Dodoma Jiji FC 0-0 Simba SCMpanzu vs Dodoma Jiji FC
  • Golikipa wa Dodoma Jiji FC, Daniel Mgore ametwaa tuzo ya man of the match
  • Dodoma Jiji FC 0-0 Simba SC Tanzania Premier League, Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.
  • Yanga SC vs Simba SC ni mchezo unaofuata kwa mnyama ikiwa ni Kariakoo Dabi

Dodoma Jiji FC 0-0 Simba SC wababe wamegawana alama mojamoja kwenye NBC Premier League 2025/26. Mnyama anapata sare ya kwanza ugenini Uwanja wa Jamhuri, Dodoma usiku. Kituo kinachofuata ni Yanga SC vs Simba SC, Machi Mosi 2026, Uwanja wa New Amaan Complex.

SOMA HII: Simba SC 3-0 Greenland FC CRDB Federation Cup/ Yanga SC vs Cosmopolitan FC, matokeo na ratiba

Je hujashinda? Cheza ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa hivi

Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

Sportpesa Aviator- 800Mil

Dodoma Jiji FC 0-0 Simba SC mlinda mlango Daniel Mgore atwaa tuzo

Dodoma Jiji FC 0-0 Simba SC
Mgore man of the match Dodoma Jiji FC 0-0 Simba SC. Source ligi.

Baada ya ubao wa Jamhuri, Dodoma kusoma  Dodoma Jiji FC 0-0 Simba SC mlinda mlango Daniel Mgore alitwaa tuzo. Hii inatokana na kuokoa michomo iliyokuwa inakwenda langoni mwake. Mbali na Mgore Andy Bikoko wa Dodoma Jiji FC naye alifanya kazi kubwa.

Hii inakuwa sare ya kwanza kwa mnyama mbele ya Dodoma Jiji FC. Rekodi zinaonyesha kuwa kwenye mechi 11, ushindi ni mechi 10 na sare 1 kwa mnyama.

Msimamo Dodoma Jiji FC vs Simba SC

 MPWDLPTS
3. Simba SC1072123
6.Dodoma Jiji FC1656521
Msimamo wa ligi
Msimamo wa ligi 2025/26.

Maoni ya kocha wa Dodoma Jiji

Amani Josiah, kocha wa Dodoma Jiji FC amebainisha wapinzani waliingia kwenye mfumo.

“Simba SC ni timu kubwa ila waliingia kwenye mfumo. Pongezi kwa wachezaji walifanya kazi kubwa licha ya kukosa ushindi,” alisema Josiah.

SOMA HII: Yanga SC yaichapa 5-0 JKT Tanzania NBC Premier League Simba SC anafuata/ Highlights, score, standings

Sportpesa Aviator- 800Mil

Maoni ya Kocha Mkuu wa Simba SC, Steve Barker

Dodoma Jiji FC 0-0 Simba SC
Nyota wa Simba SC akipambana na Dodoma Jiji FC.Source: Simba SC.

Kocha wa Mkuu wa Simba SC, Steve Barker alisema kuwa walishindwa kutumia nafasi ambazo walizipata kwenye mchezo.

 “Tulijiandaa kuwakabili Dodoma Jiji FC. Tulishindwa kutumia nafasi ambazo tulipata kwenye mchezo,” alisema Barker.

SOMA HII: Yanga SC 3-1 Dodoma Jiji FC NBC Premier League/ Highlights, stats

Hitimisho

Dodoma Jiji FC 0-0 Simba SC kila timu imevuna pointi moja. Unakuwa ni mchezo wa 11 kwa wababe hawa kumenyana katika ligi. Mnyama alipata ushindi mechi 10 na sare ya kwanza imepatikana msimu 2025/26.




Share this: