Bayern Munich vs Paris Saint-GermainBayern Munich vs Paris Saint-Germain
  • Bayern Munich vs Paris Saint-Germain utakuwa mchezo wa mvua ya magoli tena? Ndilo swali kubwa ambalo wadau wa soka wanajiuliza.
  • Hii ni kuelekea mchezo mkali wa marudiano wa Nusu Fainali ya UEFA Champions League utakaopigwa kwenye Uwanja wa Uwanja wa Allianz Arena.
  • Ikumbukwe mchezo wa kwanza uliisha kwa matokeo ya Paris Saint-Germain 5-4 Bayern Munich.

Bayern Munich vs Paris Saint-Germain je, ni mvua ya magoli tena? Ndilo swali kubwa ambalo wadau wa soka wanajiuliza. Hii ni kuelekea mchezo mkali wa marudiano wa Nusu Fainali ya UEFA Champions League. Mchezo huu ambao utapigwa kwenye Uwanja wa Uwanja wa Allianz Arena siku ya Jumatano, utakuwa mchezo wa mkondo wa pili. Hii ni baada ya mchezo wa kwanza ulioisha kwa matokeo ya Paris Saint-Germain 5-4 Bayern Munich.

Fuatilia mwenendo wote wa mashindano ya UEFA Champions League 2025/26; Ratiba, matokeo, mechi, magoli na habari za papo kwa papo kupitia SportPesa Blog.

Unataka kushinda mamilioni? Unaweza kushinda mpaka Shilingi Milioni 800 na SportPesa

Wengi tayari wamevuna mamilioni kupitia mchezo wa Kindege yaani ‘Aviator’ ya SportPesa. Wewe unasubiri nini? Nafasi ni yako cheza Aviator na kushinda mpaka Shilingi Milioni 800 sasa kwa kubonyeza picha hii chini.

Aviator game promotional banner featuring a red propeller plane and a jackpot of 800,000,000.
Aviator: Paisha kindege ujishindie mpaka zaidi ya Milioni 800,000,000

Bayern Munich vs Paris Saint-Germain h2h

Paris Saint-Germain or Bayern München #UCL
Paris Saint-Germain or Bayern München UCL

Timu hizi zimekutana katika michezo 17 katika historia ya soka la ushindani, ambapo Bayern Munich wameshinda mechi 9. Paris Saint-Germain wao wameshinda mechi 8, na hakujawahi kupatikana matokeo ya droo wanapokutana. Hivyo mchezo huu unatarajiwa kutoa rekodi mpya, ya mikutano kwa wakubwa hao wawili wanapokutana.

SOMA HII PIA: PSG vs Inter Milan 31/5/2025 Fainali UEFA: H2H, Vikosi, utabiri, habari za timu

Fomu za timu UCL Champions League

Bayern Munich

W W W W W L

PSG

D W W W W W

Vikosi vinavyotarajiwa kuanza Bayern Munich vs Paris Saint-Germain

Bayern Munich

Kipa: Neuer

Walinzi: Stanisic, Upamecano, Tah, Davies

Viungo: Kimmich, Pavlovic, Olise, Musiala, Diaz

Mshambuliaji: Kane

PSG

Kikosi cha PSG
Kikosi cha PSG

Kipa: Safonov

Walinzi: Zaire-Emery, Marquinhos, Pacho, Mendes

Viungo: Ruiz, Vitinha, Neves, Doue

Washmabuliaji: Dembele, Kvaratskhelia

SOMA HII ZAIDI: Ligue 1 football betting – SportPesa covers the best teams in France

Habari za timu

Dembele x Olisse
Dembele x Olisse

Mchezo wa kwanza baina ya timu hizi uliisha kwa matokeo ya Paris Saint-Germain 5-4 Bayern Munich, mchezo huu uliandika historia ya mchezo uliozaa mabao mengi zaidi kuwahi kutokea katika nusu fainali ya UCL. Safu kali ya ushambuliaji ya PSG ya Ousmane Dembele, Desire Doue na Khvicha Kvaratskhelia ilitawala kwa dakika 60 za mwanzo. Mastaa hawa walihusika moja kwa moja kwenye mabao saba.

Bayern walitoka nyuma kwa mabao 2-5 hadi 4-5 ndani ya dakika nne tu, kuifanya mechi ya marudiano kuwa ya kusisimua na isiyotabirika. Katika mara 10 zilizopita ambapo Bayern walipoteza mchezo wa kwanza wa nusu fainali ya Ulaya, walitolewa mara tisa. Wakifanikiwa kurejea mara moja tu, kufika fainali dhidi ya CSKA Sofia mwaka 1981-82.

Kocha wa PSG, Luis Enrique, alipinga vikali hoja kwamba timu hizo zilikuwa dhaifu kiulinzi licha ya mabao mengi, akisema hiyo ni “maoni mabovu”. PSG wana rekodi nzuri wanaposhinda mechi ya kwanza, wakifanikiwa kusonga mbele mara 36 kati ya 43 katika hatua za mtoano za UEFA. Mchezo uliopita wa ligi, PSG walilazimishwa sare ya 2-2 na Lorient licha ya kuongoza mara mbili. Hata hivyo, rekodi yao ya ugenini ni nzuri sana, wakishinda mechi 6 mfululizo, katika mashindano yote na kutoruhusu bao katika mechi tano zilizopita.

Habari za majeruhi

Bayern Munich

Wenyeji Bayern Munich hawana majeraha mapya, na wanatarajia kijana Lennart Karl kupona kwa wakati. Serge Gnabry na Raphael Guerreiro hawatacheza, lakini hawakutarajiwa kuanza. Wachezaji kama Manuel Neuer, Dayot Upamecano, Alphonso Davies, Joshua Kimmich, Olise, Luis Diaz na Harry Kane wanatarajiwa kurejea kikosi cha kwanza. Harry Kane analenga kufunga katika mechi ya saba mfululizo ya Champions League.

Paris Saint-Germain

Bayern Munich vs Paris Saint-Germain
Hakimi x Dembele

Kwa upande wa PSG, beki Achraf Hakimi ameumia na anatarajiwa kukosa mchezo huu, Warren Zaire-Emery anatarajiwa kucheza beki, huku Fabian Ruiz akirejea kiungo pamoja na Vitinha na Joao Neves. PSG pia watamkosa kipa Lucas Chevalier, lakini kikosi kingine kiko tayari. Kvaratskhelia anahitaji bao moja tu, kuweka rekodi mpya ya mabao mengi kwa PSG katika msimu mmoja wa UCL.

SOMA HII PIA:Bayern Munich vs Real Madrid : UEFA Champions League, Live Score, h2h & predicted lineups

Utabiri na hitimisho

Bayern Munich vs Paris Saint Germain ni mchezo unaotabiriwa kushuhudia mabao mengi, kama ilivyokuwa mchezo wa awali Kukosekana kwa Hakimi kunaweza kuwa pigo kubwa kwa PSG. Bayern wamekuwa wakifunga mabao mengi nyumbani, hivyo wanapewa nafasi kubwa ya kushinda na kuiondoa PSG. Lakini ni wazi tunatarajia mchezo mkubwa, mgumu na ushindani.

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.