SportPesa watangaza mshindi wa Supa Jackpot ya zaidi ya Milioni 51
- Baada ya kubashiri kwa usahihi mechi zote 16/17 za Supa Jackpot.
Dar es Salaam. Oktoba 3, 2024. KAMPUNI ya kubashiri Michezo na Burudani SportPesa imemtangaza mshindi wa Supa Jackpot ya zaidi ya shilingi Milioni 51 ambaye ni, Emmanuel Thomas James mwenye umri wa miaka 36 ambaye ni mfanyabiashara wa nafaka kutoka Nyamagana Mwanza, ambaye alibashiri kwa usahihi mechi 16 kati ya 17 kwenye mechi za Supa Jackpot ambayo ina mgawanyiko wa Jackpot za mechi 17,16,15,14 na 13 iliyopata mshindi.

KUHUSU MSHINDI WA SUPA JACKPOT
Akizungumzia mchakato mzima mpaka kuwa mshindi Emmanuel ambaye anaishi na mke wake na mtoto wao mmoja alikuwa na haya ya kusema kupitia mahojiano mafupi aliyoyafanya makao makuu ya SportPesa Masaki, Dar es Salaam;
Ulianza lini kujihusisha na michezo ya kubashiri na umeifahamu vipi SportPesa?
“Nilianza kujihusisha na ubashiri mwaka 2021 ambapo kwa wakati huo nilijifunza kutoka kwa Baba yangu mdogo aitwaye Mzee Mabula (Kwa sasa ni Marehemu) na niliifahamu Kampuni hii kwake na sijawahi kutumia kampuni nyingine zaidi ya SportPesa kwa kuwa watu wengi wanaobashiri wanaielezea kama Kampuni ambayo haina longolongo.
Kwa kawaida huwa unaweka bashiri (mikeka) mingapi?
“Mwanzoni nilikuwa naweka bashiri mbili ambapo huwa napindua matokeo ya baadhi ya mechi kwenye ubashiri wa pili, lakini kwa sasa huwa naweka mkeka mmoja pekee.
Unakumbuka ubashiri wako wa ushindi ulivyokuwa?
“Septemba 28, mwaka huu niliweka ubashiri wa mechi zangu 17 kama ilivyokuwa kawaida yangu ambapo siku hiyo kulikuwa na michezo mitatu ambayo yote nilipatia na Septemba 29, kulikuwa na michezo 14 ambapo nilipatia ubashiri wa mechi 13 na mchezo pekee ambao ulinikwamisha ni kati ya Real Madrid na Atletico Madrid ulioisha kwa sare.
Je, hii ni mara yako ya kwanza kushinda au umewahi kushinda kabla?
“Tangu nilipoanza kubashiri Jackpot za SportPesa mwaka 2021 hii ndio mara yangu ya kwanza kushinda kwenye ubashiri.

Ulipokea taarifa ya ushindi wako kutoka SportPesa ukiwa kwenye mazingira gani?
“Meseji ya ushindi wangu niliipokea usiku wakati nimelala, ilinibidi nitoke chumbani maana mke wangu alikuwa hataki niendelee kujihusisha na mambo ya kubashiri, baad ay akuona nimeshinda nilifurahi sana na nikarudi kulala bila kumwambia mke wangu chochote mpaka kesho yake asubuhi.
“Kiukweli hakuamini kama nimeshinda lakini alipothibitisha nimeshinda ameomba na mimi nimnunulie simu naye ajifunze kubashiri.
Umepanga kufanyia nini fedha zako za ushindi?
“Fedha hizi kwanza kabisa nimepanga kumalizia nyumba yangu ambayo tayari nilishamaliza msingi ili namimi nipate mji wangu, baada ya hapo kiasi kinachofuata nimepanga kukuza biashara yangu ili kuwafikia wateja wengi zaidi na kuboresha kipato changu na maisha ya familia yangu.
UBORA NA UTOFAUTI WA BONASI ZA SPORTPESA
Akizungumzia ubora wa huduma ambazo zinatolewa na SportPesa kulinganisha na Kampuni nyingine, Meneja huduma kwa wateja wa SportPesa, Godwin MwetenI amesema: “Kwanza sisi kama SportPesa tunajivunia kuendelea kutoa washindi kama ilivyo kauli mbiu yetu ya nyumba ya washindi.
“Hapo nyuma tumewahi kupata mshindi wa zaidi ya Bilioni 1 na wengine wakijishindia zaidi ya Milioni 200 na sasa tumempata Emmanuel mshindi wetu wa zaidi ya Shilingi Milioni 51. Kwa faida ya wateja wetu tuna huduma za michezo mingi ambayo wanaweza kushinda ambapo mbali na Supa Jackpot aliyoshinda Mr. Emmanuel tuna huduma nyingi kama vile Single bet, Multbet ambazo zinaenda mpaka mechi 50, kuna live na virtual games.
“lakini pia tuna michezo ya Casino ambapo huko Aviator ‘Kindege’ kinapatikana ambapo unaweza kushinda hadi x1000 ya dau lako na tuna Aviator rain, pia tuna SportPesa league, tuna karata ‘cards’ na michezo mingine mingi inayokuwezesha wewe kushinda ikiwemo goal rush ambayo unacheza bure.
MAELFU YA WASHINDI KILA WIKI

Naye Mkuu wa kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa SportPesa, Sabrina H. Msuya alimpongeza mshindi na kumhimiza kuwa balozi kwa wengine. ‘’Kwanza nikupongeze kwa ushindi huu wa Supa Jackpot. Wewe ni mmoja wa watanzania wengi wanaoshinda mamilioni ya Shilingi kila siku na SportPesa na kuona manufaa yake ambapo bila shaka wewe ni shuhuda.
“Niwakumbushe watanzania Supa Jackpot ipo na itaendelea kuwepo kutegemeana na matokeo ya kila wiki. Endeleeni kutuamini kama ambavyo, Emmanuel ametuamini na matokeo ya ushindi mtayapata’’
Ni miaka saba sasa tangu kuanzishwa kwa kampuni ya SportPesa ikiwa imetangaza jumla ya washindi zaidi ya 10 wa Jackpot na maelfu ya washindi wa bonasi kila wiki.

