- Mudathir Yahya ameongeza mkataba wa miaka miwili kuendelea kuwa ndani ya kikosi cha Yanga SC msimu wa 2025/26 yupo mpaka 2027.
- Simba SC walikuwa wanatajwa kuwania saini ya kiungo huyo mwenye nguvu katika kutumia mguu wake wa kulia.
- Dickson Job kwenye orodha ya wachezaji wanaofuata kutambulishwa kuongeza mkataba wa miaka miwili.
Mudathir Yahya ameongeza mkataba wa miaka miwili ndani ya Yanga SC. Kiungo huyo alikuwa anatajwa kuwa kwenye rada za Simba SC hivyo wamepishana naye. Rasmi Julai 22 2025, Yanga SC wametangaza kukamilisha mpango wa kumuongezea mkataba wa miaka miwili.

Soma hii: Yanga SC imekomalia saini ya Balla Conte
Cheza Aviator uvune mamilioni sasa
Muda wakuvuna mamilioni huu hapa. Usichelewe cheza sasa Aviator upate mgao wako. Kila siku ni kushinda ukipaisha kindenge.

Mkataba wake uliisha baada ya msimu wa 2024/25 kukamilika. Atakuwa Jangwani kutimiza majukumu mpaka 2027. Ikumbukwe kwamba alisajiliwa na Yanga SC akiwa mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake Azam FC.
Rekodi za Mudathir Yahya
Mudathir Yahya ndani ya Ligi Kuu Tanzania Bara inayodhaminiwa na NBC alicheza jumla ya mechi 26. Katika mechi hizo alifunga mabao matatu na kutoa pasi nne za mabao. Alihusika kwenye mabao 7 kati ya 83 yaliyofungwa na Yanga SC.
Yanga SC ilikamilisha ligi ikiwa nafasi ya kwanza kwenye msimamo. Ni pointi 82 ilikusanya baada ya mechi 30. Ina kazi ya kutetea taji hilo kuelekea msimu wa 2025/26.
Wachezaji wengine wanaotajwa kuongezewa kandarasi Yanga SC
Dickson Job
Huyu ni beki anatarajiwa kuongezewa mkataba mpya. Mara baada ya msimu wa 2024/25 kukamilika naye mkataba wake ulisha. Kwa sasa ni mchezaji huru ila inaelezwa kuwa amepewa kandarasi ya miaka miwili kwa ajili ya kusaini Yanga SC.
Beki huyo yupo kwenye kambi ya timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars inayojiaanda na CHAN. Tanzania itakuwa na mchezo Agosti 2 2025, Uwanja wa Mkapa. Tanzania itacheza na Burkina Faso, ukiwa ni mchezo wa ufunguzi.
Pacome Zouzoua
Amefunga jumla ya mabao 12 na pasi 10 za mabao ndani ya ligi Pacome. Mkataba wake umeisha na mazungumzo yanaendelea. Alionyesha kiwango bora Juni alipocheza mechi tatu na kufunga mabao matatu. Miongoni mwa timu ambazo alizifunga ni Simba SC Kariakoo Dabi.
Pacome inaelezwa kuwa amepewa kandarasi ya miaka miwili ili aongeze kuendelea kubaki Jangwani. Kuna uwezekano mkubwa akasalia ndani ya Yanga SC. Kiungo huyo ni raia wa Ivory Coast mguu wake wenye nguvu ni ule wa kulia.
Maxi Nzengeli
Kwa msimu wa 2024/25 alifungua pazia la kufunga mabao ndani ya ligi. Maxi alifunga bao hilo kwenye mchezo dhidi ya Kagera Sugar uliochezwa Uwanja wa Kaitaba. Baada ya dakika 90 ilikuwa Kagera Sugar 0-2 Yanga SC.
Alitumia pasi ya Pacome kwenye mchezo huo. Nyota huyu mkataba wake naye umeisha. Inaelezwa kuwa ni kandarasi ya miaka miwili ataongeza.
Khalid Aucho
Khalid Aucho raia wa Uganda kandarasi yake imeisha. Inaelezwa kuwa dili jipya ambalo atasaini ni mwaka mmoja. Ikiwa watafikia makubalianao mazuri atabaki Jangwani ikishindikana huenda akaondoka bure.
Orodha ya wachezaji wanaotajwa kuachwa Yanga SC
Jonas Mkude
Kiungo mkabaji Jonas Mkude kandarasi yake imeisha. Aliongezewa mkataba wa mwaka mmoja kusalia Jangwani. Inatajwa kuwa Singida Black Stars wanahitaji huduma yake.
Kennedy Musonda
Mshambuliaji Kennedy Musonda anatajwa kuwa hatakuwa sehemu ya kikosi msimu ujao. Musonda mkataba wake naye umeisha. Inaelezwa kuwa hataongezewa mkataba mwingine.
Dennis Nkane
Kiungo mshambuliaji Dennis Nkane bado hajawa chaguo la kwanza ndani ya Yanga SC. Inatajwa kuwa huenda akasajiliwa na Singida Black Stars. Nyota huyu mzawa alifanya kazi na Miguel Gamondi ambaye kwa sasa yupo Singida Black Stars.
Tetesi za wachezaji wanaowindwa na Yanga SC
Feisal Salum – Yanga SC
Feisal Salum, kiungo wa Azam FC anatajwa kuwa kwenye rada za Yanga SC. Kiungo huyo mshambuliaji aliibuka Azam FC akitokea Yanga SC. Imekuwa inaelezwa kuwa huenda akarejea kwa mara nyingine Jangwani.
Taarifa zinaeleza kuwa mbali na Yanga SC kuiwinda saini ya kiungo huyo Simba SC nayo inaiwinda saini ya Feisal. Nyota huyo bado ana kandarasi ya mwaka mmoja na Azam FC. Ni pasi 13 za mabao alitengeneza na kufunga mabao manne msimu wa 2024/25 katika kikosi cha Azam FC kwenye NBC.
Mohamed Hussen Zimbwe Jr-Yanga SC

Beki huyu wa upande wa kushoto tayari amewaaga mashabiki wa Simba SC. Julai 19 Zimbwe Jr alibainisha kuwa hatakuwa ndani ya kikosi hicho. Ni miaka 11 alidumu kwenye maisha ya kutimiza majukumu ndani ya kikosi cha Simba SC.
Taarifa zinaeleza kuwa atajiunga na Yanga SC. Inaelezwa kuwa beki huyo kasaini dili la miaka miwili. Hivyo msimu wa 2025/26 atakuwa kijani na njano.
Edmund John – Yanga SC
Huyu ni winga mzawa mwenye ambaye ni mali ya Singida Black Stars. Taarifa zinaeleza kuwa tayari mazungumzo yameanza kufanyika. Ni suala la makubaliano na kutambulishwa ndani ya Yanga SC ni jambo ambalo limebaki.
Mshambuliaji Boyeli

Inaelezwa kuwa Yanga SC ipo kwenye mazungumzo na mshambuliaji Andy Boyeli. Nyota huyo anacheza Afrika Kusini katika timu inayoitwa Sekhukhune United ya Afrika kusini hiyo.Ujio wake utakuwa ni mbadala wa Kennedy Musonda ambaye anatajwa kutoongezewa mkataba.
Hitimisho
Yanga SC imekamilisha usajili wa mchezaji Balla Conte. Haya ni maandalizi kuelekea msimu wa 2025/26 unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa. Yanga SC ni mabingwa watetezi wa taji la Ligi Kuu Tanzania Bara inayodhaminiwa na NBC.


