- Yanga SC (1) vs TMA Stars (0) ndio matokeo kamili CRDB Federation Cup raundi ya 16 bora.
- Maxi Nzengeli ndiye aliyewafungia wananchi goli la kipekee kwenye dakika ya 76 lililoipeleka timu hiyo robo fainali ya kombe hili.
- Mchezo huu wa kukata na shoka ulichezwa Uwanja wa KMC Complex, Aprili 11, 2026 saa 12:30 jioni.
Yanga SC (1) vs TMA Stars (0) ndio matokeo rasmi kwenye mchezo wa CRDB Federation Cup iliyopigwa Uwanja wa KMC Complex. Mechi hii ilionekana kuwa na ushindani mkubwa kwa kuangalia head to head dhidi ya TMA Stars kutokuwa ya mara nyingi. Licha ya hilo, mchezaji Maxi Nzengeli alifunga goli pekee kwa Yanga SC likiipa tiketi ya kufuzu robo fainali.
Je, bado hujashinda mamilioni ya aviator ‘Kindege’ cha SportPesa? Cheza ushinde mamilioni sasa
Changamka! sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

Yanga SC (1) vs TMA Stars (0) CRDB Federation Cup

Yanga SC (1) vs TMA Stars (0) mabingwa watetezi wakiendeleza rekodi yakutopoteza mchezo kwenye mashindano haya. Dakika 45 za mwanzo wanaume 22 uwanjani walitoshana nguvu kwa kwenda mapumziko bila kufungana. Kipindi cha pili goli la ushindi lilipatikana zikiwa zimesalia dakika 20 mchezo kufika tamati.
Pacome Zouzoua alitoa pasi kwa Edmund John aliyempa pasi Maxi aliyefunga goli la ushindi. Hilo lilikuwa ni goli la juhudi kwa timu ya Yanga SC wakiwa nyumbani. Ukuta wa TMA Stars ulifunguliwa kipindi cha pili na kuruhusu goli moja.
SOMA HII: Yanga SC yatambulisha mashine mpya nne 2025/26 | Benchi la ufundi balaa zito

Maxi azawadiwa laki 5 na wadhamani
Mara baada ya mchezo wa leo kiungo wa Yanga SC, Maxi Nzengeli amezawadiwa kiasi cha shilingi laki 5 na wadhamini CRDB. Hii ni mara baada ya kuchaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo. Nzengeli alionyesha kiwango bora na utulivu kwenye kubadili matokeo katika mchezo muhimu.
Yanga SC chini ya Kocha Mkuu, Pedro Goncalves imefungua safari nyingine kulifukuzia taji wanalolitetea. Ili kutinga hatua ya nusu fainali itapaswa kushinda mchezo ujao wa hatua ya robo fainali. Timu hiyo imekuwa kwenye mwendo bora kwenye mashindano ya ndani.
Coastal Union 2-0 Pamba Jiji FC

Coastal Union imepata ushindi wa magoli 2-0 Pamba Jiji FC. Ni kwenye mchezo wa mapema saa 10:00 jioni, Uwanja wa Mkwakwani, Tanga robo fainali. Magoli ya Coastal Union yamefungwa na Gradi Lassa Kiala dakika ya 30 na Ally Msangi dakika ya 35. Ni Ally Msangi alichaguliwa kuwa mchezaji bora akipata zawadi ya laki 5.
Ratiba ya hatua ya 16 bora Aprili 12, 2026
Simba SC vs Dodoma Jiji FC, saa 10:00 jioni
Singida Black Stars vs Mbeya City, saa 10:00 jioni
Namungo FC vs TRA United, saa 10:00 jioni
Azam FC vs Fountain Gate, saa 1:00 usiku.
SOMA HII: Yanga SC: Historia, Usajili wote, kikosi, Ratiba, Matokeo na Takwimu
Hitimisho
Yanga SC (1) vs TMA Stars (0) CRDB Federation Cup wenyeji wakitinga hatua ya robo fainali. Mabingwa hawa watetezi walitinga hatua ya 16 bora kwa kuichapa Polisi Tanzania 7-1 katika hatua ya 32 bora. Depu aliandika rekodi kwenye mchezo huo kwa kufunga hat trick, Uwanja wa KMC Complex.

