- Kiungo wa Yanga SC Mudathiri Yahya kuikosa mechi ya Simba SC Mei 3, 2026
- Taarifa rasmi kutoka TPLB imemtaja mchezaji Ibrahim Ibrahim wa Pamba Jiji FC kupigwa kiwiko
- Matokeo ya mchezo uliopita Yanga SC iliichapa Mbeya City 6-0 NBC Premier League
Kiungo wa Yanga SC Mudathiri Yahya kuikosa mechi ya Simba SC Mei 3, 2026. Sababu ya kuukosa mchezo huo ni adhabu ya kufungiwa mechi tatu na faini ya milioni 1. Mudathiri alifanya kosa la kumpiga mchezaji wa Pamba Jiji kiwiko mchezo uliochezwa Uwanja wa CCM Kirumba.
SOMA TAARIFA HII: Yanga SC: Historia, Usajili wote, kikosi, Ratiba, Matokeo na Takwimu
Bado hujashinda mamilioni ya aviator ‘Kindege’ cha SportPesa? Cheza ushinde mamilioni sasa hivi
Changamka! sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

Mudathiri kuikosa mechi ya Simba SC Mei 3, 2026

Ni wazi kuwa kiungo Mudathiri Yahya kuikosa mechi ya Simba SC Mei 3, 2026. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara, (TPLB). Katika mechi hizo tatu ipo ile ya Kariakoo Dabi.
Taarifa hiyo imeeleza: “Mchezaji Mudathir Yahya wa Klabu ya Yanga SC amefungiwa michezo mitatu (3) na kutozwa faini ya Sh. 1,000,000 (milioni moja) kwa kosa la kumpiga kiwiko mchezaji wa Pamba Jiji FC, Ibrahim Abraham wakati mchezo unaendelea kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
“Adhabu hii ni kwa mujibu wa Kanuni ya 41:5(5.2) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti kwa Wachezaji,” ilieleza taarifa hiyo iliyotolewa Aprili 20, 2026.

Mechi atakazokosekana Mudathir Yahya

Simba SC vs Yanga SC Mei 3, 2026
Yanga SC vs KMC, Mei 6, 2026
Yanga SC vs Coastal Union, Mei 9, 2026.
Wachezaji wengine waliopata adhabu Yanga SC
Mudathir Yahya sio mchezaji wa kwanza kufungiwa na TPLB kutokana na makosa ya utovu wa nidhamu. Beki Ibrahim Bacca naye aliwahi kufungiwa. Mlinda mlango namba moja Djigui Diarra anaingia kwenye orodha kwa kosa la kuonyesha dole la kati. Ikumbukwe kwamba katika mchezo dhidi ya Pamba Jiji FC alichaguliwa kuwa Man of The Match, (MoTM).
SOMA HII: Djigui Diarra amemaliza adhabu ya kufungiwa mechi 3 na TPLB
Hitimisho
SC Mudathiri Yahya kuikosa mechi ya Simba SC itakuwa ni adhabu yake ya kwanza msimu huu. Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza alikuwa huru na alishuhudia ubao ukisoma Yanga SC 0-0 Simba SC. Je mzunguko wa pili matokeo yatakuaje?

