Hemed SulemanHemed Suleman
  • Simba SC vs Gaborone mchezo wa kimataifa unaotarajiwa kuwa wa maamuzi kwenye mashindano ya CAF
  • Kocha mpya Simba SC Hemed Morocco hana presha kuelekea kwenye mechi za kimataifa akiwa kwenye majukumu mapya.
  • Fadlu Davids bado ataishi kwenye mioyo ya Wanasimba kutokana na kazi yake aliyofanya.

Kocha mpya Simba SC Hemed Morocco hana presha kutokana na uzoefu alionao. Morocco ametambulishwa kuwa kocha wa muda ndani ya timu hiyo baada ya Fadlu Davids kusitisha mkataba wake Septemba 22 2025. Mchezo wake wa kwanza unatarajiwa kuwa dhidi ya Gaborone United katika Ligi ya Mabingwa Afrika.

Paisha Kindege cha SportPesa uvune mamilioni sasa hivi

image

Ni muda wa kupaisha Kindege cha SportPesa uvune mamilioni yako. Rahisi sana na inawezekana bila matatizo. Cheza Aviator sasa upate mgao wako.

Kocha mpya Simba SC Hemed Morocco hana presha

Kocha mpya Simba SC Hemed Morocco hana presha
Hemed Morocco Kocha Mkuu wa Simba SC kwenye majukumu mapya. Source: Simba SC.

Soma hii: Simba SC 1-0 Gaborone United CAF Champion League 2025

Baada ya kutambulishwa kocha huyo anatarajiwa kuanza kazi mapema. Kocha mpya Simba SC Hemed Morroco hana presha katika mechi ambazo ataziongoza. Septemba 28 2025 mbinu zake zinatarajiwa kutumika kwenye mchezo wa kimataifa dhidi ya Gaborone United.

Kocha huyo amebainisha kwamba hakutarajia kama jambo hilo litatokea. Kwa kuwa limetokea kwake ni fursa ataifanyia kazi. Ameongeza kuwa mchakato wakufanya vizuri utajenga picha kubwa kwa wazawa kuendelea kuaminika.

“Hakuna presha kwangu nimeshakuwa mzoefu kwenye mechi za kimataifa kwa muda mrefu. Nina amini kwamba tukishirikiana tutapata matokeo mazuri. Inawezekana na nina amini itakuwa hivyo.

Hemed Morocco
Hemed Morocco, Kocha Mkuu wa Simba SC kwa muda 2025/25.

“Nafikiri ni nafasi ambayo imetokea, haikuwa kitu rahisi. Nilipopata taarifa hii sikuona kitu rahisi kwa kuwa sikutarajia. Unajua baada ya kupata simu nilishtuka si kitu ambacho nilikuwa nategemea.

 “Watu wameona ninaweza kuwasaidia nami ninakwenda kuwasaidia. Mtu yoyote ambaye atahitaji nimsaidie nitamsaidia kuna kitu atakuwa ameona.

“Wanasimba wanahitaji mafanikio na naona kwamba kwa kuwa wamenichagua basi nitakwenda kufanya vizuri. Mimi ninaona kwamba kuna kitu ambacho kinaendelea kwa kuwa wazawa tunapewa nafasi basi nitakwenda kufanya kazi kubwa kwa ajili ya kuhakikisha kwamba wazawa wanaendelea kuaminika,”.

Mchezo wa kwanza kwa kocha mpya Simba SC kimataifa

Kocha Morocco mchezo wake wa kwanza unatarajiwa kuwa mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika. Simba vs Gaborone United, Septemba 28 2025 Uwanja wa Mkapa. Huu utatoa maamuzi mshindi kutinga hatua ya pili katika mashindano ya CAF.

Katika mchezo wa kwanza ugenini Simba SC ilipata ushindi. Kazi kubwa itakuwa kwa wachezaji kulinda ushindi ili kusonga mbele. Matokeo yanayohitajika ni ushindi kwa Simba SC ama kutofungwa kujihakikishia nafasi kusonga mbele kimataifa.

Soma hii: Kocha Fadlu Davis kuondoka Simba SC? Utata waibuka! Simba watoa tamko hili

Tayari ameanza kazi akishirikiana na kocha msaidizi Suleman Matola. Septemba 23 2025 amewasili kambini na kuanza kuwafundisha wachezaji. Timu hiyo inafanya maandalizi ya mwisho kuelekea mchezo wa ligi dhidi ya Fountain Gate Septemba 25 2025, Uwanja wa Mkapa.

Mchezo wa mwisho kwa Fadlu Davids Simba SC

Davids Fadlu (-)
Fadlu Davids aliyekuwa kocha wa Simba SC 2024/25. Source: Simba SC.

Fadlu Davids amewaaga mashabiki wa Simba SC Septemba 22 2025. Amebainisha kuwa licha ya kwamba hatakuwa ndani ya timu hiyo bado moyo wake utawakumbuka mashabiki na viongozi. Maisha yake mapya yanakwenda kuwa ndani ya Raja Casablanca ya Morocco.

Mchezo wake wa mwisho kimataifa ilikuwa dhidi ya Gaborone United. Septemba 20 2025 wakiwa ugenini nchini Botswana. Baada ya dakika 90 ubao ulisoma Gaborone United 0-1 Simba SC. Goli la ushindi lilifungwa na Ellie Mpanzu.

Soma hii: Fadlu Davids ameondoka Simba SC

Katika ardhi ya Tanzania mchezo wake wa mwisho ilikuwa Septemba 16 2025. Ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Yanga SC 1-0 Simba SC, fainali Ngao ya Jamii. Goli la ushindi kwa Wanajangwani, Kariakoo Dabi lilifungwa na Pacome Zouzoua.

Hitimisho

Kocha mpya Simba SC Hemed Morocco hana presha kuanza majukumu mapya. Anajiunga na wekundu wa msimbazi akiwa na majukumu ya timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars. Mbinu zake ziliifikisha Tanzania katika hatua ya robo fainali CHAN 2024.

image
Share this: