Azam FC v MashujaaAzam FC v Mashujaa

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara Yanga chini ya Kocha Mkuu Miguel Gamondi walifungua pazia kwa mchezo wa kwanza wa ligi nyumbani kwa kufosi kukomba pointi tatu mbele ya KMC ubao baada ya dakika 90 uliposoma Yanga 1-0 KMC.

MAXI Nzengeli
KIUNGO mshambuliaji wa Yanga Maxi Nzengeli kwenye mchezo dhidi ya KMC 2024/25. Source : Yanga.

Katika mchezo huo KMC waliingia kwa tahadhari kubwa wakitumia nguvu kubwa kwenye kujilinda huku wakifanya mashambulizi ya kushtukiza kuelekea kwenye lango la Yanga ambapo kipa Djigui Diarra alianza kikosi cha kwanza.

Diarra wa Yanga inayodhaminiwa na SportPesa kakomba dakika 270 bila kufungwa akiwa langoni huku akishuhudia timu hiyo ikifunga jumla ya mabao manne. Yeye ni chaguo la kwanza la Gamondi kwenye eneo la mlinda mlango.

Ikumbukwe kwamba Yanga iliyokamilisha msimu wa 2023/24 ikiwa na jumla ya pointi 80 kibindoni msimu wa 2024/25 ni mechi mbili ilicheza ugenini kwa kuanza na Kagera Sugar 0-2 Yanga, Ken Gold 0-1.

Katika msako wa pointi sita ugenini Yanga ilikomba zote na safu ya ushambuliaji kufunga jumla ya mabao matatu ndani ya mechi mbili ambazo ni dakika 180 za ushindani uwanjani.

HUYU HAPA MKALI WA NYAVU

Nzengeli Yanga
Nzengeli Yanga kinara wa utupiaji ndani ya Yanga 2024/25 akiwa katupia mabao mawili. Source: Yanga.

Kwenye mechi tatu kinara wa utupiaji Yanga ni kiungo mshambuliaji Maxi Nzengeli ambaye amefunga jumla ya mabao mawili. Bao la kwanza alifunga kwenye mchezo dhidi ya Kagera Sugar uliochezwa Uwanja wa Kaitaba baada ya dakika 90 ubao ukasoma Kagera Sugar 0-2 Yanga na bao la pili alifunga Mzize Clement.

Kwenye mchezo wa pili ubao uliposoma Ken Gold 0-1 Yanga mtupiaji alikuwa ni Ibrahim Bacca ambaye alitumia pasi ya Aziz Ki kinara wa pasi ndani ya Yanga akiwa nazo mbili kwa kuwa pasi ya kwanza alitoa kwenye mchezo dhidi ya Kagera Sugar alimpa Mzize.

Maxi alifunga bao la pili kwenye ligi kwenye mchezo dhidi ya KMC akifikisha mabao mawili na anaongoza kwenye orodha ya wakali wa kucheka na nyavu katika kikosi hicho kwa sasa.

BOCCA KWENYE REKODI YAKE

Boka Tuzo
Nyota wa Yanga Bocca akiwa na tuzo yake ya mchezaji bora. Sourc: Yanga.

Nyota Ladrack Bocca alichaguliwa kuwa mchezaji bora kwenye mchezo dhidi ya KMC ikiwa ni rekodi yake kutwaa tuzo hiyo mara mbili mfululizo akiwa na uzi wa Yanga kwenye mechi za ushindani.

Alianza kutwaa tuzo hiyo kwenye mchezo dhidi ya Ken Gold waliposepa na pointi tatu kwenye mchezo huo kutokana na kushirikiana na wachezaji wenzake kufanya kazi kubwa kusaka ushindi ndani ya uwanja.

YANGA YAFIKISHA 9 KIBINDONI

Yanga imeshinda mechi zake zote tatu mfululizo kwenye ligi ikiwa nafasi ya nne kwenye msimamo na pointi zake ni 9. Vinara wa ligi ni Singida Black Stars wakiwa na pointi 13 kibindoni baada ya kucheza mechi 5 ushindi ni kwenye mechi nne mfululizo na sare kwenye mchezo mmoja dhidi ya JKT Tanzania kwa kufungana bao 1-1.

AZAM FC NGOMA NZITO

Matajiri wa Dar, Azam FC ngoma ni nzito kwenye mchezo wao sita baada ya kugawana pointi mojamoja na Mashujaa katika mchezo wa ligi uliochezwa Uwanja wa Lake Tanganyika, mwisho wa reli Kigoma.

Ikumbukwe kwamba Azam FC mchezo wake uliopita ilipoteza pointi tatu mbele ya Simba kwenye Mzizima Dabi mchezo uliochezwa Uwanja wa New Amaan Complex na ubao ukasoma Azam FC 0-2 Yanga kwa mabao ya Leonel Ateba na Fabrince Ngoma.

Kukomba pointi moja kwa Azam FC kunaifanya iwe nafasi ya 5 na pointi zake ni 9 kama ilivyo Yanga ambayo imecheza mechi tatu na kushinda zote ikiwa nafasi ya nne kwenye msimamo na watani zao wa jadi Simba nafasi ya tatu pointi 12.

MNYAMA ASHINDA KWA PENALTI

Ateba na Ngoma
WACHEZAJI wa Simba wakishangilia moja ya bao kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Dodoma Jiji.Source: Simba.

Mnyama Simba mchezo wake wanne wa ligi mbele ya Dodoma Jiji Septemba 29 ilikomba pointi tatu mazima kwa ushindi wa bao 1-0 huku mtupiaji akiwa ni Jean Ahoua kwa pigo la penalti dakika ya 63 kwenye mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa.

Ni Mohamed Hussen Zimbwe Jr nahodha wa Simba alionekana kuchezewa faulo ndani ya 18 na mwamuzi akaamuru upigwe mkwaju wa penalti ukaleta bao pekee la ushindi kwenye mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.

Simba ni nafasi ya tatu kwenye msimamo huku Dodoma Jiji ikiwa nafasi ya 10 ina pointi 6 baada ya kucheza jumla ya mechi 6 kwenye ligi msimu wa 2024/25.

PENALTI YA SIMBA YALETA KILIO

Meky Mexime Kocha Mkuu wa Dodoma Jiji mara baada ya mchezo huo kupitia Azam TV amesema kuwa hajaona hilo na malalamiko kama hayo yapunguzwe kwa kuwa makosa yale hayakustahili penalti.

“Nimeona namna ilivyokuwa lakini sijaona kama ilikuwa ni penalti kwa sababu mpira tumecheza vizuri na nimeona yule alicheza mpira na haikupaswa kuwa hivyo, lakini kwa vitu kama vile haifai sio kila siku lazima tulalamike, haifai.”

Share this: