Simba SC ina mgogoro mzito kwa sasa?Magori Simba SC
  • Mo Dewji muwekezaji wa Simba SC na Murtanza Mangungu ukweli wa sakata lao huu hapa
  • Simba SC ina mgogoro mzito kwa sasa? Kila kitu kimewekwa hadharani.
  • Zijue sababu za timu hiyo kuyumba, CAF Champions League hesabu ndefu zinapigwa

Simba SC ina mgogoro mzito kwa sasa? Hilo limekuwa ni swali linalosubiri majibu kutokana na timu hiyo kutopata matokeo mazuri. Uongozi wa timu hiyo umeweka wazi yote yaliyosababisha kuwa kwenye mwendo mbovu. Baada ya kuachana na Dimitar Pantev mchezo uliopita ilipoteza kwa kufungwa magoli 2-0 dhidi ya Azam FC.

SOMA HII: Matokeo ya Simba SC 2025/26 | Ratiba, vinara wa ufungaji

Muda wakupaisha kindege na kuvuna mamilioni ni sasa hivi

Rubani makini hakosi kuvuna mamilioni. Yote haya yanakusubiri wewe, paisha Kindege cha SportPesa uvune mamilioni sasa hivi. Ni rahisi sana cheza aviator ushindi unakusubiri.

image

Simba SC ina mgogoro mzito kwa sasa? Haya hapa majibu

Simba SC ina mgogoro mzito kwa sasa?
Magori, Mtendaji wa Bodi ya Simba SC. Source: Simba SC.

Je ni kweli Simba SC ina mgogoro mzito kwa sasa? Hatimaye zile tetesi zimepata majibu. Hiyo ni kupitia mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika leo Desemba 19,2025. Mwenyekiti wa Bodi, Crescentius Magori amesema kuwa timu ipo imara.

“Kikao chetu cha mwisho tulipitisha katiba ambayo kama sio leo au kesho itasajiliwa. Hili ni jambo kubwa kwa Simba, miaka nane ilikuwa kupanda na kushuka lakini sasa tunaingia makubaliano ya kujua mwekezaji atafanya nini na wanachama watafanya nini. Kubwa tulikuwa tumesimamisha kutoa kadi na sasa tunaenda kuanza kutoa kadi. Nawahakikishia tunaenda kuwa klabu ya kwanza yenye wanachama wengi sio ndani tu ya Tanzania hata nje.

Mchakato wa mabadiliko Simba SC

“Wapenzi wa Simba sasa tunakwenda kufanya mambo makubwa. Lakini la pili tunakwenda kutengeneza kadi za kisasa ambazo hapa Tanzania hakuna mfano wake, itakuwa kadi yenye matumizi mengi kwa mwanachama. Lakini mabadiliko yakikamilika mwekezaji sasa anakwenda kujenga miundombinu. Muda si mrefu pale Bunju panakwenda kujengwa uwanja wa mazoezi wenye nyota tano.

“Kwanza tunatoa shukrani kwa watu ambao wameifanya Simba kupiga hatua kubwa. Tunatoa shukrani kwa wanachama, mashabiki na wote wanaoiombea vizuri Simba. Tunatoa shukrani kwa partners wote na bila kusahau Serikali lakini pamoja na yote shukrani za kipekee zimwendee Mwenyezi Mungu.

“Napenda kuwambia kwamba mchakato wa mabadiliko ambao ulianza 2017 sasa unakwenda kufikia tamati. Ni kipindi kigumu tumepita ukiacha Ujerumani hakuna sehemu nyingine unatumika hivyo tumeona changamoto ilivyokuwa namna ya kuupitisha. Unaitwa Hybrid. Kusema kwa uwazi ni miaka nane ambayo ilikuwa na changamoto sana.

“Sisi tuna bahati tumepata mwekezaji ambaye ni mwanachama wa Simba na hata akiteua bodi anateua Wanasimba kwahiyo hayo maneno yanayokuja tutayamaliza. Sisi tuko kitu kimoja.

“Lugha za kutugawanya sasa zifike mwisho. Lakini kikubwa tunaandaa mfumo wa utoaji wa kadi ambao utakuwa ni wa kisasa. Sisi ni klabu ambayo itakuwa na pesa nyingi kuliko klabu yoyote. Tunakwenda kutengeneza klabu yenye uongozi bora.

SOMA HII: Simba SC kufanya usajili mkubwa | Maeneo yatakayoboreshwa | Mo atoa tamko zito | Ahmed atamba

image

Hii hapa sababu ya Simba SC kuyumba

Simba SC kuwakosa wachezaji muhimu watatu wakiikabili Petro de Luanda CAF Champions League
Camara, kipa namba moja wa Simba SC. Source: Simba SC.

“Kiufundi timu iliyumba sababu kocha aliyeanza msimu na timu aliondoka, akaja kocha hatukukubaliana. Kitu kingine ambacho watu hawakisemi ni mechi ya ngao beki muhimu wa kati ameumia, mechi inayofuata kipa namba moja ameumia. Tukiwa Mali beki muhimu mwingine wa kati ameumia. Lakini maneno yanakuzwa. Tumecheza mechi tano za ligi na kupoteza mechi moja, kelele kama mwisho wa dunia.
“Tusipoingia robo fainali ya Ligi ya mabingwa ni jambo baya hatukusudia lakini mwaka jana kuna timu haikuingia robo mlipiga kelele? Tuongee mpira, Wanasimba msitolewe kwenye reli. Ooh Morice anaingia sijui timu gani Januari lakini hizo kelele zinatengenezwa lakini sisi bodi tuko imara kwelikweli,”.

SOMA HII: Kocha mpya Simba SC CV yake hii hapa | Ratiba ya mechi zijazo CAF Champion League

image

Mangungu na Mo kuna mtafaruku?

Mangungu
Mangungu, Mwenyekiti wa Simba SC. Source: Simba SC.

Makamu Mwenyekiti wa Bodi na Mwenyekiti wa Klabu, Murtaza Mangungu amebainisha kuhusu mawasiliano yake na Mo. Mangungu ameweka wazi kuwa wanaongea na kiongozi huyo mara kwa mara.

“Wanasema kuna mgogoro kati ya upande wa klabu na mwekezaji, mimi na mwenyekiti wa bodi tunaongea kila mara, kama ni Mo mimi mara ya mwisho niliongea nae jana saa 8. Sisi hatuna jambo la siri, timu inafanya mipango yake kama kuna taarifa ya kutoka inatoka,”.

Hitimisho

Simba SC ina mgogoro mzito kwa sasa? Mwendo wake uwanjani ulizua maswali mengi jambo ambalo kwa sasa lipo wazi. Timu hiyo imeweka wazi itafanya mageuzi makubwa kwenye eneo la uwekezaji. Je hayo yatatimia lini? Endelea kusoma SportPesa blog tutakujuza kila hatua.

Share this: