Simba SC vs Azam FCZidaneee
  • Yanga SC vs Simba SC Kariakoo Dabi yanukia Zanzibar Januari 2026
  • Simba SC vs Azam FC 2026 NMB Mapinduzi Cup ni Mzizima Dabi visiwani
  • Steve Barker kocha mpya Simba SC kwenye mtihani mgumu kufuta Simba SC 0-2 Azam FC mchezo wa NBC League.

Simba SC vs Azam FC ni mchezo unaofuata NMB Mapinduzi Cup. Hii ni hatua ya nusu fainali ya kwanza Uwanja wa New Amaan Complex saa 2:15 usiku. Mshindi wa mchezo atakutana na mshindi wa nusu fainali ya pili Yanga SC vs Singida Black Stars. Kocha Mkuu wa Simba SC, Steve Barker katika kibarua kufuta Simba SC 0-2 Azam FC mchezo uliopita wa NBC League.

SOMA HII: Simba SC 0-2 Azam FC ni matokeo yaliyovunja rekodi/ Ratiba ya mechi zijazo CAF Champions League

Vuna mamilioni sasa hivi

Kuna jambo umekwama kwa sasa kuhusu mkwanja? Usiogope, rubani ni jasiri na kazi yake ni kupaisha kindege cha SportPesa. Cheza sasa hivi Aviator uvune mamilioni bofya hapa chini, muda ni wako na nafasi ya ushindi inakusubiri.

image

Simba SC vs Azam FC matokeo yao NMB Mapinduzi Cup 2026

Simba SC vs Azam FC
Kitambala nyota wa Azam FC. Source: Azam FC.

Simba SC vs Azam FC mpaka zinakutana zilianzia hatua ya makundi. Azam FC ilicheza mechi tatu huku Simba SC ikicheza mechi mbili. Ushindi kwa Simba SC ni mechi zote mbili huku Azam FC ikishinda mbili na kulazimisha sare mchezo mmoja. Kariakoo Dabi inanukia ikiwa Simba SC atapata ushindi na Yanga SC atashinda nusu fainali ya pili.

Utabiri wa matokeo Simba SC vs Azam FC

Kwenye mchezo wa nusu fainali ya kwanza ni matajiri Azam FC wanapewa nafasi kubwa yakushinda. Hii inatokana na aina ya wachezaji walionao, spidi na ubora kwenye kutumia nafasi. Simba SC licha yakupewa nafasi ndogo sio timu ya kuibeza.

Matokeo ya Simba SC NMB Mapinduzi Cup

 Januari 3,2026

Simba SC 1-0 Muembe Makumbi City

Mfungaji:-Bajaber

Januari 5,2026

Fufuni FC 1-2 Simba SC

Wafungaji:-Hassan Mbegu na Nabby Camara

SOMA HII: Matokeo ya Simba SC 2025/26 | Ratiba, vinara wa ufungaji

image

Kikosi cha Simba SC kinachotarajiwa kuanza

Mlinda mlango

Hussen Abel

Mabeki

Duchu

Mligo

Chamou

De Reuck

Viungo

Kante

Chasambi

Naby Camara

Ellie Mpanzu

Neo Maema

Bajaber

Matokeo ya Azam FC NMB Mapinduzi Cup

Himid
Wachezaji wa Azam FC NMB Mapinduzi Cup 2026. Source: Azam FC.

Desemba 31,2025

Azam FC 1-1 Singida Black Stars

Mfungaji:-Kitambala Jephte

Januari 2,2026

Azam FC 2-0 Mlandege

Wafungaji:-Zidane na Himid Mao

Januari 5,2026

Azam FC 2-1 URA Uganda

Wafungaji:-Kitambala Jephte na Alobogast

Kikosi cha Azam FC kinachotarajiwa kuanza

Langoni

Air Manula

Chilambo

Zouzou

Lawi

Twalib

Himid

Zidane

Kibeku

Kitambala

Akaminko

Diakite

Wachezaji wakuchungwa kwa Simba SC

Nabby Camara

Nyota huyu alishikilia ufunguo wa ushindi mchezo dhidi ya Fufuni kwa goli la jioni. Ni imara katika kuzuia na kushambulia. Uwezo wake kwenye mguu wa kulia umekuwa na hatari kwa wapinzani.

Ellie Mpanzu

Mpanzu S
Mpanzu Ellie nyota wa kikosi cha Simba SC. Source: Simba SC.

Licha ya kiwango chake kutokuwa kwenye ubora ni mchezaji tegemeo. Kurejea kwake kikosi cha kwanza kunaongeza nguvu kwa Simba SC na hatari kwa wapinzani. Ni mchezaji mwenye spidi na maamuzi ya haraka kwenye kushambulia.

De Reuck

Beki huyu alikuwa nje kwa muda kutokana na kutokuwa fiti. Amerejea uwanjani hivyo hatari yake akiachwa huwa ni kubwa. Uwezo kwenye matumizi ya mipira ya adhabu katika kufunga upo kwenye miguu yake.

Wachezaji wakuchungwa kwa Azam FC

Zidane

Ni kiungo mwenye hatari akiwa uwanjani. Kwenye mechi kubwa amekuwa na matokeo mazuri kutokana na kujihatarisha mara nyingi. Simba SC wanamkumbuka kwenye mchezo wa ligi 2024/25 aliwafunga goli dakika ya 88.

Kitambala

Kwenye Mapinduzi Cup amefunga magoli mawili katika mechi tatu.Ni mchezaji ambaye anapenda kufunga akiwa uwanjani. Uwezo wake katika maamuzi ya haraka ni kitu cha kutazamwa na wapinzani Simba SC.

Alobogast

Mshambuluaji ambaye amekwenda hewani matumizi ya nguvu na akili. Ni mchezaji anayepaswa kutazamwa kwa ukaribu kutokana na uwezo wake katika kufunga.

SOMA HII: Simba SC ina mgogoro mzito kwa sasa? Ukweli huu hapa/ Mo na Mangungu sakata lipo hivi

image

Maneno ya makocha wa Simba SC vs Azam FC

Steve Barker, Kocha Mkuu wa Simba SC amesema wanatambua utakuwa mchezo mgumu. Maandalizi yamefanyika ili kupata matokeo mazuri.

“Tutakuwa na mchezo mgumu lakini tumefanya maandalizi mazuri.Kikubwa ambacho tunahitaji ni matokeo mazuri,”.

Florent Ibenge, Kocha Mkuu wa Azam FC amesema kutakuwa na mabadiliko kwenye kikosi na watacheza kama siku zote. Malengo makubwa ni kupata ushindi.

“Tumefanya maandalizi mazuri na tupotayari kwa mchezo. Kutakuwa na mabadiliko kwenye kikosi ila malengo ni kupata matokeo mazuri,”.

Hitimisho

Simba SC vs Azam FC mchezo wa nusu fainali NMB Mapinduzi Cup itaamua nani kwenda hatua ya fainali. Mshindi wa mchezo Januari 9 atakuwa jukwaani kuwatazama Yanga SC vs Singida Black Stars nusu fainali ya pili. Je inawezekana Kariakoo Dabi ya Yanga SC vs Simba SC kuanza visiwani? Matokeo yataamua.

Share this: