Yanga SC vs Wiliete SCYanga SC vs Wiliete SC
  • Mashindano ya kimataifa yaliyochini ya Shirikisho Africa (CAF), yanatarajiwa kuanza rasmi wikiendi hii.
  • Tayari wawakilishi wa Tanzania ambao wanaanzia ugenini wameshasafiri.
  • Wiliete SC vs Young Africans Africans SC huko Angola, ni miongoni mwa michezo inayosubiriwa kwa hamu Tanzania.

Safari ya kuisaka hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika inaendelea wikiendi hii. Kwa upande wa Tanzania Yanga SC na Simba SC zitashuka uwanjani wikiendi hii. Wananchi, baada ya ushindi muhimu ugenini watarudiana tena katika mechi ya mkondo wa pili ya Young Africans SC vs Wiliete SC itakayopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Cheza na ushinde sasa na ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni muda huu

Hujashinda na kindege cha SportPesa? Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kubashiri SportPesa bonyeza picha hii chini

image

H2H kati ya Yanga SC vs Wiliete SC

Timu hizi zimekutana mara moja katika historia katika mashindano rasmi ambapo Yanga SC ilifanikiwa kushinda 3-0. Matokeo hayo Yanga SC waliyapata katika mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa Ijumaa iliyopita ya Septemba 19, 2025. Hivyo mchezo huu unatarajiwa kuwa wa pili kwa timu hizi kukutana.

SOMA HII ZAIDI: Wiliete SC vs Young Africans SC CAFCL: ‘LIVE’, vikosi, H2H, Utabiri, Yanga Yatua Angola kibabe

Michezo mitano iliyopita ya Yanga SC

Matokeo yaliyopita
Matokeo yaliyopita

19 Sep 2025 Wiliete 0-3 Young Africans

25 Jun 2025 Young Africans 2-0 Simba SC

22 Jun Young Africans 5-0 Dodoma Jiji FC

18 Jun Tanzania Prisons 0-5 Young Africans

13 May Young Africans 3-0 Namungo FC

Michezo mitano iliyopita ya Wiliete SC

24 Sep 1º de Maio 0-1 Wiliete

19 Sep Wiliete 0-3 Young Africans

25 May Wiliete 1-2 Sagrada Esperança

18 May 1º de Agosto 0-0 Wiliete

11 May Wiliete 2-1 Académica do Lobit

Utabiri

Kutokana na matokeo hayo na namna ambayo Yanga SC walicheza mchezo wa kwanza, Wananchi wanapewa nafasi kubwa ya kuibuka na ushindi. Ikumbukwe mchezo wa kwanza Yanga SC walishinda mabao 3-0 ugenini. Faida kubwa ya kucheza nyumbani inatarajiwa kuwabeba katika mchezo wa kesho.

SOMA HII PIA: Yanga SC watachuana na vijana wa Angola Wiliete SC kwenye CAF Champions League 2025

Kikosi cha Yanga SC kinachotarajiwa kucheza dhidi ya Wiliete SC

Kikosi cha Yanga
Kikosi cha Yanga

Kipa:

Diarra

Walinzi:

Israel, Zimbwe, Job, Baka

Viungo:

Kouma, Andabwile, Maxi

Washambuliaji:

Ecua, Pacome, Boyeli

Taarifa mpya za Yanga SC

Young Africans SC vs Wiliete SC
Jezi mpya Yanga SC

Kuelekea mchezo huu, Yanga SC wamefanya uzinduzi wa jezi zao mpya. Uongozi wa Yanga wameutaja uzinduzi huo kama sehemu ya vita dhidi ya walanguzi wa jezi feki. Jezi hizo mpya zina chapa mpya ya Kampuni ya NIA.

Akizungumzia jezi hizo Ofisa Habari wa Yanga, Ali Kamwe amesema: “Vita ya jezi feki ni vita ngumu, sio vita rahisi. Mzigo wetu wa msimu huu tulioleta umeisha, lakini cha ajabu bado tunapewa taarifa kuwa mizigo mikubwa bado inaendelea kuingia nchini ya jezi ambayo sio ya Mdhamini wetu GSM.

“Tumekuja na mpango tofauti wa kupambana na JEZI feki sana na ninaamini itakomesha hii tabia ya jezi feki. Tunazindua leo jezi toleo la pili ambayo tofauti ni mzalishaji mpya wa jezi na kitambaa pia kipo tofauti. Tumekuwa tukiwanufaisha watu kwa kuuza jezi feki ambazo washabiki wetu huwa ni ngumu kutofautisha Kati ya jezi feki na original.

“Tunaamini kwa toleo hili itakuwa ni solution kubwa sana kwa tatizo hili ambalo limekuwa sugu. Klabu haiwezi kuendelea kupoteza mapato, hii vita safari hii tumedhamiria kupambana nayo kwa akili kubwa. Niwapongeze Viongozi kwa kuja na suluhisho hili ambalo ili kusapoti ni kununua jezi hizi mpya kwa wingi na kesho tuzivae pale kwa Mkapa.”

SOMA HII ZAIDI: Rekodi zinaibeba Yanga SC mbele ya Pamba Jiji FC Septemba 24 | Presha hakuna,mabingwa kazini

Taarifa mpya za Wiliete SC

Wiliete vs Yanga
Wiliete

Kikosi cha Wiliete SC kimewasili jana Alhamisi majira saa 10 jioni. Mara baada ya kuwasili Wiliete wametamba kuwa wako tayari kwa mchezo wa hapo kesho, majira ya saa 11 katika uwanja wa Mkapa. Wapinzani hao wa Yanga SC walishinda mechi yao ya ligi iliyopita hivyo wanatarajia kutoa ushindani mkubwa.

Hitimisho

Licha ya ushindi wa mabao 3-0, Yanga SC hawapaswi kubweteka na kudhani wamemaliza mechi. Ushindi wa Wiliete kwenye mchezo uliopita inatoa taswira ya timu iliyo tayari kutoa ushindani. Hivyo mechi ya Yanga SC vs Wiliete SC inatarajiwa kuwa ya ushindani mkubwa.

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.