Yanga SC vs Mbeya CityYanga SC vs Mbeya City
  • Ni Yanga SC vs Mbeya City kuumana kwenye Uwanja wa KMC Complex, Dar es Salaam kesho Alhamisi.
  • Hii ni katika mfululizo wa mechi za Ligi Kuu Bara (NBC Premier League).
  • Baada ya Mnyama kumaliza na kicheko cha ushindi wa Simba SC 3-0 Fountain Gate FC leo Jumatano, kesho Alhamisi ni zamu ya Wananchi Yanga SC.
  • Je, Diarra atacheza? Kipa huyo amerejea kikosini baada ya kumaliza adhabu.

Yanga SC vs Mbeya City kitaumana kwenye Uwanja wa KMC Complex, Dar es Salaam kesho Alhamisi. Hii ni katika mfululizo wa mechi za Ligi Kuu Bara (NBC Premier League). Baada ya Mnyama kumaliza na kicheko cha ushindi wa Simba SC 3-0 Fountain Gate FC leo Jumatano, kesho Alhamisi ni zamu ya Wananchi Yanga SC. Habari njema kwa Wananchi ni kurejea kikosini kwa kipa wao namba moja, Djigui Diarra ambaye amemaliza adhabu.

Fuatilia matukio ya karibuni ya mashindano ya NBC Champions League, mabao, takwimu na habari za hivi sasa kupitia SportPesa blog

SOMA HII PIA: Yanga SC vs Mbeya City Septemba 30 | H2H, vikosi, takwimu muhimu

Je, bado hujashinda na SportPesa? Cheza mchezo wa aviator ‘Kindege’ uvune mpaka milioni 800 sasa

Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

Aviator game jackpot banner TSh 800 Million prize
Rukia ushindi! 🛫 Win up to TSh 800,000,000 with Aviator. Cheza leo

Yanga SC vs Mbeya City h2h

Rekodi zinaonyesha Yanga SC na Mbeya City zimekutana katika michezo 19, ya mashindano tofauti. Yanga SC wamekuwa na rekodi bora dhidi ya wapinzani wao, hii ni baada ya kuandikisha ushindi mara 10. Mbeya City wameibuka na ushindi mara 1 pekee dhidi ya Yanga SC, huku mechi 8 zikiisha kwa sare.

Kikosi cha Yanga SC kinachotarajia kuanza mchezo huu

Kikosi cha Yanga SC
Kikosi cha Yanga SC

Kuelekea katika mchezo huu Yanga SC itaendelea kukosa baadhi ya mastaa wao walio majeruhi. Pamoja na wachezaji walio majeruhi, wapo pia wanaotumikia adhabu za kadi. Kuendana na mazoezi ya mwisho Yanga SC wanatarajia kuanza na kikosi hiki;

Kipa: Djigui Diarra

Walinzi: Mwenda, Baka, Mwamnyeto, Mohammed Hussein

Viungo: Duke, Pacome, Maxi, Damaro na Okello

Mshambuliaji: Dube

Taarifa ya benchi la ufundi Yanga SC

Yanga SC vs Mbeya City
Kocha Pedro

Kuelekea mchezo huo, kocha mkuu wa Yanga Pedro amesema: “Mchezo wa mwisho nillifanya mabadiliko kadhaa ili kutoa fursa kwa baadhi ya wachezaji kupata utimamu wa kimwili, ulikuwa wasaa mzuri pia kupumzisha baadhi ya nyota wetu. Hivyo nina matarajio kesho ufanisi wa wachezaji wangu utakuwa mkubwa, na malengo yetu ni kupata alama 3. Mechi ya mwisho ugenini dhidi ya Mbeya City, ulikuwa mchezo mgumu sana kutokana na hali ya uwanja.”

“Kesho tutacheza kwenye mazingira tofauti ambayo tumeyazoea, tupo imara zaidi na tunauhitaji mkubwa wa pointi 3. Nafahamu hata wao wanahitaji pointi lakini kwetu ni hadithi nyingine, ninajiamini kwa kiwango kikubwa. Licha ya kwamba tunahitaji alama 3 kwa namna yoyote, lakini tunapaswa kuwa na tahadhari. Lazima tuwaheshimu wapinzani wetu.”

SOMA HII ZAIDI:Yanga SC: Historia, Usajili wote, kikosi, Ratiba, Matokeo na Takwimu

Taarifa za majeruhi; Dube arejea, Depu bado

Kocha Pedro akizungumzia hali ya majeruhi wa kikosi amesema: “Prince Dube amerejea, mchezo uliopita alipata dakika 14 baada ya kutoka kwenye majeraha, ujio wake utaongeza nguvu na ufanisi kwenye eneo la ushambuliaji. Bado Depu hajaanza kurejea uwanjani, hivyo kurejea kwa Dube kutaongeza nguvu kwa washambuliaji. Tunaratajia kumkosa Mwanengo pia, lakini ni kazi yetu kama benchi la ufundi kutafuta njia mbadala ya kuziba pengo la majeraha”

Diarra amaliza adhabu arejea

Djigui Diarra wa Yanga SC amefungiwa mechi 3 na TPLB
Djigui

Mlinda mlango namba 1 wa Yanga SC, Djigui Diarra rasmi amemaliza adhabu yake na anatarajiwa kurejea uwanjani. Ikumbukwe, Diarra kupitia Kamati ya masaa 72 alikutwa na hatia ya utovu wa nidhamu mara baada ya mchezo wao na Mtibwa Sugar, ambapo kufuatia vitendo hivyo alifungiwa mechi 3 na kutozwa faini ya Shilingi Milioni 4 za Kitanzania. Diarra raia wa Mali mwenye miaka 31, alikosa  mechi hizi dhidi ya Tanzania Prisons, Pamba Jiji FC na TMA Stars.

Utabiri

Yanga wanapewa nafasi kubwa ya kuibuka na ushindi katika mchezo huu, hasa kutokana na ubora ambao wameuonyesha kwenye mexhi 3 mfululizo zilizopita. Mbeya City ni miongoni mwa timu chache, ambazo bado hazijapoteza mchezo dhidi ya Yanga SC msimu huu. Matokeo ya sare baina ya timu hizi yaliyopatikana jijini Mbeya, yanazidi kuufanya mchezo kuwa mgumu.

SOMA HII PIA: Yanga SC bado ipo kazini, ratiba ya NBC Premier League, msimamo wa 5 bora

Hitimisho

Yanga SC ina Unbeaten 27 CRDB Federation Cup
Yao

Yanga SC vs Mbeya City ni miongoni mwa michezo migumu ambayo haijawahi kutabirika. Mchezo wa mzunguko wa kwanza Yanga SC walilazimishwa sare, hii inadhihirisha ushindani huu. Kukosekana kwa baadhi ya mastaa wa Yanga SC kunatarajiwa kuwa changamoto kubwa kwa Wananchi.

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.