- Djigui Diarra amemaliza adhabu yakufungiwa mechi 3 na TPLB
- Yanga SC vs Mbeya City ni ratiba inayofuata je ataanza langoni?
- Raia huyo wa Mali ana umri wa miaka 31 ni kipa namba moja kikosi cha wananchi
Djigui Diarra amemaliza adhabu yakufungiwa mechi 3 na TPLB (Bodi ya Ligi Kuu Tanzania). Sababu iliyofanya akutane na rungu hilo ni matukio ya utovu wa nidhamu mchezo wa Mtibwa Sugar 1-1 Yanga SC, uliochezwa Uwanja wa Jamhuri, Dodoma, Machi 21, 2026. Kipa huyo alitozwa jumla ya milioni kwa makosa tofauti.
SOMA HII: Djigui Diarra wa Yanga SC amefungiwa mechi 3 na TPLB
Paisha Kindege cha SportPesa uvune mamilioni sasa hivi
Muda ni sasa kushinda mamilioni ukicheza mchezo wa Aviator. Ni rahisi sana kwa kila rubani kuvuna mamilioni. Cheza sasa upate mgao wako bila chenga ni rahisi sana

Djigui Diarra amemaliza adhabu ya kufungiwa mechi 3 kuanza na Mbeya City

Djigui Diarra amemaliza adhabu ya kufungiwa mechi 3 na TPLB. Raia huyo wa Mali mwenye miaka 31 ni chaguo la kwanza kwa Kocha Mkuu, Pedro Goncalves. Anatarajiwa kurejea kwenye mchezo ujao wa ligi vs Mbeya City.
Yanga SC vs Mbeya City ni Aprili 16, 2026 Uwanja wa KMC Complex. Alipokuwa nje ya uwanja ni Aboutwalib Mshery na Hussen Masalanga walichukua mikoba yake. Mshery alianza mchezo dhidi ya Tanzania Prisons, Masalanga vs Pamba Jiji FC na ule dhidi ya TMA Stars.

Adhabu alizopewa Diarra na TPLB
Diarra alipewa adhabu yakufungiwa mechi 3 na kutozwa faini ya Sh. 2,000,000 (Milioni mbili) kwa kosa la kumshambulia mwamuzi baada ya mchezo kumalizika. (Kwa mujibu wa Kanuni ya 41:5(5.3). Pia alitozwa faini ya milioni mbili kwa kosa la kuonyesha kidole cha kati wakati akitoka uwanjani, kitendo kinachotafsiriwa ni utovu wa nidhamu. Kwa adhabu zote jumla ametozwa faini ya milioni 4.
Mechi ambazo alikosekana Diarra

Yanga SC 3-0 Tanzania Prisons, Uwanja wa KMC Complex, Aprili 4, 2026.
Pamba Jiji FC 0-3 Yanga SC, Uwanja wa Kirumba, Aprili 8, 2026
Yanga SC 1-0 TMA Stars, Aprili 11, 2026, Uwanja wa KMC Complex
SOMA HII: Tuzo ya kipa bora 2024/25 Camara wa Simba SC na Diarra wa Yanga SC vitani
Hitimisho
Djigui Diarra amemaliza adhabu ya kufungiwa mechi 3 na TPLB 2025/26. Kurejea kwake uwanjani kunaongeza machaguo kwa benchi la ufundi. Ni Mshery, Masalanga na Diarra watakuwa na kazi kwenye milingoti mitatu mechi zijazo.

