Simba SC 0-2 Azam FC ni matokeo yaliyovunja rekodi laSeleman Matola
  • Simba SC 0-2 Azam FC ni matokeo yaliyovunja rekodi kwa timu hiyo kucheza mechi za ligi bila kuangusha pointi.
  • CAF Champions League hatua ya makundi mechi zote mbili wamepoteza hatua ya makundi.
  • Ratiba na matokeo kwa mechi za Simba SC 2025/26 tumekusogezea hapa katika anga la kitaifa NBC Premier League na CAF.

Simba SC 0-2 Azam FC ni matokeo yaliyovunja rekodi ya kucheza bila kufungwa. Kwenye mechi 4 zilizopita kwenye ligi timu hiyo ilipata ushindi asilimia 100. Ikiwa nyumbani rekodi hiyo ikavunjwa kwa matajiri wa Dar.

SOMA HII:Dimitar Pantev kibarua kimeota nyasi Simba SC/ CAF Champions League matokeo, mrithi wake

Vuna mamilioni sasa hivi

Kuna jambo umekwama kwa sasa kuhusu mkwanja? Usiogope, rubani ni jasiri na kazi yake ni kupaisha kindege cha SportPesa. Cheza sasa hivi Aviator uvune mamilioni bofya hapa chini, muda ni wako na nafasi ya ushindi inakusubiri.

image

 Simba SC 0-2 Azam FC ni matokeo yaliyovunja rekodi, matokeo mengine

Simba SC 0-2 Azam FC ni matokeo yaliyovunja rekodi
Joshua Mutale kwenye mchezo dhidi ya Azam FC. Source: Simba SC.

Wakati Simba SC 0-2 Azam FC ni matokeo yaliyovunja rekodi hapa tunakusogezea mengine. Kwenye mechi zote ambazo mnyama alipoteza msimu wa 2025/26 alikuwa nyumbani. Kimataifa hajapata ushindi mechi za nyumbani akiwa hatua ya makundi.

Matokeo ya mechi zilizopita Simba SC

Oktoba Mosi 2025, Simba SC 3-0 Namungo FC, mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Septemba 28 2025, Simba SC 1-1 Gaborone United, Ligi ya Mabingwa Afrika.

Septemba 25 2025, Simba SC 3-0 Fountain Gate mchezo wa Ligi Kuu Bara.

Septemba 20 2025, Gaborone United 0-1 Simba SC, Ligi ya Mabingwa Afrika.

Septemba 16 2025, Yanga SC 1-0 Simba SC, Ngao ya Jamii.

Septemba 10 2025, Simba SC 2-0 Gor Mahia mchezo wa kimataifa wa kirafiki.

Nsingizini Hotspurs 0-3 Simba SC, Oktoba 19 2025, CAF Champions League.

Simba SC 0-0 Nsingizini Hotspurs, Oktoba 24,2025, CAF Champions League.

JKT Tanzania 1-2 Simba SC, Novemba 8 2025, Uwanja wa Meja Jeneral Isamuhyo, NBC Premier League.

Simba SC 0-1 Petro de Luanda, CAF Champions League.

Stade de Malien 2-1 Simba SC, CAF Champions League, Novemba 30,2025.

Simba SC 3-0 Mbeya City, Ligi Kuu Bara, Desemba 4,2025.

Simba SC 0-2 Azam FC, Desemba 7,2025.

SOMA HII: Nsingizini Hotspurs 0-3 Simba SC | CAF Champions League | Highlights | Magoli yote |  

image

Mechi zijazo kwa Simba SC

Simba vs Azam
Ellie Mpanzu kwenye mchezo dhidi ya Azam FC. Source: Simba SC.

Es Tunis vs Simba SC, CAF Champions League, Januari 23,2026.

Simba SC vs Mtibwa Sugar, Januari 29,2025.

Simba SC vs ES Tunis, Januari 30,2025, CAF Champions League.

Simba SC vs Singida Black Stars, Februari Mosi,2025.

KMC vs Simba SC, Februari 6,2025 unatarajiwa kuchezwa.

Nafasi ya Simba SC

Matokeo ya CAF Champions League 2025/26
Nahodha wa Simba SC, Shomari Kapombe na Ellie Mpanzu baada ya mchezo. Source: Simba SC.

Katika mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara ya NBC baada ya mechi 5 imepoteza mchezo mmoja. Imekusanya jumla ya pointi 12 ikiwa nafasi ya 5 kwenye msimamo. Mchezo wa kwanza kupoteza ilikuwa dhidi ya Azam FC, Uwanja wa Mkapa.

Idadi ya magoli ambayo imefunga ni 11. Kipa namba moja ni Moussa Camara ambaye alipata maumivu mchezo dhidi ya Gaborone United. Kipa namba mbili ni Yakoub Suleman ambaye anakaa langoni kwenye mechi wakati huu.

Katika anga la kimataifa, Simba SC baada ya kucheza mechi mbili hatua ya makundi imepoteza zote. Ilikuwa dhidi ya Petro de Luanda na Stade Malien ya Mali. Kwenye msimamo inaburuza mkia.

SOMA HII: JKT Tanzania 1-2 Simba SC NBC Premier League 2025/26/ Highlights, goal

image

Hitimisho

Simba SC 0-2 Azam FC ni matokeo yaliyovunja rekodi kwa msimu mpya ndani ya ligi. Seleman Matola alikuwa benchi baada ya Dimitar Pantev kuvunjiwa mkataba. Kwa sasa timu hiyo imecheza michezo 5 ikipoteza mchezo mmoja katika Mzizima Dabi, Uwanja wa Mkapa.

Share this: