- Moshi mzito umetanda kwenye makao makuu ya klabu ya Yanga SC maeneo ya Jangwani.
- Hii ni kufuatia taarifa ya Roman Folz kufukuzwa Yanga SC.
- Uongozi wa Yanga SC kumtangaza kocha mpya huyu kutoka Algeria.
Hali imezidi kuwa tete kwenye viunga vya Jangwani, hii ni kufuatia taarifa ya Roman Folz kufukuzwa Yanga SC. Taarifa hiyo kutoka ndani imeeleza kuwa, uongozi wa Yanga SC tayari umefikia muafaka wa kumfuta kazi kocha Folz. Hii ni baada ya tathimini yao kuonyesha kocha huyo ameshindwa kuthibitisha ubora wake. Kufuatia uamuzi huo Yanga wanatajwa kumrudisha aliyekuwa kocha wao, Sead Ramovic.
SOMA HII PIA: Romain Folz kuondoka Yanga SC ukweli upo hivi | Ali Kamwe abainisha, matokeo, CV
Cheza na ushinde sasa na ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni muda huu
Hujashinda na kindege cha SportPesa? Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kubashiri SportPesa bonyeza picha hii chini

Kocha Roman Folz kufukuzwa Yanga SC nini kimetokea?

Taarifa kuhusu kocha Folz kufukuzwa Yanga SC ziliripotiwa muda mrefu, lakini zilipata nguvu zaidi baada ya mchezo wao dhidi ya Mbeya City. Ripoti za hivi karibuni zimethibitisha kuwa uongozi wa Yanga SC umemfuta kazi kocha Folz. Taarifa hiyo inaeleza sababu kubwa ya maamuzi hayo ni kutokana na shinikizo la mwenendo usioridhisha wa kikosi.
Romain Folz alipewa nafasi ya kuwa kocha wa Yanga kuanzia msimu wa 2025/26, akichukua nafasi ya Miloud Hamdi. Kocha huyo alipewa malengo ya kudumisha utawala wa ndani, pamoja na kuifikisha mbali Yanga SC katika michuano ya Afrika. Lakini licha ya matumaini makubwa, kuna dalili zinazoonyesha kutoridhika kwa baadhi ya mashabiki na uongozi.
SOMA HII ZAIDI: Romain Folz kocha mpya Yanga SC mwenye CV kubwa | Wachezaji wenye uhakika 2025/26

Sababu nyingine za kumng’oa folz ni zipi?

Ukiachana na kiwango cha timu kuelezwa kushuka, mchezo dhidi ya Mbeya City uliomalizika 0-0 umeibua malalamiko makubwa ya mashabiki. Mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo, baadhi ya mashabiki walipiga kelele “Hatumtaki, hatumtaki” kumkosoa Folz. Pia inaelezwa kuna matatizo ya mambo ya ndani, kama kufanya marekebisho katika benchi la ufundi, wasaidizi na wataalamu wengine.
Kocha mpya Yanga SC huyu hapa

Kufuatia uamuzi wa kumfuta kazi Folz, Yanga SC wametajwa kuwa kwenye mpango wa kumrudisha aliyekuwa kocha wao, Sead Ramovic. Kocha huyo ambaye aliwahi kuhudumu kwa muda mfupi ndani ya Yanga SC kwa sasa yupo nchini Algeria. Lakini taarifa kutoka huko zinaeleza kuwa huenda akafutwa kazi na kutoa nafasi ya kurejea Yanga SC.
Historia ya Sead Ramović na Kuondoka kwake Yanga SC
Sead Ramović alijiunga na Yanga SC tarehe 15 Novemba 2024, akichukua nafasi ya Miguel Gamondi. Mwanzoni alionyesha uzoefu mzuri katika ligi ya ndani, Yanga ilishinda michezo mingi kwa soka lake maarufu ‘Gusa Achia, twende kwao’. Lakini licha ya mwanzo mzuri, matokeo ya kimataifa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika hayakuenda kama walivyopanga. Hii ilipelekea Ramović kuondoka na kujiunga na klabu ya CR Belouizdad ya Algeria.
Je, kocha Ramović anaweza Kurudi?
Tetesi za Ramović kurudi zimeonekana kuzua mjadala miongoni mwa mashabiki na wachambuzi wa soka. Kila mmoja anazichambua kwa namna yake. Wapo wanaozungumzia uwezo wake wa kuleta matokeo mazuri, ndani ya ligi na jinsi ambavyo alishinda michezo kwa mfululizo. Pia kumekuwa na takwimu kwamba alikuwa na mahusiano mazuri kwenye kikosi na tabia ya usimamizi wa benchi.
Haya hapa maboresho yanayohitajika Yanga SC

Ikiwa Yanga itafikiria tena kumrudisha Ramović au kuchagua kocha mwingine badala ya Folz, hapa kuna mambo muhimu ambayo yatahitaji kuangaliwa:
Utulivu wa kikosi – kuhakikisha wachezaji wanaweka imani na mabadiliko yanayofanyika, kuwasiliana kwa uwazi juu ya malengo ya klabu na kocha.
Matokeo ya ndani na kimataifa – Malengo ya Yanga SC sio tu kushinda ligi, bali pia kushindana vizuri katika michuano ya Afrika, hiki ndiyo kipimo kikubwa cha mafanikio kwa klabu ya kiwango cha Yanga.
Benchi la ufundi lenye uzoefu na ubunifu – wachezaji wanahitaji msaada wa wataalamu wa viwango tofauti lakini muhimu ikiwemo mazoezi, uimarishaji wa misuli, afya, mbinu na uchambuzi wa video.
Kuheshimu mashabiki na utamaduni wa klabu – msukosuko kati ya mashabiki unaweza kuleta presha kubwa, uongozi lazima uzingatie jinsi wanavyoweza kushikilia nafasi ya klabu kama sehemu ya jamii na utamaduni.]
SOMA HII PIA: Yanga SC yashusha mashine hii nyingine usiku: Tetesi, usajili Ligi Kuu ya NBC 2025/26

Hitimisho
Ingawa hakuna uthibitisho rasmi wa kuwa Roman Folz kufukuzwa Yanga SC, lakini ni wazi kwamba shinikizo limekua kubwa kutokana na matokeo pamoja na kiwango cha timu. Hivyo inaelezwa tutarajie taarifa kubwa siku za usoni. Hii ni juu ya majaaliwa ya benchi la ufundi la Yanga SC.

