Romain Folz kocha mpya wa Yanga SC CV yake kubwa ina balaa zito akiwa ni kocha kijana. Kocha huyo ni mrithi wa mikoba ya Miloud Hamdi aliyekuwa Kocha Mkuu wa Yanga SC 2024/25. Miloud alipewa Thank You Julai 3 2025 hivyo hatakuwa ndani ya Yanga SC msimu wa 2025/26 amepata changamoto mpya Klabu ya Ismaily SC ya Misri.

Soma hii:Lassine Kouma mrithi wa Khalid Aucho Yanga SC
Marubani huwa wanakuwa na mamilioni wikiendi
Wikiendi kwa marubani huwa inakuwa bomba kutokana na mamilioni mfukoni. Paisha ndege sasa uvune mkwanja wako. Hakuna kwenda kinyonge, mgao upo wakutosha ukicheza Aviator.

Ni Julai 23 Kocha Mkuu Romain Folz alitambulishwa Yanga SC. Rekodi zinaonyesha kuwa ni kocha ambaye amefundisha timu mbalimbali. Atakuwa ndani ya kikosi cha Yanga SC ambacho kinaendelea na usajili wa wachezaji wapya. Wapo wengine ambao wataongeza kandarasi zao.
CV ya kocha mpya Yanga SC hii hapa
Kuhusu kocha mpya wa Yanga SC, mchambuzi Hans Rafael alibainisha kuwa ni miongoni mwa makocha bora. Hans alisema ana uzoefu na mashindano makubwa na alianza kazi akiwa kijana mdogo. Baada ya utambulisho wake alisema namna hii:
“Anaitwa Romain Folz (35) kocha mpya wa Yanga SC. Alizaliwa Bordeaux, Ufaransa. Huyu kocha amefanya kazi sehemu zifuatazo: -2025 alikuwa mkurugenzi wa michezo wa Olympique Akbou ya Algeria. 2024 alikuwa kocha msaidizi wa Mamelodi Sundown ya Afrika Kusini.
“2023 alikuwa Kocha Mkuu wa Horoya ya Guinea. 2022 alikuwa Kocha Mkuu wa Amazulu ya Afrika ya Kusini. 2021 alikuwa Kocha Mkuu wa Township Rollers ya Botswana. 2019 alikuwa kocha msaidizi wa Pyramid ya Misri. 2018 alikuwa kocha msaidizi wa timu ya taifa ya Uganda.
“Huyu kocha ana UEFA Pro Licence na Pro Licence ya CONMEBOL (America). Huyu kocha ni muumini wa (4-3-3) na timu yake ina-press kinoma. Wananchi Remember the Name Romain Folz, balaa jingine ndani ya NBC Premier League,”.
Hawa atafanya nao kazi Yanga SC 2025/26
Lassine Kouma

Soma hii: Mudathir Yahya ameongeza mkataba miaka miwili Yanga SC
Kiungo mpya Lassine Kouma atakuwa ndani ya Yanga SC kuelekea msimu wa 2025/26. Kiungo huyo ni mrithi wa mikoba mikoba ya Khalid Aucho. Kasajiliwa Yanga SC akitokea Stade Malien anakutana na kocha mpya.
Balla Conte
Ilikuwa Julai 18 2025 Yanga SC ilimtambulusha Moussa Balla Conte. Ingizo hili jipya ni kutoka CS Sfaxien ya Tunisia yeye ni raia wa Guinea. Nyota huyu mpya alisaini mkataba wa miaka mitatu.
Mudathir Yahya
Mzawa Mudathir Yahya Julai 22 2025 aliongeza mkataba wa miaka miwili. Atakuwa ndani ya Yanga SC mpaka 2027. Uhakika kufanya kazi na kocha mpya Jangwani.
Offen Chikola

Soma hii: Offen Chikola atambulishwa Yanga SC
Mkali kwenye kutumia mguu wa kushoto atakuwa chini ya kocha mpya. Ni Offen Chikola alitambulishwa Yanga SC Julai 22 2025. Ni kandarasi ya miaka miwili. 2024/25 akiwa na Tabora United alifunga mabao 8 kati ya 28 yaliyofungwa na timu hiyo.
Casemiro
Anaitwa Abdulnassir Mohamed maarufu kwa jina la Casemiro alitambulishwa rasmi Jangwani, Julai 23 2025. Huyu ni mzawa ambaye atakuwa kwenye changamoto mpya. Kazi kubwa itakuwa kwenye kupambania nafasi ndani ya uwanja.
Dennis Nkane
Huyu ni kiungo mshambuliaji jina anaitwa Dennis Nkane aliongeza mkataba wa miaka miwili mpaka 2027. Nkane hakuwa na nafasi kikosi cha kwanza msimu wa 2024/25. Kazi kubwa itakuwa kwenye kupambania namba msimu mpya chini ya kocha mpya.
Nkane ilikuwa wazi rasmi Julai 25 2025 kwamba ameongeza kandarasi ya miaka miwili. Hivyo bado mchezaji huyo ataendelea kuwa Jangwani. Ni miongoni mwa wachezaji waliovaa medali za ubingwa msimu wa 2024/25.
Pacome

Soma hii: Uongozi wa Yanga SC umeweka wazi vita ya MVP
Pacome Zouzoua aliongeza mkataba wa miaka miwili Julai 24 2025. Nyota huyu alikamilisha msimu akiwa kafunga jumla ya mabao 12 na pasi 10. Kwenye mabao hayo 12 alifunga mabao mawili kwa penati.
Pacome yupo ndani ya kikosi cha Yanga SC msimu wa 2025/26. Ni miongoni mwa wachezaji waliovaa medali kwenye mchezo wa fainali Kombe la Shirikisho Afrika. Mguu wake wenye nguvu ni ule wa kulia.
Djigui Diarra
Kipa namba moja wa Yanga SC ni Djigui Diarra. Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga SC aliweka wazi kuwa kipa huyo yupo sana. Ilikuwa inaelezwa kuwa huenda kipa huyo ataondoka katika kikosi hicho.
Job
Licha ya kwamba beki Dickson Job hajatangazwa kuhusu kusaini mkataba mpya inaelezwa kuna asilimia kubwa atabaki. Mkataba wake uliisha mwishoni mwa msimu wa 2024/25. Huyu ni beki ambaye kwa sasa yupo kwenye majukumu ya timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars itakayocheza mchezo dhidi ya Burkina Faso, Agosti 2 2025 kwenye CHAN.
Hitimisho
Kocha mpya wa Yanga SC ana kibarua cha kutetea mataji ambayo timu hiyo ilitwaa msimu wa 2024/25. Miongoni mwa mataji hayo ni taji la Ligi Kuu Bara inayodhaminiwa na NBC, CRDB Federation Cup. Katika Ligi ya Mabingwa Afrika hesabu za Yanga SC ni kufanya vizuri zaidi ya msimu uliopita nalo litakuwa jukumu kocha mpya.


