Jonathan Sowah amerejeshwa Simba SCMed Kicheko
  • Yanga SC vs Simba SC, Uwanja wa New Amaan Complex, NBC Premier League 2025/26.
  • Simba SC kuigomea Kariakoo Dabi? Sababu yatajwa.
  • Uongozi wa Simba SC umeandika barua Bodi ya Ligi kuhoji kuhusu mabadiliko ya uwanja kutangazwa na klabu.

Simba SC kuigomea Kariakoo Dabi? Ni swali linalohitaji majibu kutokana na tetesi kuanza kusikika. Yanga SC vs Simba SC ni New Amaan Complex, mchezo wa NBC Premier League 2025/26. Machi Mosi 2026 mchezo unatarajiwa kuchezwa, awali ulitarajiwa kupigwa Uwanja wa Mkapa.

SOMA HII: Yanga SC vs Simba SC joto linazidi kupanda/ Ratiba, msimamo

Cheza na ushinde sasa na ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa hivi

Hujashinda na kindege cha SportPesa? Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Bashiri na SportPesa uvune mkwanja sasa hivi.

Sportpesa Aviator- 800Mil

Simba SC kuigomea Kariakoo Dabi? Mabadiliko ya uwanja yatajwa

Simba SC kuigomea Kariakoo Dabi?
Clatous Chama kiungo wa Simba SC anayetarajiwa kuwa sehemu ya mchezo wa Dabi. Source: Simba SC.

Je Simba SC kuigomea Kariakoo Dabi? Majibu yatakuwa wazi hivi karibuni kutokana na fukuto linalotajwa kuendelea mitaa ya Msimbazi. Miongoni mwa sababu ni mabadiliko ya uwanja ambapo awali mchezo ulitarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa.

Taarifa rasmi iliyotolewa na Bodi ya Ligi Februari 16 ilieleza kuwa mchezo utachezwa Uwanja wa New Amaan Complex. Taarifa hiyo awali ilitolewa na Ofisa Habari wa Yanga SC, Ali Kamwe kabla ya bodi kutangaza. Mkanganyiko wa taarifa hiyo ukawaaibua Simba SC ambao wameandika barua bodi ya ligi kuhoji.

SOMA HII: Yanga SC vs Simba SC Uwanja wa New Amaan Complex/ Matokeo ya CAF Champions League

Sportpesa Aviator- 800Mil

Yanga SC vs Simba SC msimamo NBC Premier League 2025/26

 MPWDLPTS
3. Yanga SC871022
7. Simba SC861119

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari Simba SC ufafanuzi

Ahmed Semaji
Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari Simba SC. Source: Simba SC.

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC amekiri kuwa uongozi umeandika barua kwa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania, (TPLB). Aliongeza kuwa mchezo wa Yanga SC vs Simba SC sio mchezo mdogo hivyo taratibu lazima zifuatwe.

“Kwanza nikiri ni kweli tumeandika barua kwenda bodi ya ligi na siyo barua ya kulalamika. Ni barua ya kutaka kupata ufafanuzi zaidi. Mkubwa halalamiki. Barua yetu sio ya kulalamika yaani sisi Simba SC tumlalamikie nani? Kwa sababu kulalamika umeonewa halafu unalalamika. Sisi Simba SC nani wakutuonea nchi hii?

“Sisi tumeandika barua yakutaka kupata ufafanuzi juu ya baadhi ya mambo kuelekea mchezo wetu wa Machi Mosi. Hatutapenda kuweka wazi ni mambo gani ambayo tunataka kupatiwa ufafanuzi.

“Tunafanya hivyo ili kuepusha taharuki. Kwa sababu mechi ya Simba SC na Yanga SC ni mechi kubwa. Tumeandika hiyo barua imekwenda bodi ya ligi na mambo yanakwenda vizuri kwelikweli.

“Tusingependa kukimbilia kwenye jamii kwa kuwa mechi ya Simba SC na Yanga SC ni kubwa. Tumeandika hiyo barua imekwenda Bodi ya Ligi na barua imefika kwa bodi ya ligi. Na tumeshapata majibu na mambo mengine yataendelea.

Je Simba SC wanaogopa mchezo wa Kariakoo Dabi?

Simba SC vs Nsingizini Hotspurs CAF Champions League
Kapten Kapombe, nahodha wa Simba SC. Source: Simba SC.

“Sisi hatuogopi chochote, ambacho tunahitaji kuona ni kwamba kila kitu kinakwenda vizuri. Tupate uhalali wa kikanuni juu ya mambo haya. Kinachotushangaza sisi taarifa ya mabadiliko ya uwanja wa mchezo kwa nini yatangazwe na klabu kabla ya mamlaka ya mpira?

“Haijawahi kutokea mabadiliko ya uwanja yanatolewa na klabu kabla ya bodi ya ligi. Hapo ndipo tulipopata mashaka. Tunavyofahamu sisi mabadiliko yoyote yanatolewa na bodi ya ligi na sio klabu ama ofisa habari wa klabu husika,” alisema Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC.

SOMA HII: Dabi ya Kariakoo Yanga SC vs Simba SC ni Machi Mosi 2026/ NBC Premier League ratiba

Hitimisho

Simba SC kuigomea Kariakoo Dabi? Uwezekano unatajwa kuwa mdogo kutokana na mazungumzo yanayoendelea. Taarifa rasmi kuhusu hatma ya mchezo huo inatarajiwa kutolewa hivi karibuni kutoka mitaa ya Msimbazi.

Share this: