- Simba SC vs RS Berkane Jumapili 25/5/2025 ni mchezo amza arejesha mzuka Simba SC vs RS Berkane, hii ni baada ya taarifa kuwa kitasa huyo amerejea mazoezini kujiandaa na fainali ya 25/05/2025.
- Ni miaka 22 imepita tangu mara ya mwisho Simba kucheza hatua kubwa ya mashindano yaliyochini ya CAF, ambapo mara ya mwisho kufika hatua hiyo ilikuwa mwaka 1993.
- Simba wataikaribisha RS Berkane Jumapili ya Mei 25, mwaka huu kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Kuelekea mchezo wao wa Fainali ya pili ya combo la Shirikisho Afrika Simba SC vs RS Berkane, uongozi wa Simba umetamba kuwa utamkabidhi Kombe la Afrika Rais Hussein Ali Mwinyi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, kama sehemu ya kumuenzi baba yake mzee Ali Hassan Mwinyi ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati Simba wakicheza fainali ya kombe la washindi mwaka 1993. Uongozi wa Simba umeyasema hayo mara baada ya kutembelea kaburi la mzee Mwinyi, Zanzibar.
Ziara ya Simba kwenye kaburi la Mzee Mwinyi kuelekea Simba SC vs RS Berkane Jumapili 25/5/2025

Ziara ya Simba ilifanyika jana Ijumaa Mei 23, mwaka 2025 ambapo iliongozwa na baadhi ya viongozi wa bodi ya wakurugenzi na viongozi wa zamani wa time hiyo akiwemo Mwenyekiti wa zamani wa Simba Mzee, Hassan Dalali ambapo pamoja na mambo mengine, Simba walisoma dua maalum ya kumuombea marehemu mzee Mwinyi na pia kusoma dua maalum kwa ajili ya kuombea mchezo huo muhimu wa Jumapili.
Mara baada ya dua hizo viongozi hao wa Simba walipata nafase ya kuzungumza na kuweka wazi kuwa maandalizi yote ya kuhakikisha ubingwa unapatikana Jumapili yamekamilika na wana imani kubwa kuwa baada ya Mzee Mwinyi kuukosa ubingwa wa kwanza sasa ni lazima wahakikishe wanampa mtoto wake.
“Mwaka 1993 tulipokuwa na fainali iliyopigwa Uwanja wa Uhuru mbele ya Rais Mwinyi hatukuweza kushinda ubingwa na jambo hilo lilimhuzunisha Mzee wetu, lakini miaka 22 baadae tumepata nafasi nyingine ambayo hatutaki kuipoteza na wakati huu tunataka kuhakikisha tunapambana kushinda ubingwa huu na kumkabidhi mtoto wake na Rais wa sasa wa Zanzibar, Hussein Ali Mwinyi,” amesema Ahmed Ali meneja wa habari na mawasiliano Simba.
Ziara kwa watoto wenye mazingira magumu

Mara baada ya zara hiyo ya kumswalia, Mzee Mwinyi uongozi wa Simba pia ulifanya ziara ya kutembelea vituo viwili vya watoto wenye mazingira magumu na kuwapelekea mahitaji mbalimbali ambayo yanaweza kuwasaidia katika maisha yao ya kawaida ya kila siku ambapo pamoja na hilo walipata nafasi ya kushiriki nao dua ya pamoja.
SOMA HII PIA: JKT Tanzania FC Vs Simba SC 5/5/2025: Mabosi Simba wafanya kikao kizito cha Ubaya ubwela
Fadlu kichwa kuwaka moto
Kazi kubwa iko mbele ya kocha mkuu wa Simba, Fadlu Davis ambaye anatakiwa kuwaandaa vijana wake kisaikolojia kwa ajili vita ya kuvaana na RS Berkane ambao wamekuwa na wakati mzuri na mashindano hayo katika siku za karibuni. Kurejea kwa, Hamza kunafanya kocha mkuu wa Simba, Fadlu Davis kukuna kichwa juu ya nani na nani wanaweza kuanza katika mchezo huo wa Jumapili, ambapo mara kadhaa amekuwa akiwatumia kwa utofauti Hamza, Che Malone na Chamou Karabou.
Simba vs RS Berkane: “HII TUNABEBA.”

Uongozi wa Simba umeendelea kutamba kuwa wanakwenda kupindua meza kuifunga zaidi ya mabao mawili Berkane na kubeba ubingwa wa mashindano hayo ya pili kwa ukubwa barani Afrika.
Akizungumzia mchezo huo Meneja wa habari na mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally amesem: “Mashabiki 16,000 walikuwa tayari wamenunua tiketi kwa ajili ya kushuhudia mchezo wa marudiano wa fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.
“Kutokana na mazingira ya kubadilishwa Uwanja, sasa tiketi zao zitatumika katika Tamasha la Simba Day. Uwanja wa Amaan Zanzibar ambao utapigwa fainali hiyo unaingiza mashabiki 15,000 pekee hivyo tayari kuna watu 10,000 ambao wasingekuwa na nafasi.
“Hivyo tumeamua kuzitumia kwenye tamasha la Simba Day, na tunawaomba mashabiki wetu wazitunze hadi itakapofika siku ya Tamasha la Simba Day.
“Uongozi ulikuwa unapambana kuhakikisha mchezo unapigwa Benjamin Mkapa lakini ilivyoshindikana imebidi tusitishe zoezi la kuuza tiketi, huku walionunua wakiwa ni wengi zaidi ya uwezo wa uwanja wa Amaan Zanzibar,” amesema Ahmed.
SOMA HII PIA: Simba SC wanautaka ubingwa wa CAF, kuwavutia kasi RS Berkane Zanzibar, Mei 25 2025 fainali ya maamuzi
Unaiona Simba SC vs RS Berkane kwa Shilingi ngapi?

Katika hatua nyingine, Ahmed Ahmed ametaja viingilio vya mchezo huo wa Mei 25, mwaka huu ambavyo ni kama ifuatavyo; VIP A Sh. 50,000 Jukwaa la Urusi 30,000 Mzunguko Sh. 10,000. Tayari tiketi zimeanza kuuzwa kwa njia ya mtandao.
Wanaotaka kuiona Simba SC vs RS Berkane kwa ndege wamefikiwa
Ahmed ameongeza kuwa kutakuwa na usafiri wa Ndege wa kwenda na kurudi siku ileile ya mchezo, ambayo gharama yake itakuwa Shilingi 350,000.
“Tutakuwa na usafiri wa Ndege wa kwenda na kurudi na mashabiki watakaolipa kiasi hicho watapata tiketi za VIP A, jezi za fainali pamoja na usafiri wa kutoka na kurudi Uwanja wa Ndege,” amesema Ahmed.
Tujikumbushe sakata la Uwanja wa Benjamin Mkapa
Ikumbukwe hapo awali mchezo huo ulitarajiwa kuchezwa kwenye Uwanja wa Mkapa na tayari mchakato wa kuanza kuuza tiketi za mchezo huo zilianza kuuzwa.
Wakati mchaakato wa mauzo ya tiketi ukiendelea kwa mshituko mkubwa taarifa kutoka Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF), Mei 14 kupitia ripoti ya wakaguzi huru wa kimataifa walibatilisha ubora wa dimba la Mkapa na kuamuru mchezo huo uchezwe Uwanja wa Amaan.
CAF walibainisha kuwa sababu kubwa ni sehemu ya kuchezea ya Uwanja wa Mkapa ‘pitch’ kutofikia viwango ambavyo vinatakiwa kuelekea kwenye fainali na hivyo kuelekeza mchezo uchezwe Zanzibar.
Licha ya jitihada za Serikali, Simba SC na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, (TFF) kupambania mchezo uchezwe Uwanja wa Mkapa kutokana na maboresho ambayo yamefanyika kwenye uwanja huo bado msimamo wa CAF ulibaki palepale.

