- Simba SC vs JKT Tanzania NBC Premier League, Mei 6, 2026 Uwanja wa Meja Jeneral Isahmuyo
- Steve Barker abainisha Simba SC ipo tayari kupambania pointi tatu
- Simba SC imecheza mchezo mmoja na JKT Tanzania msimu huu ikipata ushindi wa magoli 2-1
Simba SC vs JKT Tanzania NBC Premier League ni mchezo unaofuata kwenye ratiba leo. Mnyama mchezo uliopita aligawana pointi mojamoja kwa kufungana magoli 2-2 dhidi ya Yanga SC. Uwanja wa Meja Jeneral Isahmuyo utapigwa saa 12:15 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.
SOMA HII:JKT Tanzania 1-2 Simba SC NBC Premier League 2025/26/ Highlights, goal
Vuna mamilioni sasa hivi na SportPesa
Kuna jambo umekwama kwa sasa kuhusu mkwanja? Usiogope, rubani ni jasiri na kazi yake ni kupaisha kindege cha SportPesa. Cheza sasa hivi Aviator uvune mamilioni bofya hapa chini.

Simba SC vs JKT Tanzania NBC Premier League utabiri upoje?

Leo ni Simba SC VS JKT Tanzania NBC Premier League utabiri ukiwa ni mgumu kwa timu zote mbili. Hii inatokana na wababe hawa wote kuwa ndani ya nne tano bora. Mnyama yupo nafasi ya 3 pointi 43 baada ya mechi 20. Wageni wapo nafasi ya 5 pointi 32.
JKT Tanzania ni imara kwenye ulinzi kutokana na kukusanya sare nyingi ambazo ni 8. Ushindi ni michezo 8 huku ikipoteza mechi 4. Simba SC imepoteza mchezo mmoja, ushindi mechi 12 na kuvuna sare katika mechi 7.
Mchezo uliopita JKT Tanzania ilishinda katika Uwanja wa Meja Jeneral Isahmuyo kwa goli 1-0 KMC FC. Ikumbukwe kwamba mwanzo wa msimu timu hii ilipata nafasi kuongoza ligi. Hivyo sio timu yakubeza kwenye mechi za ushindani.
SOMA HII: Ratiba ya Simba SC NBC Premier League 2025/26 ni moto | Msimamo, Mzizima Dabi, Kariakoo Dabi

H2H Simba SC vs JKT Tanzania NBC Premier League
8/11/2025, JKT Tanzania 1-2 Simba SC
05/05/2025, JKT Tanzania 0-1 Simba SC
24/12/2024, Simba SC 1-0 JKT Tanzania
28/05/2024, Simba SC 2-0 JKT Tanzania
15/02/2024, JKT Tanzania 0-1 Simba SC
Wachezaji watakaokosekana Simba SC vs JKT Tanzania

Mshambuliaji Jonathan Sowah hayupo kwenye mpango wa Simba SC hii ni kutokana na makosa ya nidhamu. Wilson Nangu ambaye ni beki naye bado hajarejea uwanjani kwa kuwa hayupo fiti. Wawili hawa walifunga mchezo uliopita dhidi ya JKT Tanzania. Yakoub Suleman ambaye ni kipa, Hamza Jr ambaye ni beki wote kwa upande wa Simba SC hawajawa fiti.
Anicet Oura bado hajaimarika. Mousa Camara kipa namba moja wa Simba SC anatarajiwa kuwa nje ya uwanja msimu mzima. Ni wachezaji sita kwa Simba SC hawatakuwepo huku JKT Tanzania wakibainisha kuwa wapo imara.
Maoni ya makocha
Steve Barker Kocha Mkuu wa Simba SC amesema kuwa wapo tayari kupambana kwa ajili ya pointi tatu. Kocha huyo ameongeza wachezaji wanatambua ugumu wa mchezo. Barker anaamini watajituma kutimiza majukumu.
“Tupo tayari kwa ajili ya kupambania pointi tatu muhimu. Hautakuwa mchezo mwepesi kutokana na aina ya wapinzani. Kikubwa ni kuona tunafikia malengo mara baada ya mchezo,” alisema Barker.
Kwa upande wa Ahmad Ally, Kocha Mkuu wa JKT Tanzania amesema kila kitu kipo tayari kwa mchezo: “Hakuna changamoto yoyote mpaka sasa. Tupo tayari kwa mchezo wetu dhidi ya Simba SC,”.
SOMA HII: Usajili wa Chama Simba SC washtua! Mayele, Kagere, Okwi wafunguka Mazito
Hitimisho
Simba SC vs JKT Tanzania NBC Premier League unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa. Kwa mechi za Mei rekodi zinampa ushindi mnyama. Je ataendelea na rekodi hiyo au itatibuliwa? Endelea kufuatilia SportPesa Blog kwa taarifa na matokeo zaidi.

