Kapten KapombeKapten Kapombe
  • Beki Rushine amefungua akaunti ya magoli kwenye mchezo wa kwanza Ligi Kuu ya NBC Uwanja wa Mkapa.
  • Simba SC 3-0 Fountain Gate FC Septemba 25 2025, jasho liliwavuja wachezaji katika kutafuta ushindi.
  • Jean Ahoua atwaa tuzo ya mchezaji bora wa mchezo na kutoa ahadi nzito kwa mashabiki wa msimbazi.

Simba SC 3-0 Fountain Gate FC dakika 90 za jasho kwenye kutafuta ushindi. Mbinu za Seleman Matola zilimzidi ujanja Kocha Mkuu wa Fountain Gate FC, Dennis Kitambi. Mchezo huo ulichezwa Uwanja wa Mkapa Septemba 25 2025.

Paisha Kindege cha SportPesa uvune mamilioni

image

Muda wa kuvuna mamilioni ni sasa hasa ukipaisha Kindege cha SportPesa. Kuna fedha ambazo zinakusubiri rubani wikiendi hii. Rahisi sana cheza Aviator upate mgao wako.

Simba SC 3-0 Fountain Gate FC wafungaji wa magoli

Simba SC 3-0 Fountain Gate FC
Jean Ahoua na Jonathan Sowah wachezaji wa Simba SC walifunga dhidi ya Fountain Gate FC. Source: Simba SC.

Soma hii: Kocha mpya Simba SC Hemed Morocco hana presha

Magoli ya Simba SC yamefungwa na Rushine dakika ya 5. Hiyo ilikuwa ni baada ya Simba SC kupata kona na mpigaji alikuwa ni Jean Ahoua. Goli la pili lilifungwa na Ahoua dakika ya 36 kwa pasi ya Yusuph Kagoma.

Soma hii: Simba SC vs Fountain Gate FC Ligi Kuu NBC ‘Live’: Vikosi, H2H, utabiri, Highlights

Kipindi cha pili Simba SC walifunga goli moja pekee. Mfungaji ni Jonathan Sowah ilikuwa dakika ya 57. Mshambuliaji huyo mpya wa Simba SC alitumia pasi ya Ellie Mpanzu.

Tuzo ya mchezaji bora wa mchezo

Baada ya dakika 90 kukamilika kiungo mshambuliaji wa Simba SC Jean Ahoua alichaguliwa kuwa mchezaji bora. Ahoua alihusika katika mabao mawili kwenye mchezo. Alitoa pasi ya goli kwa Rushine na alifunga goli moja.

Ahoua amesema kuwa ni mwanzo mzuri kwa Simba SC. Huku akiongeza kuwa wataendelea kufanya vizuri kwenye mechi zinazofuata. Mchezo ujao kwa timu hiyo itakuwa dhidi ya Gaborone United Ligi ya Mabingwa Afrika.

“Ni furaha kuona tunapata ushindi kwenye mchezo wetu wa ufunguzi. Kupata tuzo ni kitu kizuri pia. Kikubwa ni kuendelea kupambana kwa mechi zijazo ili kupata matokeo mazuri.” amesema Ahoua.

Hakuna kadi dakika 90

Katika mchezo wa Simba SC 3-0 Fountain Gate FC zilikamilika dakika 90 bila mwamuzi kuonesha kadi. Hii ilitokana na nidhamu kwa wachezaji. Licha ya kucheza faulo zilikuwa hazina hatari kwa wachezaji wa pande zote mbili.

Wachezaji waliofanyiwa mabadiliko

Simba vs Fountain Gate
Simba vs Fountain Gate, Uwanja wa Mkapa. Source: Simba SC.

Kipindi cha pili Simba SC walifanya mabadiliko dakika ya 45. Kibu Dennis alimpisha Morice Abraham na Mzamiru alimpisha Kante. Fountain Gate walikuwa na wachezaji wawili pekee benchi. Hassan Ally alitoka dakika ya 60 akimpisha Anack Mtambi.

Kikosi cha Simba SC dhidi ya Fountain Gate


Mousa Camara, Shomari Kapombe, Naby Camara, Chamou, De Reuck, Yusuph Kagoma, Kibu Dennis, Mzamiru Yassin, Sowah, Jean Ahoua, Ellie Mpanzu.

Wachezaji wa akiba Simba SC


Yakoub Suleiman, Duchu, Anthony Mligo, Nangu, Kante, Morice Abraham, Steven Mukwala, Maema, Joshua Mutale na Seleman Mwalimu.

Kikosi cha Fountain Gate

Fadhil Kisunga, Daniel Jolam, Elie Mokono, Abdallah Kulandana, Lamela Maneno, Sadick Ramadhani, Jackson Kataga, Shaaban Pandu, Mudrick Abdi, Shomari Musa na Hassan Ally.

Wachezaji wa akiba

Anack Mtambi na Hassan Juma.

Jean Ahoua mtambo wa pasi za mwisho Simba SC

Simba SC 3-0 Fountain Gate FC
Jean Ahoua kiungo mshambuliaji wa Simba SC 2025/26. Source: Simba SC.

Jean Ahoua ni mtambo wa pasi za mwisho ndani ya kikosi cha Simba SC. Rekodi zinaonesha kuwa kwenye mechi za mwanzo katika Ligi Kuu Bara kuanzia msimu wa 2024/25 alikuwa ni mchezaji wa kwanza kutoa pasi. Ikumbukwe kwamba msimu wa 2024/25 alitoa jumla ya pasi 9 na alifunga magoli 16.


Soma hii: Kocha mpya Simba SC Hemed Morocco hana presha
Msimu wa 2024/25 kiungo huyo alitoa pasi ya bao kwa Che Malone. Hiyo ilikuwa kwenye mchezo dhidi ya Tabora United. Uwanja wa KMC Complex. Msimu wa 2025/26 ametoa pasi ya bao kwa Rushine ilikuwa katika mchezo dhidi ya Fountain Gate. Mechi zote za ufunguzi Simba SC ilishinda mabao 3-0.

Hitimisho

Simba SC 3-0 Fountain Gate ni mwanzo wa msimu mpya wa 2025/26. Mchezo ujao kwa Simba SC kwenye ligi itakuwa dhidi ya Namungo FC, Uwanja wa Mkapa. Fountain Gate watakutana na Mtibwa Sugar katika mchezo ujao wa ligi ya NBC.

image

Share this: