- Kitaeleweka kesho Ijumaa Aprili 17, 2026 jijini Dar es Salaam, ni katika droo ya Robo Fainali CRDB federation Cup.
- Droo hii itafanyika kuanzia saa 6:00 mchana EAT, hii ni mara baada ya hatua ya 16 bora kumalizika kwa kishindo.
- hatimaye droo ya hatua ya Robo Fainali ya mashindano itafanyika ambapo kila timu itafahamu watakutana dhidi ya mpinzani gani.
- Ikumbukwe mpaka sasa zimesalia timu 8 tu ambazo ni; Yanga SC, Simba SC, Azam FC, Singida United, TRA United, JKT Tanzania, Mashujaa FC, na Coastal Union.
Historia itaandikwa kesho Ijumaa Aprili 17, 2026 jijini Dar es Salaam. Hii ni mara baada ya hatua ya 16 bora ya Kombe la CRDB Bank Federation Cup kumalizika kwa kishindo, hatimaye droo ya hatua ya Robo Fainali ya mashindano itafanyika ambapo kila timu itafahamu watakutana dhidi ya mpinzani gani. Ikumbukwe mpaka sasa zimesalia timu 8 tu ambazo ni; Yanga SC, Simba SC, Azam FC, Singida United, TRA United, JKT Tanzania, Mashujaa FC, na Coastal Union. Droo hii itafanyika kuanzia saa 6:00 mchana EAT.
SOMA HII PIA: Matokeo: Yanga SC (1) vs TMA Stars (0) CRDB Federation Cup | Highlights, goal, stats
Je, wajua? Unaweza kushinda mpaka Shilingi Milioni 800 na SportPesa
Wengi tayari wamevuna mamilioni kupitia mchezo wa Kindege yaani ‘Aviator’ ya SportPesa. Wewe unasubiri nini? Nafasi ni yako cheza Aviator na kushinda mpaka Shilingi Milioni 800 sasa kwa kubonyeza picha hii chini.

Kuhusu droo ya Robo Fainali ya Kombe la CRDB Federation Cup

Droo ya Robo Fainali ya mashindano ya CRDB Federation Cup, ni hatua ya mashindano ambayo imefikiwa mara baada ya kumalizika kwa hatua tatu ambazo ni 64 bora, 32 bora na 16 bora. Droo hufanyika kwa mfumo wa machaguo ya chungu ‘Pot’, Pot hizi zinatarajiwa kuwa na timu nane ambazo ni; Yanga SC, Simba SC, Azam FC, Singida United, TRA United, JKT Tanzania, Mashujaa FC, na Coastal Union. Yoyote kati ya timu hizi, ana nafasi ya kukutana na timu nyingine.
Ratiba ya Robo Fainali ya CRDB Confederation Cup
Robo fainali ya mashindano ya Kombe la Shirikisho la CRDB imepangwa kupigwa Mei 16 na Mei 17, mwaka huu. Hii ina maana mechi mbili za Robo Fainali ya kwanza zitapigwa Mei 16 na zile za Robo Fainali ya 2 zitapigwa Mei 17. Kuhusu ratiba ya mud ana Uwanja upi utatumika kwa kila mechi, itajulikana mara baada ya droo ya kesho.
SOMA HII ZAIDI: Yanga SC ina Unbeaten 27 CRDB Federation Cup | Mataji miaka minne mfululizo
Timu za Ligi Kuu Bara zaandika rekodi

Kwa mara ya kwanza msimu huu, droo ya Robo Fainali haitashuhudia timu ya Championship. Droo hiyo inahusisha timu za Ligi Kuu Bara pekee, na ni kama imepewa jina la Droo ya wakubwa. Mpaka kufikia hatua ya 16 bora, zilisalia timu 3 pekee kutoka Championship ambazo pia zilikutana na vipigo.
Yanga SC hawakamatiki ‘Unbeaten 27’
Mabingwa watetezi wa mashindano hayo Yanga SC wanaendelea kutikisa. Hii ni baada ya kufikisha mechi 27, bila kupoteza mchezo yaani ‘Unbeaten’. Yanga SC walifikisha rekodi hiyo baada ya kuichapa TMA Stars ya Arusha bao 1-0 lililofungwa na Maxi Nzengeli Aprili 11, 2026.
SOMA HII PIA: Simba SC yajivunia ubora wa kikosi 2025/26 | Fixture, Standings
Yanga SC mabingwa mara 9

Achana na rekodi ya ‘unbeaten’ 27, Ikumbukwe Yanga SC bado wanashikilia rekodi ya kuwa mabingwa wa kihistoria wa mashindano hayo. Hii ni baada ya kutwaa ubingwa huo mara 9, huku mara 4 ikiwa ni katika misimu 4 iliyopita. Kama watashinda tena ubingwa huo msimu huu, inamaanisha watafanya hivyo mara ya 10. Yanga SC wanafuatiwa na watani zao wa jadi Simba SC, ambao wamebeba ubingwa mara 4.

