Bayern Munich vs Real MadridBayern Munich vs Real Madrid
  • Mchezo wa raundi ya pili ya UEFA Champions League kati ya Bayern Munich vs Real Madrid, utapigwa pale Uwanja wa Allianz Arena, 15 April 2026, 19:00 UTC.
  • Mechi ya kwanza iliyopigwa Uwanja wa Santiago Bernabeu, iliishia kuwa na matokeo haya Real Madrid 1-2 Bayern Munich.
  • Bayern Munich inahitaji angalau matokeo ya sare tu, ikiwa nyumbani ili kufuzu hatua ya Nusu Fainali na kuitoa Real Madrid.

Mchezo wa marudiano wa UEFA Champions League kati ya Bayern Munich vs Real Madrid utapigwa leo kwenye Uwanja wa Allianz Arena, Munich nchini Ujerumani. Mechi hii maarufu inayojulikana kama ‘European Classico’ inatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa dhidi ya miamba hii miwili ya Ulaya. Mchezo wa mkondo wa kwanza Bayern Munich walionekana kuwa tishio sana, na kuilaza Real Madrid kwa mabao 2-1. Je, ni nani atafuzu kuingia Nusu Fainali ya UEFA Champions League kati ya hizi timu mbili?

Fuatilia matukio ya karibuni ya UEFA Champions League Quarter Finals match , mabao, takwimu na habari za hivi sasa kupitia SportPesa blog

SOMA HII PIA: Bayern Munich’s Epic Showdown: 3 Wins Each vs Leverkusen

Je, bado hujashinda na SportPesa? Cheza mchezo wa aviator ‘Kindege’ uvune mamilioni sasa

Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

Sportpesa Aviator Rain Free Bets- Mil
Sportpesa Aviator Rain Free Bets- Mil

Bayern Munich vs Real Madrid h2h

h-h
h-2-h

Bayern Munich vs Real Madrid wanakutana leo head to head kwenye Uwanja wa Allianz Arena, Munich nchini Ujerumani. Kwa ujumla timu hizi zimekutana mara 29, Bayern Munich wakishinda mechi 12, Real Madrid 13 na mechi 4 zikiisha kwa sare. Kwenye mkondo wa kwanza wa Robo Fainali ya UEFA Champions League, Bayern Munich wanajivunia ushindi wa mabao 2-1. Ushindi huu unawapa motisha wakiwa nyumbani kuelekea kwenye Nusu Fainali.

Jedwali hili linaonyesha Bayern Munich vs Real Madrid Head to Head

CategoryBayern MunichDrawsReal Madrid
Total Wins13412
Goals Scored4644
Record TypePlayerAchievement
All-time Top ScorerCristiano Ronaldo105 goals
Bayern Top ScorerRobert Lewandowski69 goals
CategoryBayern MunichReal Madrid
Total Titles615
Most Recent Title2019/202023/24

Vikosi vinavyotarajia kuanza Bayern Munich vs Real Madrid

Bayern Munich:

Kipa: Neuer

Walinzi: Laimer, Upamecano, Tah, Stanisic

Viungo: Kimmich, Pavlovic, Olise, Gnabry

Washambuliaji: Diaz, Kane

Real Madrid:

Real Madrid vs Bayern
Real Madrid vs Bayern

Kipa: Lunin

Walinzi: Alexander-Arnold, Rudiger, Huijsen, Carreras

Viungo: Valverde, Camavinga, Bellingham, Guler

Washambuliaji: Mbappe, Vinicius Jr

Taarifa za timu

Fuatilia habari za hivi punde za mechi ya Bayern Munich vs Real Madrid ikiwemo Live odds, stats, Match Updates na Lineups kupitia SportPesa. Kwa wale wanaotaka kujua sehemu ya kuona mechi hii, masaa na TV Channel zinazorusha live; mchezo wenyewe utapigwa Uwanja wa Allian Arena, masaa ni 19:00 UTC, Wednesday 15 April 2026, Broadcast-Stan sport, Supersport & TNT sports.

Habari za hivi sasa za Bayern Munich vs Real Madrid

Bayern Munich vs Real Madrid
Bayern Munich vs Real Madrid

Huu ni mchezo wa 30 kwa timu hizi kukutana katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Kikosi cha Vincent Kompany kinaingia kwenye mchezo huu wa marudiano wa robo fainali kikiwa na faida ya ushindi wa 2-1 katika mchezo wa kwanza uliochezwa Bernabeu wiki iliyopita. Mabao ya Luis Diaz na Harry Kane, yalitosha kuizamisha Real Madrid mbele ya mashabiki wao wa nyumbani.

Ushindi huo uliifanya Bayern kuvunja rekodi ya kucheza mfululizo wa mechi tisa bila ushindi, dhidi ya wapinzani hao kutoka Hispania. Hata hivyo, bao la dakika za mwisho la Kylian Mbappe limeifanya mechi hii kubaki wazi. Bayern wamefanikiwa kushinda michezo 29 kati ya 30 ya hatua za mtoano za UEFA walizoshinda ugenini katika mchezo wa kwanza, isipokuwa mara 1 tu, msimu wa 2010-11 walipofungwa vs Inter Milan.

Baada ya kuichapa Madrid, Bayern wikendi hii waliendeleza vipigo baada ya kuifunga St Pauli mabao 5-0 katika Bundesliga. Kwa sasa wanaongoza ligi kwa tofauti ya pointi 12, na wanaweza kutwaa ubingwa mapema kabisa. Hata hivyo, kipaumbele chao kikuu ni Ligi ya Mabingwa, wakilenga kufika nusu fainali kwa mara ya kwanza tangu walipotwaa taji hilo msimu wa 2019-20. Huu ni mtihani mkubwa kwao hasa ukizingatia wamekuwa na rekodi mbaya dhidi ya timu za Hispania, katika hatua za mtoano.

Bayern wamekuwa bora sana wakicheza kwenye Uwanja wao wa, Allianz Arena ambapo wana wastani wa kushinda kwa mabao 3.2 kwa kila mechi. Pia wamepoteza mechi 1 tu, kati ya 28 za nyumbani za Ligi ya Mabingwa, kwa upande wa Real Madrid, wanakabiliwa na hatari ya kumaliza msimu bila taji kubwa. Kwenye La Liga wamevuna pointi moja tu, katika mechi mbili zilizopita, walipoteza 2-1 dhidi ya Mallorca kabla ya kutoka sare ya 1-1 nyumbani dhidi ya Girona. Matokeo hayo yamewapa Barcelona nafasi ya kuongoza ligi kwa tofauti ya pointi 9, huku zikisalia mechi 7 tu ligi kuisha.

SOMA HII ZAIDI: Top 5 Dominating Soccer Teams in 2023-2024: Who Will Reign Supreme?

Taarifa za wachezaji majeruhi Bayern Munich vs Real Madrid

Bayern Munich

Vigogo hawa wa Ujerumani watakosa baadhi ya wachezaji kutokana na majeraha, huku Harry Kane akitarajiwa kucheza licha ya kuwa na maumivu madogo. Mshambuliaji huyo amehusika katika upatikanaji wa mabao kwenye mechi zote 4 za mwisho za Ligi ya Mabingwa dhidi ya Real Madrid. Serge Gnabry anatarajiwa kurejea kikosini baada ya kupona jeraha dogo, huku safu ya kiungo ikiongozwa na Joshua Kimmich na Aleksandar Pavlovic.

Real Madrid

Bayern Munich vs Real Madrid
Kylian Mbappe

Kwa upande wa Real Madrid, baadhi ya wachezaji muhimu hawatakuwepo kutokana na majeraha na adhabu. Kylian Mbappe, ambaye anaongoza kwa mabao katika michuano hii, yuko kwenye hali ya mashaka baada ya kupata jeraha la uso. Iwapo atakuwa fiti, ataungana na Vinicius Junior katika safu ya ushambuliaji.

Utabiri

Kwenye mechi zilizopita, Bayern Munich wamekuwa na changamoto kukabiliana na Real Madrid kwenye Uefa Champions League. Watabiri kadha wa kadha wanaipa Bayern Munich nafasi kubwa ya kuibuka na ushindi wa mechi hii. Ingia kwenye tovuti ya SportPesa na ubashiri matokeo ya mchezo huu wa Bayern Munich vs Real Madrid na ujishindie pesa taslimu.

Hitimisho

Bayern Munich vs Real Madrid ni mchezo mkubwa na mgumu kwa timu zote mbili, Real Madrid wanataka kufanikisha Remontada ili kuweka hai matumaini ya kushinda ubingwa mkubwa msimu huu. Presha ni kubwa kwa pande zote mbili kwani Bayern nao kipaumbele chao kikubwa ni ubingwa huu. Ingawa Real Madrid wana historia nzuri katika michuano hii, ubora wa Bayern wakiwa nyumbani pamoja na safu yao kali ya ushambuliaji utakuwa mtihani mkubwa na licha ya ugumu wa mchezo, Bayern wanatabiriwa ushindi.

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.