- Clement Mzize mshambuliaji hodari kwenye kufunga mabao akiwa nje ya 18 ama ndani ya 18 anatajwa kuwa kwenye rada za mabosi wa Zamalek FC.
- Mzize alifunga bao kali kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya TP Mazembe, Uwanja wa Mkapa kwa kuachia kombora nzito akiwa nje ya 18.
- Aziz Ki aliyecheza mechi 114 ndani ya kikosi cha Yanga SC muda wowote kuanzia sasa atatangazwa kwenye timu yake mpya.
Clement Mzize anafuata kuondoka Yanga SC baada ya Aziz Ki ambaye inaelezwa kuwa muda wowote atatangazwa kuwa mchezaji mpya wa Klabu ya Wydad Casablanca ya Morocco ambayo imeweka ofa kubwa kuinasa saini yake. Mzize na Aziz Ki zote ni tetesi kuwa timu mbalimbali zinahitaji huduma zao kutokana na uwezo walionao ndani ya uwanja kwenye mechi za ushindani.

Taarifa zinaeleza kuwa Mzize ambaye ni chaguo la kwanza la Kocha Mkuu wa Yanga SC, Miloud Hamdi yupo kwenye rada za mabosi wa Zamalek FC ya Misri ambayo inahitaji saini ya mshambuliaji huyo kijana mwenye nguvu kubwa kwenye mguu wake wa kulia.
Mzize kwenye mechi za ligi amekuwa akitimiza majukumu yake kwa umakini katika kikosi cha Yanga SC. Ni mabao 13 kafunga akiwa mzawa namba moja mwenye mabao mengi ndani ya Ligi Kuu Tanzania Bara ambayo ni namba nne kwa ubora.
Ipo wazi kwamba Mzize ni mchezaji wa kwanza mzawa kufunga bao ndani ya kwa upande wa kikosi cha Yanga SC ilikuwa dhidi ya Kagera Sugar. Kwenye mchezo huo Mzize alianzia benchi na aliingia kipindi cha pili na kufunga bao la kwanza ndani ya msimu wa 2024/25.
Katika mchezo huo baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Kaitaba ulisoma Kagera Sugar 0-2 Yanga SC, bao la kwanza la ufunguzi lilifungwa na kiungo mshambuliaji Maxi Nzengeli ambaye huyu ni rai awa DR Congo.
Kwa nini Zamalek FC kumpigia hesabu Mzize?
Zamalek FC ya Misri inatajwa kuwa kumpigia hesabu Mzize kutokana uwezo alionao kwenye umiliki wa mpira na nguvu miguuni. Mzize rekodi zinaonyesha kuwa amekuwa na uwezo wakufunga mabao kwenye kila eneo ambalo atakuwa iwe nje ya 18 hata ndani ya 18. Jambo hilo limewapa shauku mabosi wa timu hiyo kumfuatilia Mzize.

Mbali na uwezo wakufunga mabao kwa aina zote, nyota huyo anacheza timu ya taifa hivyo uwepo wake ndani ya timu ya taifa unamaanisha kwamba ni miongoni mwa wachezaji ambao wanafuatiliwa kwa ukaribu na makocha wengi.
Nidhamu aliyonayo Mzize kwenye mechi za ushindani ni sababu ambayo inatajwa kuwavutia mabosi wa Zamalek. Hivyo ni suala la muda kusubiri kuona ikiwa dili la mshambuliaji huyo litajibu kwa kuondoka ndani ya Yanga SC ama kuendelea kubaki ndani ya kikosi hicho.
Ikumbukwe kwamba miongoni mwa bao kali alilofunga Mzize ilikuwa kwenye mchezo wa kimataifa Ligi ya Mabingwa Afrika. Januari 4 2025 kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika uliochezwa Uwanja wa Mkapa baada ya dakika 90 uliposoma Yanga SC 3-1 TP Mazembe, Mzize alifunga bao kali kwa mguu wa kulia akiwa nje ya 18 alipoachia kombora iliyomshinda mlinda mlango wa TP Mazembe kwenye mchezo wa hatua ya makundi.
Rekodi za Aziz Ki na Yanga SC
Ipo wazi kwamba Aziz Ki ndani ya kikosi cha Yanga SC amekuwa kwenye rekodi bora baada ya kujiunga na timu hiyo akitokea ASEC Mimosas ya Ivory Coast. Jina lake lilikuwa linatajwa kwa muda mrefu kuhitajika na timu mbalimbali ndani na nje ya Tanzania.

Rekodi zinaonyesha kuwa kiungo Aziz Ki ndani ya kikosi cha Yanga SC ni jumla ya mechi 114 kacheza, akifunga mabao 32 na kutengeneza pasi 57 za mabao rekodi ambazo zinafanya kila timu kuhitaji saini yake.
Bao lake la kwanza kufunga ndani ya ligi ilikuwa kwenye mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar ambapo alianzia benchi katika mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Mkapa na alimtungua kipa Faroukh Shikalo.Ilikuwa ni Septemba 13,2022 Uwanja wa Mkapa dakika ya 90 alipachika bao lake la kwanza akitokea benchi na alimtungua Faroukh Shikalo aliyekuwa langoni akiwa nje ya 18 kwa mguu wa kushoto jambo lililompa lawama kipa huyo.
Nyota huyo msimu wake wa kwanza akiwa na uzi wa Yanga SC alitupia mabao 9 kibindoni na alitoa jumla ya pasi tano za mabao baada ya kucheza jumla ya mechi 23 ndani ya msimu wa 2022/23. Kwenye msimu wake wa kwanza ndani ya Yanga SC alihusika kwenye mabao 14 kati ya 56 ambayo yalifungwa na timu hiyo iliyotwaa ubingwa wa ligi ikiwa na pointi 74.
Inahusiana na hii:Aziz Ki anaondoka Yanga SC kusaini Wydad AC, Simba SC yatajwa
Ofa ya Aziz Ki yatua mezani Yanga SC
Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga SC ameweka wazi kuwa kuna ofa ambayo wamepokea ikiwa inamuhitaji mchezaji wao Aziz Ki kwa kuwa bado ana mkataba wa mwaka mmoja kuendelea kuitumikia timu hiyo. Mchezo wa mwisho kwa Aziz Ki unatajwa kuwa ule wa CRDB Federation Cup dhidi ya JKT Tanzania.
“Tumepokea ofa ya moja ya timu ambayo inahitaji huduma ya Aziz Ki ambaye ni mchezaji wetu. Kwa mujibu wa taratibu tunafanya mazungumzo ili kuona namna gani tutafikia muafaka kwenye jambo hili kwa kuwa Aziz Ki aliongeza mkataba wa miaka miwili na tayari ametumikia mwaka mmoja hivyo bado mkataba wa mwaka ili kuisha.”
Inahusiana na hii:Yanga SC 2-0 JKT Tanzania; Yanga yatinga Fainali Shirikisho CRDB yawasubiri Simba/Singida BS

Ikiwa Aziz Ki ataondoka ndani ya kikosi cha Yanga SC inaeleza kuwa Clatous Chama ambaye ni kiungo mshambuliaji aliyeibuka hapo akitokea Simba SC atakabidhiwa majukumu yake moja kwa moja kwa kuwa katika mechi zilizopita walikuwa wakipishana.

