- Tanzania Premier League mchezo namba 54 wababe wamegawana alama mojamoja
- Fulltime: Yanga SC 0-0 Simba SC NBC Premier League 2025/26
- Simba SC walitawala kwenye eneo la kushambulia na mwisho wameambulia sare ugenini
Tambo kwishaa, sasa ni matamko. Baada ya matokeo ya Yanga SC 0-0 Simba SC katika mchezo wa dabi ya Kariakoo, maneno yamezidi kuwa mengi. Safu ya Waamuzi wa mchezo huo ikiogozwa na mwamuzi mkongwe, Nassor Mwinchui ikiacha gumzo. Wasemaji wa timu zote mbili wamechapisha matamko mazito.
SOMA HII PIA: Yanga SC vs Simba SC: Pacome ashtua, msimamo, Ratiba, Moto utawaka Kariakoo Dabi ya ‘Damaro Day’
Bado hujashinda mamilioni ya SportPesa?
Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Bashiri na SportPesa uvune mkwanja sasa hivi kwa kubonyeza picha hapo chini.

Yanga SC 0-0 Simba SC, nini kilitokea?

Huu ni mchezo ambao ulitawaliwa na ushindani mkubwa ndani nan je ya uwanja. Mlinda mlango wa Yanga SC, Djigui Diarra alifanya kazi kubwa kutimiza majukumu yake, ya kulinda lango la Yanga na hatimaye kutajwa kama mchezaji bora wa mechi. Mastaa wenguine waliong’aa katika mchezo huo ni Kibabage, Oura na Liombe wote wa Simba SC.
Simba SC walionekana kutawala sehemu kubwa ya mchezo huo, licha ya kwamba kulikuwa na vipindi vya timu zote kushambuliana kwa kushtukiza.
Matukio yaliyozua taharuki kwenye mechi ya Yanga SC vs Simba SC

Licha ya kwamba mchezo huo ulikuwa na matukio kadhaa ya utata. Matukio mawili ndiyo yanazungumzwa zaidi. Mosi ni tukio la ‘Offside’ ya Dube na la pili ni goli la Selemani Mwalimu kukataliwa. Kufuatia matukio haya kila upande umelalamika kudhulumiwa na Yanga SC.
SOMA HII ZAIDI: Yanga SC vs Simba SC matukio mawili makubwa kufanyika/ Waamuzi kutoka mataifa matatu
Kauli ya Ali Kamwe

Kufuatia matukio hayo, Ofisa Habari wa Yanga SC, Ali Kamwe amesema: “Tukio la goli la Selemani Mwalimu, kwanza ilikuwa ‘OFFSIDE’ pili akaushika mpira. Mchezo ukaruhusiwa kuendelea kama hakijatokea kitu. Sitaki kabisa kukumbusha kuwa mchezaji huyu alitakiwa kufungiwa mechi 5, kwa kosa la kumpiga kiwiko mchezaji wa Dodoma Jiji. Sitaki kuwakumbusha, kuwa Waamuzi walishatishiwa kufungiwa maisha kimpira na kupelekwa jela kuhusu mechi hii.
“Turidi uwanjani, Watu hawa baada ya mazoezi ya mwisho siku moja kabla ya mchezo, wakagoma kuondoka. Wakafanya Ushirikina na vurugu za kila aina, wakaja kutolewa kwa msaada wa Polisi. Hawakumaliza, Siku ya mechi wametumia mlango wa VVIP kuingia uwanjani, wakavunja mlango wa chumba cha waandishi wa Habari.
“Muda wa ‘Pitch Feeling’, wakautumia kuzunguka uwanja na kufanya vitendo vya kishirikina bila wasiwasi wowote. Hapa najaribu kuwaonyesha kwa uchache tu, nguvu iliyotumika hadi wamepata pointi 1 kwenye Dabi. Nguvu yote kubwa sana Iliyotumika ndani na nje ya uwanja, haijaweza kufuta Uteja wao. Wana kikosi chenye wachezaji machachari na Viongozi wenye mihemko.
Ahmed Ally ajibu mapigo

Naye Meneja wa Habari na mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally amesema: “Mnabahati sana nyie, tulikua tunawafanya vibaya. Gape la Pointi tano lililopo sasa katika msimamo wa ligi kuu, sio kwa ubora wao. Alipaswa kupoteza Mechi ya Namungo, au kupata Sare kila mtu anakumbuka kilichotokea hapo Ruangwa.
“Mechi yetu ya Derby tumenyimwa goli halali lisilokua na mashaka ndani yake. Kwenye Mechi hizi mbili alitakiwa kudondosha points 6 za wazi kabisa, lakini kwa hila ameokota points 5 zinazomfanya aongoze ligi na wala sio ubora.
SOMA HII PIA: Yanga SC vs Simba SC joto linazidi kupanda/ Ratiba, msimamo
Hitimisho msimamo unasemaje?
Matokeo ya Yanga SC 0-0 Simba SC yanaufanya msimamo uwe na mabadiliko madogo ya pointi. Yanga SC wanaendelea kuongoza msimamo na pointi zao 29. Nafasi ya pili inakamatiwa na Azam FC waliokusanya pointi 28, huku Simba SC wao wakiwa wamekusanya poiti 24 pekee. Hii inaonyesha taswira ya ushindani mkubwa uliopo baina ya timu za ligi Kuu Bara msimu huu.

