Atletico Madrid vs Real MadridAtletico Madrid vs Real Madrid
  • ‘Madrid Derby’ kinawaka leo Alhamisi usiku huko Mashariki ya Kati.
  • Ni mechi kali ya Atletico Madrid vs Real Madrid, watakaokutana katika wa mchezo wa nusu fainali ya Spanish Super Cup.
  • Mchezo huu wa kukata na shoka unatarajiwa kupigwa mjini Jeddah, Saudi Arabia katika Uwanja wa King Abdullah Sport City.

Kinawaka ‘Madrid Derby’ leo Alhamisi usiku. Ni mechi kali ya Atletico Madrid vs Real Madrid watakaokutana katika wa mchezo wa nusu fainali ya Spanish Super Cup. Mchezo huu wa kukata na shoka unatarajiwa kupigwa mjini Jeddah, Saudi Arabia katika Uwanja wa King Abdullah Sport City.

Bado hujashinda pesa? Cheza ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa

Ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

image

SOMA HII PIA: Atletico Madrid vs Real Madrid: Preview, Team News & Prediction

h2h, Atletico Madrid vs Real Madrid

Atletico Madrid vs Real Madrid (-)
Atletico Madrid vs Real Madrid

Timu hizi mahasimu wa jiji la Madrid, Spain zimekutana mara 72 katika historia ya mechi za ushindani. Real Madrid wametawala pambano hili la dabi mara nyingi zaidi, ambapo wameshinda mechi 33. Atletico wao wameshinda mechi 16 pekee, huku mechi 23 zikiisha kwa matokeo ya sare.

Fomu ya Atletico Madrid hivi karibuni katika mashindano yote

L W W W D

Fomu ya Real Madrid hivi karibuni katika mashindano yote:

L L W W W

Vikosi vinatarajiwa Atletico Madrid vs Real Madrid

Atletico

Kikosi cha Atletico (-)
Kikosi cha Atletico

Kipa: Oblak

Walinzi: Llorente, Pubill, Le Normand, Hancko

Viungo: Simeone, Gallagher, Koke, Baena

Washambuliaji: Sorloth, Alvarez

Real Madrid

Kikosi cha Real Madrid

Kipa: Courtois

Walinzi: Valverde, Huijsen, Rudiger, Carreras

Viungo: Camavinga, Tchouameni, Rodrygo, Bellingham.

Washambuliaji: Vinicius; Garcia

SOMA HII PIA: La Liga Table 2025/26

Dondoo za muhimu kuelekea mchezo huu

Atletico wanawania kushinda kombe lao la nne la Spanish Super Cup, huku Los Blancos wao wakilenga kulinyanyua kwa mara ya 14 katika historia yao adhimu.  Atletico hawajapoteza katika mechi tano zilizopita, lakini sare ya 1-1 Jumapili dhidi ya Real Sociedad kwenye Uwanja wa Reale Arena imewachanganya. Sare hiyo iliwaacha katika nafasi ya nne na pointi 11 nyuma ya vinara Barcelona.

Atletico, ambao wako kwenye michuano ya Super Cup kutokana na kumaliza katika nafasi ya tatu msimu uliopita. Wameelekea Saudi Arabia, wakiwa na matumaini ya kutwaa taji hilo kwa mara ya tatu katika historia yao. Walifanya hivyo hapo awali 1985 na 2014.

Licha ya historia hiyo Atletico wanaingia katika mchezo huo wakiwa na jeuri. Hii ni kufuatia kumbukumbu ya ushindi wa 5-2 dhidi ya Real Madrid, kwenye Uwanja wa Metropolitano mwezi Septemba. Hii ilikuwa mara ya kwanza kufanya hivyo baada ya kupita miaka 75.

Alonso presha imeshuka

Alonso
Alonso

Kocha wa Real Madrid Xabi Alonso amepunguza presha kubwa ambayo ilikuwa kwenye mabega yake kwa kushinda mara nne mfululizo. Miongoni mwa ushindi alioupata ni ule wa mabao 5-1 kwenye pambano la nyumbani Jumapili dhidi ya Real Betis. Ushindi huu waliupata licha ya kuendelea kukosa huduma ya staa wao, Kylian Mbappe aliye majeruhi.

Mshambuliaji, Gonzalo Garcia aliziba vizuri nafasi ya Mbappe. Hii ni baada ya kufunga mabao matatu (hat-trick) kamili akifunga mabao hayo kwa mguu wake wa kulia, mguu wa kushoto na Kichwa. Garcia anakuwa mchezaji mwenye umri mdogo zaidi kufunga hat-trick kamili ya La Liga katika karne ya 21 akiwa na umri wa miaka 21 na siku 286.

SOMA HII ZAIDI: Real Madrid vs Celta Vigo: Live Score, h2h, lineups, utabiri

Habari za majeruhi wa kila timu

Mbappe
Mbappe

Atletico Madrid wanatarajia kuwakosa, Clement Lenglet na Nicolas Gonzalez, ambao watasalia Uhispania kuendelea na matibabu yao ya majeraha ya goti na nyama za paja mtawalia. Kiungo, Pablo Barrios huenda pia akakosekana, baada ya kushindwa kumaliza mchezo wa Jumapili. Conor Gallagher, anaweza kupewa nafasi ya kuanza pamoja na Koke katika safu ya kati, ingawa Cardoso ni chaguo jingine kwa Simeone.

Kwa upande wa Real Madrid, Mbappe amesalia mjini Madrid kuendelea kupata nafuu kutokana na jeraha la goti lililomfanya akose ushindi dhidi ya Betis. Eder Militao pia ameachwa nje ya timu iliyosafiri kutokana na tatizo la misuli ya paja. Brahim Diaz staa wa kimataifa wa Morocco naye amesalia kwenye Kombe la Mataifa ya Afrika AFCON 2025.

Hitimisho

Atletico Madrid vs Real Madrid unatarajiwa kuwa mchezo mgumu sana. Hii ni kutokana na historia ya upinzani, mbinu na mapungufu ya kila kikosi. Licha ya muono huo wafanya tathimini wengi, wanaipa Real Madrid nafasi kubwa ya kushinda. Dakika 90 zinatarajia kutoa majibu ya kweli.

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.