1992 | Louletano | Montijo | Uhamisho wa Bure |
| 1991/1992 | 01 Julai 1991 | Leiria | Louletano | Uhamisho wa Bure |
| 1990/1991 | 01 Julai 1990 | União Madeira | Leiria | Ada Haikujulikana |
| 1988/1989 | 01 Julai 1988 | Sporting CP | União Madeira | Ada Haikujulikana |
| 1987/1988 | 30 Juni 1988 | União Madeira | Sporting CP | Mwisho wa Mkopo |
| 1987/1988 | 01 Julai 1987 | Sporting CP | União Madeira | Uhamisho wa Mkopo |
| 1986/1987 | 30 Juni 1987 | O Elvas | Sporting CP | Mwisho wa Mkopo |
| 1986/1987 | 02 Julai 1986 | Sporting CP | O Elvas | Uhamisho wa Mkopo |
| 1986/1987 | 01 Julai 1986 | Sporting U19 | Sporting CP | Kupandishwa Kikosi cha Wakubwa |
| 1985/1986 | 30 Juni 1986 | União Madeira | Sporting U19 | Mwisho wa Mkopo |
| 1985/1986 | 01 Julai 1985 | Sporting U19 | União Madeira | Uhamisho wa Mkopo |
| 1984/1985 | 01 Julai 1984 | Barreirense U19 | Sporting U19 | Ada Haikujulikana |
SOMA HII ZAIDI: Kocha mpya Yanga SC huyu hapa, kuiwahi mechi ya Yanga SC vs Silver Strikers Jumamosi?
Historia ya baadhi ya timu alizowahi kufundisha

Kocha, João Paulo Mota Maria ni mzoefu wa soka la kimataifa ambapo, amewahi kuwa kocha wat imu nyingi kama inavyoonyeshwa kwenye jedwali hili;
| Msimu / Kipindi | Klabu / Timu | Nafasi | Tarehe ya Kuanza | Tarehe ya Kuondoka | Mechi | Pointi kwa Mechi (PPM) |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2025/2026 | Al-Ittihad SC | Kocha Mkuu | 22 Septemba 2025 | Anaendelea | – | 0.00 |
| 2025/2026 | Saham Club | Kocha Mkuu | 31 Agosti 2025 | 21 Septemba 2025 | 2 | 0.50 |
| 2024/2025 | Al-Hussein SC | Kocha Mkuu | 25 Septemba 2024 | 19 Aprili 2025 | 22 | 2.09 |
| 2024/2025 | Al-Tadamon SC | Kocha Mkuu | 1 Julai 2024 | 24 Septemba 2024 | – | 0.00 |
| 2023/2024 | Sudan National Football Team | Mratibu wa Timu | 9 Mei 2024 | 30 Juni 2024 | – | 0.00 |
| 2023/2024 | Al-Jabalain FC | Kocha Mkuu | 11 Februari 2024 | 30 Aprili 2024 | 6 | 1.00 |
| 2022/2023 – 2023/2024 | Al-Hussein SC | Kocha Mkuu | 15 Aprili 2023 | 9 Februari 2024 | – | 0.00 |
| 2022/2023 | GE Juventus | Kocha Mkuu | 30 Machi 2023 | 6 Aprili 2023 | – | 0.00 |
| 2022/2023 | DC Motema Pembe | Kocha Mkuu | 18 Desemba 2022 | 19 Januari 2023 | – | 0.00 |
| 2021/2022 | Al-Hilal Club | Kocha Mkuu | 10 Novemba 2021 | 30 Juni 2022 | 6 | 0.67 |
| 2021/2022 | Al-Hilal Club | Kocha Msaidizi | 1 Julai 2021 | 9 Novemba 2021 | – | 0.00 |
| 2020/2021 | Botafogo FC Buéa | Kocha Mkuu | 1 Mei 2021 | 30 Juni 2021 | – | 0.00 |
| 2020/2021 | EC Tigres do Brasil | Kocha Mkuu | 1 Januari 2021 | 30 Aprili 2021 | – | 0.00 |
| 2020/2021 | Rio Branco FC | Kocha Mkuu | 1 Julai 2020 | 30 Novemba 2020 | – | 0.00 |
| 2019/2020 | Saudi Arabia U20 | Kocha Mkuu | 1 Novemba 2019 | 30 Juni 2020 | – | 0.00 |
| 2018/2019 | Rio Branco FC | Kocha Mkuu | 1 Desemba 2018 | 30 Juni 2019 | 1 | 1.00 |
| 2017/2018 – 2018/2019 | Portuguesa U20 | Kocha Mkuu | 1 Machi 2018 | 30 Septemba 2018 | – | 0.00 |
| 2017/2018 | AD Guarulhos | Kocha wa Vijana | 1 Septemba 2017 | 28 Februari 2018 | – | 0.00 |
| 2016/2017 | Al-Khaleej FC | Kocha Mkuu | 1 Januari 2017 | 30 Juni 2017 | – | 0.00 |
| 2014/2015 – 2015/2016 | Dibba Al-Hisn SC | Kocha Mkuu | 1 Julai 2014 | 30 Juni 2016 | – | 0.00 |
| 2012/2013 – 2013/2014 | AA Aparecidense | Kocha Msaidizi | 1 Januari 2013 | 30 Septemba 2013 | – | 0.00 |
| 2011/2012 | Hatta Club | Kocha Mkuu | 1 Julai 2011 | 30 Juni 2012 | – | 0.00 |
| 2010/2011 | SC Farense | Kocha Msaidizi | 1 Oktoba 2010 | 30 Juni 2011 | – | 0.00 |
| 2009/2010 – 2010/2011 | SC Farense U19 | Kocha Mkuu | 1 Julai 2009 | 30 Septemba 2010 | – | 0.00 |
| 2007/2008 – 2008/2009 | SC Farense Youth 17 | Kocha Mkuu | 1 Julai 2007 | 30 Juni 2009 | – | 0.00 |
Hitimisho

Huku kitendawili cha ni nani kuchukua kijiti cha Kocha mpya Yanga SC kikizidi kushika hatamu, uongozi wa timu hiyo umetangaza kuwa kwa sasa timu hiyo itakuwa chini ya makocha Makocha, Abdihamid Moalin na Patrick Mabedi. Makocha hao watafanya kazi kama ‘Co-Headcoaches’ yaani wote wawili watakuwa makocha wakuu wa timu yetu. Kocha msaidizi atasalia, Matthew Silva ambaye alikuwa kocha msaidizi wa Pedro.
SOMA HII PIA: Roman Folz kufukuzwa Yanga SC, kocha mpya huyu hapa

