- Clatous Chama usajili wake umelipa CAF Champions League, NBC Premier League
- Mwamba wa Lusaka miaka 34 jezi yake inayomtambulisha uwanjani ni namba 17
- Simba SC ilimtambulisha Tanzania kwa mara ya kwanza 2018/19 akitokea Lusaka Dynamos FC
Clatous Chama usajili wake umelipa kwa mara nyingine Simba SC umelipa akitokea Singida Black Stars. Kiungo huyo mshambuliaji raia wa Zambia amezaliwa 18/06/1991 ana miaka 34. Jezi yake pendwa ni namba 17 alivaa hiyo hata alipokuwa ndani ya kikosi cha Yanga SC.
TAARIFA KUHUSU USAJILI: Usajili wa Chama Simba SC washtua! Mayele, Kagere, Okwi wafunguka Mazito
Bado hujashinda pesa? Cheza ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa
Ni zamu yako sasa, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

Clatous Chama usajili wake umelipa

Clatous Chama usajili wake umelipa kutokana na kuongeza nguvu eneo la kiungo mshambuliaji. Kwenye mechi za NBC Premier League 2025/26 ni chaguo la kwanza chini ya Kocha Mkuu, Steve Barker. Uwezo wake wakufunga na kutengeneza nafasi za magoli umekuwa mwendelezo kama alivyofanya mchezo dhidi ya Fountain Gate.
Timu kubwa zote amecheza Yanga SC na Simba SC kwa nyakati tofauti. Chama aliweka wazi kuwa atawekeza nguvu na nidhamu kwenye kutimiza majukumu yake. Kiungo huyo aliongeza kwamba ushindi ni kitu cha msingi.
“Nitawekeza nguvu katika nidhamu na ushirikiano. Haikunichukua ugumu mimi kurejea Simba SC kwa kuwa ni timu yenye ushindani. Kikubwa ni kuona tunapata matokeo mazuri kwenye mechi zetu,”.
Uhamisho wa Clatous Chama

| Msimu | Kutoka | Kwenda | Maelezo |
| 2013/14 | Nchanga Rangers FC | Zesco United | Uhamisho wa kwanza |
| 2016/17 | Zesco United | Ittihad Alexandria | Kuhamia Misri |
| 2016/17 | Ittihad Alexandria | Lusaka Dynamos FC | Alirejea Zambia ndani ya msimu huohuo |
| 2018/19 | Lusaka Dynamos FC | Simba SC | Maisha ligi ya Tanzania |
| 2021/22 | Simba SC | RS Berkane | Kuhamia Morocco |
| 2021/22 | RS Berkane | Simba SC | Alirejea Simba ndani ya msimu |
| 2024/25 | Simba SC | Young Africans (Yanga SC) | Uhamisho wa moja kwa moja kwa watani |
| 2025/26 | Young Africans (Yanga SC) | Singida Black Stars | Kuhamia Singida |
| 2025/26 | Singida Black Stars | Simba SC | Kurejea Simba tena |

Mechi za Chama timu ya taifa Zambia

| Mashindano | Mechi | Magoli | Asisti | Kadi ya Njano | Dakika |
| Africa Cup Qualifying | 15 | 1 | — | 1 | 879 |
| Mechi za Kirafiki (International) | 9 | 3 | — | 0 | 503 |
| Kufuzu Kombe la Dunia | 5 | 0 | — | 0 | 285 |
| African Nations Championship (CHAN) | 4 | 0 | — | 0 | 390 |
| Africa Cup of Nations (AFCON) | 2 | 1 | — | 0 | 21 |
| Jumla | 35 | 4 | 1 | 1 | 2,078 |
Mechi za Chama CAF akiwa Simba SC
| Msimu | Mechi | Magoli | Asisti | Dakika |
| 2018/19 | 10 | 2 | 2 | 758 |
| 2020/21 | 12 | 5 | 2 | 1,062 |
| 2022/23 | 12 | 5 | 1 | 1,080 |
| 2023/24 | 10 | 3 | 1 | 671 |
| 2025/26 | 4 | 0 | 1 | 315 |
| Jumla | 48 | 15 | 7 | 3,886 |
Mechi za CAF akiwa Yanga SC
| Msimu | Mechi | Magoli | Asisti | Dakika |
| 2024/25 | 9 | 3 | 4 | 370 |
| Jumla | 9 | 3 | 4 | 370 |
Jumla ya mechi za CAF Simba SC na Yanga SC
| Kipengele | Takwimu |
| Mechi | 57 |
| Magoli | 18 |
| Asisti | 11 |
| Dakika | 4,256 |
SOMA HII: Seleman Mwalimu anaondoka Simba SC 2025/26 | Yanga SC watajwa
Hitimisho
Clatous Chama usajili wake umelipa kwa mara nyingine Msimbazi. Kwenye mechi muhimu amekuwa akiongeza nguvu eneo la kutengeneza nafasi. Alisajiliwa unyamani dirisha dogo akitokea Singida Black Stars.

