- Simba SC watakabiliana na Fountain Gate FC kweye mchuano wao wa kwanza wa Ligi Kuu ya NBC 2025/26.
- Mchezo huu mkali wa Simba SC vs Fountain Gate FC utachezwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa Septemba 25, 2025.
- Baada ya kupata pigo kubwa la kumpoteza kocha, Fadlu Davis hatimaye Simba imemtangaza Hemed Suleiman ‘Morocco’ kuongoza jahazi.
Hatimaye Pazia la mechi za Ligi Kuu ya NBC 2025/26 kwa Simba SC litafunguliwa rasmi kesho Alhamisi Septemba 25, 2025. Hii ni kupitia mchezo mkali wa Simba SC vs Fountain Gate FC, mchezo huu mkali utapigwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa. Simba itaingia katika mchezo huu ikiwa na benchi jipya la ufundi baada ya kumpoteza kocha, Fadlu Davis. Je, wekundu wa msimbazi watapata ushindi wao wa kwanza baada ya kocha wao mkuu kuondoka?
SOMA HII PIA: Rasmi Fadlu Davids ameondoka Simba SC | Mrithi wake, Mtola majanga, Yanga SC mwiba
Cheza na ushinde sasa na ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni muda huu
Zamu yako kushinda na SportPesa, unaweza kushinda mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kupitia Kampuni bora ya michezo ya kubashiri ya SportPesa bonyeza picha hii chini.

H2H kati ya Simba SC vs Fountain Gate FC
Kiujumla tangu Fountain Gate FC kuanza kujisimamia kama timu ya kipekee kuanzia msimu wa 2024/25, imekutana na Simba SC katika mechi 2. Katika mechi hizo Simba SC ilishinda mechi moja na mchezo mmoja ukiisha kwa matokeo ya sare ya bao 1-1. Hivyo mechi ya Alhamisi usiku itakuwa mechi yao ya tatu kwao kukutana.
Michezo mitano iliyopita ya Simba SC
Gaborone United 0-1 Simba SC
Yanga SC 1-0 Simba SC
Simba SC 1-1 RS Berkane
RS Berkane 2-0 Simba SC
Stellenbosch 0-0 Simba SC
Michezo mitano iliyopita ya Fountain Gate FC
Fountain Gate 0-1 Mbeya City
Fountain Gate 2-0 Stand United
Stand United 1-3 Fountain Gate FC
Tanzania Prisons 3-1 Fountain Gate FC
Fountain Gate FC 1-1 Tanzania Prisons
Kikosi cha Simba SC kinachotarajiwa kucheza dhidi ya Fountain Gate FC
Kipa :
Camara
Walinzi:
Kapombe, Naby, Karabou, Rushine,
Viungo:
Kagoma, Kibu, Ahoua,
Washambuliaji:
Sowah, Maema, Mpanzu
Kikosi cha Fountain Gate FC kinachotarajiwa kucheza dhidi ya Simba SC
Kipa:
Fadhil Kisunga
Walinzi
Daniel Jolam, Elie Mokono, Abdallah Kulandana, Lamela Maneno
Viungo
Sadick Ramadhani, Jackson Kataga, Shaaban Pandu.
Washambuliaji
Mudrick Abdi, Shomari Musa na Hassan Ally.
SOMA HII ZAIDI: Seleman Mwalimu ametambulishwa Simba SC kwa mkopo akitokea Wydad | Takwimu zake, magoli
SOMA HII PIA: Kocha mpya Simba SC Hemed Morocco hana presha | Ameanza kazi tayari
Habari mpya kuhusu Simba SC vs Fountain Gate FC

Kufuatia kumpoteza kocha wao mkuu, Fadlu Davis ambaye anatajwa kuibukia Raja Casablanca, Simba wamelazimika kumteua kocha wa Stars, Hemed Morocco kuwa kocha wa muda.
Kutokana na taarifa hiyo Meneja wa Habari na mawasiliano wa Simba Sc, Ahmed Ally amesema: “Tumeona taarifa ya klabu yetu ikiwataja Selemani Matola na Hemed Morocco kuwa makocha wa muda wa kikosi chetu. Rai yangu kwa mashabiki wa Simba ni kuwaunga mkono Makocha hawa, kuwapa ushirikiano na kuwatia moyo, kuwa na imani nao
“Kama ambavyo tunafanya kwa Makocha wengine tunapaswa kufanya hivyo kwa Matola na Morocco, ili wapate mazingira rafiki ya kutimiza majukumu yao
Semaji Ahmed: Mambo mazuri yanakuja
Akiendelea kuzungumzia mwenendo wa kikosi chao, Ahmed amesema: “Mambo mazuri yanakuja ndugu zangu Wana Simba. Tutulie hii ni timu kubwa yenye msingi imara ya kitaasisi haiwezi kuyumba kwa namna yeyote ile. Ni jambo la kawaida Watumishi kuajiriwa na kuoandoka kwenye timu, muhimu ni kutafuta mbadala sahihi na bora zaidi ya aliyeondoka.
“Ninachoweza kuwahikikishia kwamba hakuna kitakachoharibika, wala kurudi nyuma ndani ya klabu yetu. Tunasonga mbele tukiwa bora na imara zaidi. Kwa sasa tutasikia mengi kila mtu akijaribu kupenyeza agenda zake kwa lengo la kuzua taharuki ndani ya klabu yetu. Jahazi letu lipo sawa, halijayumba wala kutikisika, Tunaendelea na safari ya mafanikio.
Hitimisho
Msimu wa Ligi Kuu ya NBC 2025/26 umeanza kwa ushindani mkubwa miongoni mwa timu shiriki. Hii inaonyesha ni kwa kiasi gani kila timu imejizatiti kutoa ushindani na ikiwezekana kuibuka na ubingwa. Hivyo licha ya utofauti wa ubora na ukubwa wa vikosi vya timu zote mbili ambao unaipa Simba nafasi kubwa ya ushindi, bado mechi ya Simba SC vs Fountain Gate FC inatarajiwa kuwa na burudani kubwa na ushindani.

