- Utamu wa mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2025) unazidi kunoga.
- Mashindano hayo yanayoendelea kutimua vumbi nchini Morocco, sasa yameingia katika hatua ya Robo Fainali.
- Tayari timu 6 zimeshakata tiketi, na zinasubiriwa timu mbili kutoka kwenye mipambano ya usiku huu.
- Makala hii inaangazia nani wamefuzu, mwenendo wa matokeo na ratiba kuelekea Robo Fainali.
Utamu unazidi kwenye mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2025). Mashindano hayo yanayoendelea kutimua vumbi nchini Morocco, sasa yameingia katika hatua ya Robo Fainali. Tayari timu sita zimekwisha kata tiketi, na zinasubiriwa timu mbili kutoka kwenye mipambano ya usiku huu. Makala hii inaangazia mwenendo wa matokeo na ratiba kuelekea Robo Fainali.
SOMA HII PIA: AFCON 2025: Matokeo, hawa hapa wafungaji bora kabla ya Ratiba ya 16 bora, Feisal na Msuva wamo?
Bado hujashinda pesa? Cheza ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa
Ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

AFCON 2025: Ni nchi gani zimefuzu kwa robo fainali?

Baada ya hatua ya makundi isiyotabirika, ambayo ilifungua milango kwa timu 20 kupambana. Hatimaye timu 16 zilizokusanya pointi nyingi zaidi kwenye makundi yao, zilifanikiwa kutinga hatua ya mtoano (hatua ya 16 bora). Timu hizo zimepambana kusaka timu 8 ambazo zitaumana kwenye Robo Fainali.
Kufikia sasa, timu 6 zimefanikiwa kutinga hatua ya robo fainali. Kila timu imetinga Robo Fainali kwa mtindo tofauti, lakini kwa lengo lilelile la kushinda ubingwa. Senegal ilikuwa taifa la kwanza kutinga robo fainali siku ya Jumamosi. Mabingwa hao wa zamani wa Afrika, walikata tiketi ya Robo Fainali baada ya kuishinda Sudan 3-1.
Baada ya Senegal, Mali nayo ilikata tiketi ya robo fainali ilipoilaza Tunisia kwa mikwaju ya penalty baada ya dakika 90 kumalizika kwa sare ya bao 1-1. Mali katika mchezo huo walilazimika kumaliza pungufu baada ya Nyota wao mmoja kupewa kadi nyekundu.
SOMA HII ZAIDI: AFCON 2025: Matokeo na Ratiba, hizi hapa timu zilizofuzu hatua ya mtoano (16 bora)
Wenyeji Morocco chupuchupu vs Tanzania

Wenyeji wa michuano hiyo Morocco walishinda kwa tabu mbele ya Tanzania siku ya Jumapili kwa ushindi mwembamba wa bao 1-0 mjini Rabat. Wakicheza mbele ya umati wa mashabiki wao wa nyumbani wenye shauku, Morocco walionyesha subira na ukomavu, huku Brahim Díaz akifunga bao pekee.
Ushindi huo haukuweka tu matumaini ya ubingwa wa Morocco hai, lakini pia uliimarisha imani yao inayokua kwamba hatimaye huu unaweza kuwa mwaka wao. Ikumbukwe ni miaka 50 imepita baada ya ubingwa wao wa mwisho wa AFCON. Ubora wa timu yao wakati huu unawapa matumaini ya kubeba.
Cameroon nao walijiunga na orodha ya waliofuzu robo fainali baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Afrika Kusini. Mabingwa hao mara tano wa Afrika, kwa mara nyingine tena walionyesha ukomavu wao katika soka. Mchezo huo ulishuhudia upinzani mkali.
Misri iliilaza Benin 3-1 baada ya muda wa ziada huku Mohammed Salah akifunga bao la mwisho la mchezo. Nigeria pia ilijihakikishia nafasi ya kufuzu robo fainali Jumatatu usiku baada ya kuifunga Msumbiji 4-0. Victor Osimhen alifunga mabao mawili na kuisaidia Super Eagles kusonga mbele.
Nani na nani kuvaana Robo Fainali?

Cameroon wanatarajia kuvaana na Morocco katika pambano kali la robo fainali. Mechi hii inatarajia kushuhudia ushindani wa nguvu, ubora na historia. Mechi nyingine ni kama ifuatavyo;
Mali vs Senegal – Ijumaa, 9 Januari
Cameroon vs Morocco – Ijumaa, 9 Januari
Egypt v (Mshindi wa Cote d’Ivoire v Burkina Faso) – Jumamosi, 10 Januari
Nigeria v (Mshindi wa Algeria v DR Congo) – Jumamosi, 10 Januari
SOMA HII ZAIDI: AFCON 2025: Sami Trabelsi kufukuzwa kazi timu ya taifa Tunisia/ Highlights, fixtures, standings
Kuhusu Fainali ya AFCON 2025

Mashindano ya AFCON 2025 yanatarajiwa kufikia tamati rasmi siku ya Januari 18, mwaka huu. Ikumbukwe mchezo wa Fainali unatarajiwa kupigwa katika Uwanja wa Prince Moulay Abdellah mjini Rabat. Swali ni je, Cote d’Ivoire wataweza kutetea ubingwa wao, au atapatikana bingwa mpya?
Hitimisho
Kuelekea Robo Fainali ya AFCON 2025. Mechi kadhaa za kuhitimisha hatua ya 16 bora zinatarajiwa kuchezwa leo Jumanne usiku. Ratiba ya Robo Fainali inatazamwa kuwa na ushindani mkubwa kutoka na mwenendo wa mashindano na inasubiriwa kwa hamu kubwa.

