- Goli la Clatous Chama gumzo kubwa kila kona
- Ahmed Ally ametamba na kulitaja kuwa goli bora 2025/26
- Simba SC 2-2 Yanga SC, Meja Jeneral Isahmuyo, Mei 3, 2026
Goli la Clatous Chama kiungo mshambuliaji wa Simba SC gumzo kubwa kila kona kutokana na kufungwa kitaalamu mchezo wa Kariakoo Dabi. Mwamba wa Lusaka alifunga goli dakika ya 10 kwa pasi ya Ellie Mpanzu. Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC amesema dunia nzima imeliona na kulipenda goli hilo. Mei 3, 2026 ubao wa Meja Jeneral Isahmuyo ulisoma Simba SC 2-2 Yanga SC goli hilo lilifungwa.
SOMA HII: Clatous Chama usajili wake umelipa | Takwimu na timu alizocheza CAF Champions League
Bado hujashinda pesa? Cheza ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa
Ni zamu yako sasa, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

Kwa nini goli la Clatous Chama gumzo kubwa kwa sasa?

Kariakoo Dabi imekwisha kwa wababe kugawana pointi mojamoja, goli la Clatous Chama gumzo kubwa kila kona kwa sasa. Kiungo huyo alifunga goli ambalo halikutarajiwa kwenye mchezo mkubwa. Hili ni goli la kwanza kwa Chama kufunga mbele ya Yanga SC msimu wa 2025/26 mara baada ya kusajiliwa akitokea Singida Black Stars.
Wakiwa wanaongoza goli 1, Chama aliongeza la pili dakika ya 10 akitumia pasi ya Mpanzu. Utulivu kwenye miguu yake na akili vilileta goli hilo. Alikuwa katikati ya mabeki wa Yanga SC aliruka juu kidogo na kufunga goli hilo lililozama nyavuni.
Licha ya Simba SC kupata uongozi wa mapema, walikwama kulinda ushindi huo.Matokeo ya mwisho ilikuwa 2-2. Magoli ya Yanga SC yalifungwa na Prince Dube dakika ya 17 na Bakari Nondo dakika ya 50.

Huyu hapa Clatous Chama maoni yake

Clatous Chama mara baada ya mchezo huo alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo. Hii ilitokana na kuhusika katika magoli yote mawili. Alifunga na kutoa pasi ya goli kwa Libase Gueye dakika ya pili.
“Ni matokeo ambayo hatukutarajia kwenye mchezo wetu. Tulipata nafasi ya kuongoza na wapinzani wakarudisha magoli. Hivyo tuna kazi kubwa kufanya katika mechi zetu ambazo zinakuja kikubwa mashabiki waendelee kuwa nasi.
“Kuchaguliwa kuwa mchezaji bora inaonesha kuna kitu ambacho kimeonekana. Kila mchezaji amefanya kazi kubwa hilo lipo wazi. Tutaendelea kushirikiana zaidi kwa ajili ya kutafuta matokeo,” alisema Chama.
Ahmed Ally atamba na goli la Chama
Ahmed amesema goli la Chama limependwa na dunia nzima. Hii inatokana na ubora wake na maajabu ambayo yapo. Aliongeza kuwa goli hilo linastahili kupelekwa sayari nyingine.
“Goli alilofunga Clatous Chama limeonwa na dunia nzima na kila mtu analipenda kwa sasa. Lile linastahili kupelekwa kwenye sayari nyingine. Hata Yanga SC wenyewe wanalipenda ni goli nzuri limefungwa kwa ustadi mkubwa.
“Ligi yetu inazidi kufahamika zaidi kila kona kwa kuwa goli la Chama linazungumzwa. Tunafurahi kuona magoli mazuri yanafungwa tena kutoka kwa mchezaji wa Simba SC. Kila mtu sasa analizungumzia kwa mazuri ujue,” alisema Ahmed, Meneja wa Idara ya Habari Simba SC.
SOMA HII: Usajili wa Chama Simba SC washtua! Mayele, Kagere, Okwi wafunguka Mazito
Hitimisho
Goli la Clatous Chama gumzo kubwa msimu wa 2025/26. Wachezaji wamekuwa wakifanya kazi kubwa katika sanaa yakufunga. Je litwatwaa tuzo ya goli bora la msimu? Endelea kufuatilia Blog ya SportPesa kwa taarifa zaidi.

