KMC FC vs Yanga SC ni leoSaliboko (-)
  • KMC FC vs Yanga SC ni leo NBC Premier League, Uwanja wa KMC Complex
  • Dhidi ya Yanga SC, KMC FC imecheza mchezo mmoja msimu wa 2025/26 ilipoteza kwa kufungwa magoli 4-1.
  • Yanga SC inaongoza ligi kwenye msimamo inakutana na KMC FC ambayo ni ya mwisho.

KMC FC vs Yanga SC ni leo Mei 6, 2026 mchezo wa NBC Premier League mzunguko wa pili. Hii ni vita ya timu inayoongoza ligi na inayoburuza mkia kwenye msimamo. KMC FC imecheza mchezo mmoja na Yanga SC ilipoteza kwa kufungwa magoli 4-1. Mchezo uliopita Simba SC 2-2 Yanga SC katika Kariakoo Dabi. Wenyeji matokeo yalikuwa JKT Tanzania 1-0 KMC FC, timu zote zilicheza Uwanja wa Meja Jeneral Isahmuyo.

SOMA HII: Yanga SC: Historia, Usajili wote, kikosi, Ratiba, Matokeo na Takwimu

Je, bado hujashinda mamilioni ya aviator ‘Kindege’ cha SportPesa? Cheza ushinde mamilioni sasa

Changamka! sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

SportPesa Aviator Challenge

KMC FC vs Yanga SC ni leo Mei 6, 2026 kupigwa saa ngapi?

KMC FC vs Yanga SC ni leo
Captain Nondo

Burudani inaendelea katika ligi namba 6 kwa ubora, KMC FC vs Yanga SC ni leo Mei 6, 2026. Mchezo huu mkali unatarajiwa kuchezwa saa 10:00 jioni, Uwanja wa KMC Complex. Huu ni moja ya mchezo mkali kati ya mitatu ambayo inatarajiwa kuchezwa leo ndani ya ligi.

KMC FC inaburuza mkia ikiwa na pointi 9 baada ya kucheza mechi 20. Inakutana na Yanga SC vinara wakiwa na pointi 48. Wananchi hawajapoteza mchezo huku wenyeji wakiwa wamepoteza mechi 15.

SOMA HII: Yanga SC bado ipo kazini, ratiba ya NBC Premier League, msimamo wa 5 bora

Aviator game promotional banner featuring a red propeller plane and a jackpot of 800,000,000.

KMC FC vs Yanga SC H2H

KMC vs Yanga SC ni leo
Allen Okello kiungo mshambuliaji wa Yanga SC

9/11/2025, Yanga SC 4-1 KMC FC

14/02/2025, KMC FC 1-6 Yanga SC

29/09/2024, Yanga SC 1-0 KMC FC

17/02/2024, KMC FC 0-3 Yanga SC

23/08/2023, Yanga SC 5-0 KMC FC

Rekodi zinaonyesha tangu 2018 timu hizi zimekutana mara 15. Yanga SC imepata ushindi mara 12, KMC FC ushindi mara moja, sare ni 2. Hivyo Yanga SC wamekuwa wababe mbele ya KMC FC wanapokutana.

Ratiba ya mechi nyingine leo Mei 6, 2026

Simba SC vs JKT Tanzania

Mtibwa Sugar vs Dodoma Jiji FC

SOMA HII: Yanga SC 4-1 KMC FC NBC Premier League 2025/26/ Highligts, magoli, msimamo

Hitimisho

KMC FC vs Yanga SC ni leo mchezo wa mzunguko wa pili. Yanga SC hawajapoteza mchezo katika mechi 20. Kwenye mechi tano walipokutana Wakusanya mapato hawajapata ushindi. Je leo watavunja rekodi hiyo? Endelea kufuatilia SportPesa Blog kwa taarifa zaidi na matokeo.

Share this: