Yanga SC (6) VS Mbeya City (0)Pacome vs Mbeya City
  • Yanga SC (6) VS Mbeya City (0) NBC Premier League, Aprili 16, 2026
  • Pacome Zouzoua amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo
  • Kocha Mecky Maxime afukuzwa kazi mara baada ya kipigo kutoka kwa wananchi

Yanga SC (6) VS Mbeya City (0) NBC Premier League ni matokeo rasmi mchezo uliochezwa Uwanja wa KMC Complex. Wafungaji hvii punde ni Pacome Zouzoa magoli mawili dakika ya 10 na 44. Prince Dube magoli mawili dakika ya 7 na 82. Maxi Nzengeli goli moja dakika ya 16 na Zimbwe Jr goli moja dakika ya 45+2.

TAARIFA KUHUSU USAJILI: Yanga SC: Historia, Usajili wote, kikosi, Ratiba, Matokeo na Takwimu

Je, bado hujashinda mamilioni ya aviator ‘Kindege’ cha SportPesa? Cheza ushinde mamilioni sasa

Changamka! sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

Aviator game jackpot banner TSh 800 Million prize

Yanga SC (6) vs Mbeya City (0) NBC Premier League

Yanga SC (6) VS Mbeya City (0)
Zimbwe Jr beki wa Yanga SC. Source: Yanga SC.

Mabingwa watetezi Yanga SC (6) vs Mbeya City (0) NBC Premier League. Kurejea kwa Prince Dube kumeogeza nguvu eneo la safu ya ushambuliaji. Kiungo mshambuliaji Allen Okelo ambaye ni ingizo jipya alitoa pasi ya goli katika mchezo ikitumiwa na Zimbwe Jr.

Huu unakuwa ni mchezo wa 19 kwa Yanga ikiwa haijapoteza ndani ya ligi. Inaongoza msimamo na pointi 47. Mbeya City kwenye msimamo ipo nafasi ya 13 baada ya mechi 19 imekusanya jumla ya pointi 17.

Takwimu mchezo Yanga SC 6-0 Mbeya City FC

Yanga SC (6) VS Mbeya City (0)
Pacome na tuzo ya mchezaji bora wa mchezo. Source: Yanga SC

Ratiba ijayo kwa Yanga SC baada ya kumalizana na Mbeya City ni Mei 3, 2026 dhidi ya Simba SC. Mchezaji Pacome ambaye alifunga magoli mawili alichaguliwa kuwa mchezaji bora. Wananchi walifurahia burudani kutoka kwa wachezaji wao waliokuwa kwenye kiwango.

Yanga SC Mbeya City FC
13Mashuti4
9Lenga lango1
60%Umiliki40%
4Mashuti yasiyolenga lango3
0Kadi nyekundu0
1Kadi ya njano1
8Kona3
6Magoli0

Kiungo Allen Okello anaongoza chati ya watoa pasi za magoli

Star Boy, Allen Okello anaongoza kwenye chati ya waota pasi za magoli 2025/26. Pasi yake aliyompa Zimbwe Jr inamfanya afikisha pasi 6. Huyu ni mchezaji mpya ambaye alisajiliwa katika dirisha dogo la usajili.

Amecheza mechi 12, ametoa akifunga magoli mawili. Katika mabao 44 yaliyofungwa na Yanga SC inayofundishwa na Kocha Mkuu, Pedro Goncalves amehusika katika magoli 8. Alisajiliwa akitokea Klabu ya Vipers ya Uganda.

SOMA HII: Allan Okelo Star Boy aliyetikisa katika usajili na anachokifanya Yanga SC | Twakimu, goli lake la kwanza 2025/26 | CAF Champions League

Aviator game jackpot banner TSh 800 Million prize

Kocha Maxime afukuzwa kazi baada ya kipigo

Mecky
Mecky aliyekuwa kocha wa Mbeya City. Source: Mbeya City.

Muda mchache baada ya Mbeya City kupokea kipigo taarifa rasmi ilitolewa kuhusu kusitisha mkataba wa kocha Mecky Maxime. Timu hiyo ilianza msimu wa 2025/26 haijawa na matokeo mazuri. Taarifa imeeleza namna hii:-

“Klabu ya Mbeya City FC imefikia makubaliano ya pande zote mbili kusitisha mkataba wa kocha Mecky Maxime pamoja na wasaidizi wake Nizar Khalfa na Francis Mkanula kocha wa utimamu wa mwili. Tunatambua na kutahamini jitihada walizofanya katika kuboresha utendaji wa timu yetu na tunamshukuru kwa mchango wake uliotukuka. Tunamtakia kocha na wasaidizi wake kila la kheri,”.

SOMA HII: Yanga SC na maajabu 2025/26 | Matokeo ya hivi punde, wafungaji na msimamo NBC Premier League

Hitimisho

Yanga SC (6) VS Mbeya City (0) NBC Premier League mvua ya magoli ilikuwa kwa wageni. Wananchi wanavuna pointi 4 dhidi ya wakusanya mapato wa Mbeya. Wanajikita kileleni wakiwaacha watani zao wa jadi Simba SC kwa tofauti ya pointi 8.

Share this: