Simba SC vs RS BerkaneSimba SC vs RS Berkane
  • Simba SC vs RS Berkane 25/5/2025 live ni zaidi ya mechi ya fainali, hii ni vita ya rekodi ya bingwa mpya wa kombe la Shirikisho Afrika kwa msimu huu wa 2024/25, mchezo unaosubiriwa na mamilioni ya watt Duniani.
  • Mechi hii ni ya fainali ya mkondo wa pili ambayo  Simba watakuwa nyumbani na itapigwa leo Jumapili saa 10:00 jioni kwenye Uwanja wa Amaan Complex, Zanzibar.
  • Kuelekea mchezo huo wa leo dhidi ya Berkane, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi ameahidi kutoa zawadi ya dola 100,000 sawa na zaidi ya Shilingi Milioni 269 ikiwa Simba watafanikiwa kupata ushindi na kubakisha kombe kwenye ardhi ya Tanzania. 
  • Mpaka sasa timu hizo zimekutana  mara 3 ambapo wenyeji Simba wameshinda mchezo mmoja huku RS Berkane wao wakishinda michezo miwili, ikiwemo mchezo wa ushindi wa mabao 2-0 kwenye mchezo wa fainali ya kwanza uliopigwa niching Morocco.

Simba SC vs RS Berkane 25/5/2025 live ni habari kubwa iliyoteka majukwaa mbalimbali ya vyombo vya habari wikiendi hii, hii ni fainali ya mkondo wa pili ya Kombe la Shirikisho Afrika ambapo Simba watakuwa wenyeji wa Berkane kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar. Mvuto wa mchezo huu unatokana na matokeo ya mchezo wa kwanza uliopigwa kwenye Uwanja wa Manispaa ya Berkane.

Simba watoa tamko zito kuelekea Simba SC vs RS Berkane 25/5/2025 live

------------------------------------------------n
Kocha wa Simba Fadlu na mastaa wa timu hiyo

Simba kupitia kwa kocha Mkuu wao, Fadlu Davids ameweka wazi kuwa mchezo wa leo dhidi ya RS Berkane utakuwa mgumu, kwani Berkane ni timu ambayo imekuwa na uzoefu mkubwa wa kucheza michezo mikubwa hususani katika daraja hilo la fainali jambo ambalo Simba inapaswa kuchukua tahadhari kubwa.

Akizungumzia hali ya kikosi chake, Fadlu amesema wachezaji wapo kwenye hali nzuri na wataingia katika mchezo wa leo kwa malengo ya kupindua meza kwa kusaka mabao mawili ya mapema na kusaka bao la ushindi, huku wakiwa makini kuzuia wasiruhusu bao la ugenini kwa Berkane. “Tumejipanga kikamilifu kwa ajili ya mchezo wa fainali hii ya pili, ni wazi kikosi chetu bado kichanga kwenye michuano hii ukilinganisha na wapinzani wetu lakini tumejipanga vizuri na malengo yetu ni kushinda taji hili.

“Tunafahamu kuwa tupo nyuma kwa mabao 2-0 ambayo wapinzani wetu waliyapata kwenye mchezo wa kwanza, ni mlima mkubwa ambao tunapaswa kuonyesha dhamira ya kuupanda kutoka dakika ya kwanza, ili ikiwezekana tupate mabao ya mapema kusawazisha mizania  na kupata la ushindi lakini kuhakikisha haturuhusu bao,” amesema Fadlu.

SOMA HII PIA: Simba SC vs RS Berkane Jumapili 25/5/2025: Simba waahidi ubingwa kwa Rais Mwinyi Zanzibar 

Kapombe aahidi maajabu ya Benjamin Mkapa kutokea Zanzibar 

Simba SC vs RS Berkane 25/5/2025 live
Shomari Kapombe

Akizungumza kwa niaba ya wachezaji mlinzi wa Simba, Shomari Kapombe amesema ubingwa wa michuano hii ni fahari ya kila mchezaji wa Simba na kila mchezaji ana ari kubwa  na wapo tayari kupambana hadi mwisho, kuhakikisha wanakuwa sehemu ya kikosi kitakachoweka historia kuchukua ubingwa wa mashindano hayo.

“Kila mchezaji ana ndoto ya kucheza fainali ya michuano hii mikubwa Afrika, tunafahamu tunaenda kukutana na mpinzani mkubwa ambaye alipata matokeo mazuri nyumbani kwao lakini tupo tayari kupambana hadi mwisho kuandika historia na kufanikisha malengo ya timu,” amesema Kapombe.

Kikosi cha Simba kinachotarajiwa kuanza mchezo wa leo Simba SC vs RS Berkane 25/2/2025 live

Simba SC vs RS Berkane
Simba SC vs RS Berkane

Kuelekea mchezo wa leo, haitarajiwi kuona kocha Simba akifanya mabadiliko makubwa ya kikosi kulinganisha na kile kilichocheza mchezo wa kwanza nchini Morocco, hivyo kikosi cha Simba kinachotarajiwa kuanza ni:

Camara, Kapombe, Zimbwe Jr, Chamou, Che Malone, Kagoma, Kibu, Ngoma, Mukwala, Ahoua, Mpanzu.

SOMA HII PIA: Hamza arejesha mzuka Simba SC vs RS Berkane 25/05/2025

Rais Dkt. Mwinyi aongeza Mzuka kambini Simba aahidi Milioni 269 Mnyama akipata ushindi

SIMBA IKULU YA ZANZIBAR
Simba Ikulu ya Zanzibar

Kuelekea mchezo huo wa leo dhidi ya Berkane, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi ameahidi kutoa zawadi ya dola 100,000 sawa na zaidi ya Shilingi Milioni 269 ikiwa Simba watafanikiwa kupata ushindi na kubakisha kombe kwenye ardhi ya Tanzania. Rais Mwinyi akizungumza katika hafla fupi kuwapa moyo Simba amesema.

“Kwanza Tunawapongeza wa hatua hii kubwa, lakini safari bado haijaisha tubalo jukumu kubwa  la kuipa heshima nchi yetu kwa kushinda ubingwa wa mashindano haya makubwa. Kama Serikali tumeanza kwa kuchukua gharama za Uwanja, lakini pamoja na marafiki zangu tumejichanga na kukusanya kiasi cha dola 100,000 kama zawadi iwapo ushindi wa ubingwa utapatikana.

“Wote tunakumbuka mwaka 1993 mbele ya Mzee wangu Mungu amrehemu, hatukuweza kufanikiwa laqkini tunayo nafasi ya kufanya vizuri zaidi na kufanikiwa kuandika historia mpya mwaka huu,” amesema Rais Mwinyi.

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.