- Seleman Mwalimu anaondoka Simba SC 2025/26
- Yanga SC yatajwa kuiwinda saini ya mshambuliaji tegemo unyamani
- Wydad Casablanca kukaa mezani na Simba SC kuzungumza hatma ya mchezaji huyo.
Seleman Mwalimu anaondoka Simba SC 2025/26 mara baada ya mkataba wake kuisha. Inaripotiwa mazungumzo yanaendelea kati ya uongozi wa Simba SC na Wydad Casablanca kuhusu mchezaji huyo. Mkataba wa mchezaji unatarajiwa kufika tamati Agosti 2026.
TAARIFA KUHUSU USAJILI: Usajili wa Chama Simba SC washtua! Mayele, Kagere, Okwi wafunguka Mazito
Je, bado hujashinda pesa? Cheza ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa
Ni zamu yako sasa, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

Seleman Mwalimu anaondoka Simba SC 2025/26, Yanga SC watajwa

Mshambuliaji Seleman Mwalimu anaondoka Simba SC 2025/26 pindi mkataba wake utakapoisha. Hiyo ni kutokana na makubaliano ya pande zote mbili. Upo uwezekano wa mchezaji huyo kuongeza mkataba endapo mazungumzo yatakwenda vizuri.
Mwalimu alitambulishwa rasmi Agosti 28 2025 kwa mkataba wa mkopo wa mwaka mmoja akitokea Wydad Casablanca ya Morocco. Mchezaji huyo wa zamani wa Fountain Gate ana miaka 20 ni mshambuliaji namba moja katika kikosi cha Steve Barker.
Alicheza Klabu ya KVZ ya Zanzibar kabla ya kusajiliwa na Fountain Gate ilikuwa Julai 15, 2024. Taarifa zinaeleza kuwa mchezaji huyo analipwa mshahara kati ya milioni 15-20 na gharama ya kukamilisha usajili wake inatajwa kuwa ni milioni 120.
SOMA HII: Seleman Mwalimu ametambulishwa Simba SC kwa mkopo akitokea Wydad | Takwimu zake, magoli

Yanga SC watajwa kuiwinda saini ya Mwalimu
Tetesi zinaeleza kuwa watani wa jadi wa Simba SC, Yanga SC wanaiwinda saini ya nyota huyo. Taarifa zinadai kwamba mabosi wa timu hiyo wanahitaji kuwa na mshambuliaji mzawa atakayeungana na Clement Mzize. Ikumbukwe kwamba Mzize yupo nje kwa muda kutokana na kutokuwa fiti.
Ikiwa Mwalimu hataongeza mkataba mwingine kuna uwezekano akahamia upande wa pili. Bado hazijathibitishwa kwa asilimia kubwa. Mchezaji mwenyewe hajazungumzia suala hilo kwa sasa.
Ameshuhudia mechi Yanga SC vs Mbeya City
Mwalimu ni miongoni mwa wachezaji walioshuhudia mchezo wa Yanga SC vs Mbeya City. Hiyo ilikuwa ni Uwanja wa KMC Complex, wananchi waliposhinda kwa magoli 6-0. Nyota huyo aliingia uwanjani kuwatazama Pacome Zouzoua, Hussen Masalanga, Mohamed Hussen.
Rekodi za Mwalimu

Mwalimu ndani ya Simba SC anaongoza kwa kufunga magoli mengi ambayo ni 6. Kwenye mchezo wa NBC Premier League vs Fountain Gate alitoa pasi moja ya goli. Ni mshambuliaji pekee aliyebaki kikosi cha kwanza mara baada Jonathan Sowah kusimamishwa kutokana na utovu wa nidhamu.
Taarifa zinaeleza kuwa Simba SC hawapo tayari kumuacha mchezaji huyo. Hiyo inatokana na uwezo alionao kwenye kufunga na kutoa pasi za magoli. Simba SC 3-1 Dodoma Jiji FC, CRDB Federation Cup alichaguliwa kuwa Man of The Match akipewa zawadi ya laki 5 na wadhamini.
Semaji kuhusu wachezaji kuondoka
Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC hivi karibuni alisema kuwa timu hiyo ina wachezaji wenye ubora. Kutajwa na timu nyingine inatokana na kile wanachoonyesha uwanjani. Aliongeza utaratibu ukifutwa hakuna kinachoshindikana.
“Tunaleta wachezaji wazuri na bora.Hilo linadhihirika kutokana na timu nyingi kuwahitaji. Kila mchezaji ambaye yupo Simba SC ana uwezo kucheza timu yoyote ile muhimu utaratibu ufuatwe,”.
Hitimisho
Seleman Mwalimu anaondoka Simba SC 2025/26 ikiwa hataongeza mkataba mwingine. Mabosi wa unyamani wanapambania kuhakikisha anabaki. Hiyo inatokana na mchango wake katika mechi za ushindani. Je atabaki Mwalimu ama atakuwa njano na kijani?

