Namungo FC vs Simba SC NBC Premier League ni leoMpanzu- Lindi
  • Namungo FC vs Simba SC NBC Premier League ni leo
  • Simba SC 3-0 Namungo FC matokeo ya mchezo uliopita walipokutana NBC Premier League
  • Namungo FC haijashinda mchezo mbele ya mnyama kati ya mechi 13 ambazo wamekutana kwenye ligi

Namungo FC vs Simba SC NBC Premier League ni leo Jumapili, Aprili 19, 2026 saa 16:00 UTC. Tangu 2020, Namungo FC imecheza jumla ya mechi 13 na Simba SC. Ushinidi kwa mnyama ni mechi 8 huku sare zikiwa 5. Wauaji wa Kusini hawajapata ushindi katika mechi za NBC Premier League.

SOMA HII: Ratiba ya Simba SC NBC Premier League 2025/26 ni moto | Msimamo, Mzizima Dabi, Kariakoo Dabi

Bado hujashinda mamilioni ya SportPesa?

Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Bashiri na SportPesa uvune mkwanja sasa hivi kwa kubonyeza picha hapo chini.

SportPesa Aviator Challenge

Namungo FC vs Simba SC Premier League ni leo utabiri upoje

Namungo FC vs Simba SC NBC Premier League ni leo
Steve Berkar Kocha Mkuu wa Simba SC.

Wakati Namungo FC vs Simba SC Premier League ni leo utabiri wageni watapata ushindi. Licha ya ugumu wa mchezo rekodi zinaonyesha kwamba mnyama amekuwa na mwendo mzuri dhidi ya Namungo FC. Ikumbukwe kwamba mchezo uliopita Simba SC ilipata ushindi wa magoli 3-0 Fountain Gate.

Mchezo wa mwisho walipokutana Uwanja wa Mkapa ubao ulisoma Simba SC 3-0 Namungo FC . Beki Rushine alifunga goli moja na alichaguliwa kuwa Man of The Match. Leo kazi inatarajiwa kuwa kubwa kwa wapinzani hawa wawili.

Licha ya Simba SC kupewa nafasi kubwa kushinda bado Namungo FC sio timu yakubeza. Chini ya Juma Mgunda imecheza jumla ya mechi 18 ikipata ushindi mechi 5. Safu ya ulinzi imeruhusu magoli 19 ikiwa na pointi 22.

Udhaifu wa Namungo FC upo hapa

Ngoyi
Fabrince Ngoyi nyota wa Namungo FC.

Namungo FC udhaifu wake upo kwenye eneo la ulinzi. Imeruhusu kufungwa magoli 16 baada ya mechi 18. Safu ya ushambuliaji inayoongozwa na Fabrince Ngoyi imefunga jumla 16. Inakutana na safu ya Simba SC ambayo imeruhusu magoli 6.

Katika eneo la ushambuliaji, Namungo FC imeachwa kwa tofauti ya magoli 13 na ile ya mnyama. Wageni wamefunga magoli 29 hivyo kuna utofauti mkubwa kati yao. Ushindi ni mechi 5 ikipoteza mechi 7.

Kinara kwa utupiaji Namungo FC ni Ngoyi akiwa nayo 8. Upande wa Simba SC ni Seleman Mwalimu mwenye magoli 6. Vita yao inatarajiwa kuendelea leo katika uwanja ndani ya dakika 90 uwanjani.

SOMA HII: Mzizima Dabi yaiachia maumivu Simba SC 2025/26 | Highlights, msimamo, h2h, ratiba mechi zijazo

image

Ubora wa Namungo FC

Ubora wa Namungo FC ni kuwa imara wanapokuwa nyumbani. Mechi 9 ambazo wamecheza Uwanja wa Majaliwa, ushindi mechi 4 sare 4 wakipoteza mchezo mmoja. Hivyo kupata matokeo ya pointi 3 kwa Namungo FC kwa timu ngeni lazima zijipange kwelikweli.

Msimamo

Namungo FC ipo nafasi ya 10 kwenye ligi 2025/26. Inakutana na Simba SC iliyo nafasi ya pili na pointi 39. Mnyama amepoteza mchezo mmoja ilikuwa Simba SC 0-2 Azam FC.

Hitimisho

Namungo FC vs Simba SC NBC Premier League ni leo wababe hawa watakuwa uwanjani. Shomari Kapombe na Yusuph Kagoma wanatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi cha mnyama. Je Namungo FC watavunja rekodi ya kutofungwa leo?

Share this: