- Kouma afungua akaunti ya mabao akiwa na uzi wa timu mpya msimu wa 2025/26 kwa pigo la kichwa cha maajabu ndani ya 18.
- Yanga SC 3-0 Pamba Jiji FC mabingwa waanza kwa kishindo wakiwa nyumbani chini ya Kocha Mkuu Romain Folz.
- Maxi Nzengeli achaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo mbele ya Pamba Jiji FC iliyopoteza pointi ugenini.
Yanga SC 3-0 Pamba Jiji FC mabingwa waanza kwa kishindo katika mchezo wa kwanza. Dakika 90 za jasho zilichezwa Uwanja wa Mkapa Septemba 24 2025. Kiungo Maxi Nzengeli amechaguliwa kuwa mchezaji bora baada ya kuvuja jasho kutimiza majukumu yake.
Paisha Kindege cha SportPesa uvune mamilioni
Muda ni sasa kuvuna mamilioni ambayo yanakusubiri. Rahisi sana paisha kindege cha SportPesa uvune mamilioni. Cheza Aviator sasa upate mgao wako wa mamilioni.

Yanga SC 3-0 Pamba Jiji FC mabingwa waanza kwa kishindo
Katika mchezo wa kwanza Yanga SC 3-0 Pamba Jiji FC mabingwa waanza kwa kishindo kwenye mchezo wa kwanza. Ipo wazi msimu walikuwa nyumbani wakifungua pazia la ligi iliyoanza Septemba 17 2025. Ushindi huo unafungua safari kuanza kuukimbizia ubingwa.

Pamba Jiji FC walianza kwa kasi katika dakika 45 za mwanzo. Jitihada zao kuwazuia Yanga SC zilikuwa imara mwanzo mwisho. Kipa Mohamed Kamara wa Pamba Jiji FC alifanya kazi kubwa kuokoa hatari za Lassine Kouma na Edmund John.
Magoli ya Yanga SC 3-0 Pamba Jiji FC

Lassine Kouma alifungua akaunti ya magoli kwa kupachika la uongozi dakika ya 45 akitumia pasi ya Edmund John. Goli la pili ni Maxi Nzengeli alifunga dakika ya 63 akitumia pasi ya Mohamed Hussen Zimbwe Jr. Chuma cha tatu kilipachikwa na Mudathir Yahya dakika ya 90 akitumia pasi maelekezo ya Pacome.
Kikosi cha Yanga SC vs Pamba Jiji FC
Djigui Diarra, Israel Mwenda, Zimbwe Jr, Bakari Mwamnyeto, Dickson Job, Balla Conte, Maxi Nzengeli, Kouma, Boyeli, Edmund John na Ecua.
Wachezaji wa akiba Mshery, Boka, Andambilwe, Aboubakari, Abdulnasir, Chikola, Doumbia, Pacome, Dube.
Kikosi cha Pamba Jiji FC vs Yanga SC

Soma hii: Yanga SC vs Pamba Jiji FC Septemba 24 2025 Uwanja wa Mkapa
Mohamed Kamara, Ibrahim Ibrahim, Brian Eshanda, Najim Mussa, Abdoulaye Yonta, Kenneth Kunambi, Hassan Kibailo, Shaphan Siwa, James Mwashinga, Kelvin Nashon, Abdallah Kheri.
Wachezaji wa akiba
Abdulmajid Mangalo, Michael Samamba, Saleh Masoud, Shashiri Nahimana, Samuel Anthwi, John Ben, Khalid Chambela, Dennis Richard, Emmanuel Charles, Henry Msabila.
Wachezaji waliofanyiwa mabadiliko
Balla Conte alitoka dakika ya 55 nafasi yake ilichukuliwa na Aziz Andambwile, Celstin Ecua dakika ya 55 nafasi yake ilichukuliwa na Doumbia. Pacome aliingia dakika ya 70 akichukua nafasi ya Edmund John na Prince Dube aliingia dakika ya 70 akichukua nafasi ya Boyel.
Soma hii: Rekodi zinaibeba Yanga SC mbele ya Pamba Jiji FC
Dakika ya 63 Mudathir Yahya aliingia akichukua nafasi ya Kouma hiyo ilikuwa ni kwa upande wa Yanga SC. Miongoni mwa wachezaji ambao walifanyiwa mabadiliko kwa Pamba Jiji FC ilikuwa ni Kibailo dakika ya 65 alimpisha Kibigwe, Najim Mussa dakika ya 45 alitoka alimpisha Kelvin Sabato.
Kadi za njano
Mchezaji wa kwanza kuonyesha kadi y anjano katika mchezo hu oni beki wa Pamba Jiji FC, Abdalah Kheri dakika ya 37. Kwa upande wa Yanga SC ni Kouma alionyesha kadi ya njano dakika ya 46 baada ya kumchezea faulo nyota wa Pamba Jiji.
Hitimisho
Yanga SC 3-0 Pamba Jiji FC mabingwa waanza kwa kishindo ukiwa ni mchezo wa ufunguzi. Mashabiki walijitokeza kushuhudia burudani ndani ya uwanja. Mchezo ujao kwa Wanajangwani itakuwa kimataifa dhidi ya Wiliete FC Ligi ya Mabingwa Afrika.


