- Wananchi wametambulisha uzi mpya utakaotumika kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika 2026/27 usiku wa Septemba 2, 2026
- Mwandishi maarufu kwenye masuala ya Habari za Michezo duniani raia wa Italia, Fabrizio Romano kupitia Liveherewego amefungua boxi rasmi lenye jezi mpya.
- Jezi hizo mpya za Wananchi zipo madukani na mashabiki wameanza kuzinunua kwa kasi
Rasmi Yanga SC imetambulisha jezi ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF) 2026/2027. Ni usiku wa Septemba 2, 2026 jambo hilo lilifanyika. Uzinduzi huo umeongozwa na mwandishi wa habari za michezo kutoka Italia, Fabrizio Romano.Moja ya sababu kubwa inayompa umaarufu Romano ni uandishi wa tetesi ambazo asilimia kubwa hukamilika. Liveherewego ni ukurasa rasmi ambao umetumika katika utambulisho wa jezi mpya. Romano alifungua boxi maalumu lilikuwa na jezi za kimataifa akazitambulisha rasmi.
Ijue orodha ya wachezaji wa Yanga SC: Orodha ya wachezaji waliosajiliwa Yanga SC 2026/27 | Benchi la ufundi | SportPesa Blog
Je, bado hujashinda pesa? Cheza aviator ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa
Changamka! sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi zaidi ya Milioni 800 muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

Namna Romano alivyozindua jezi mpya ya Yanga SC CAF

Romano amesema, “Siku ya kufungua vifungashio (unboxing day) leo, washikaji. Haya basi, twende kazi.”
Baada ya maneno hayo alianza kuonyesha jezi mpya za Yanga SC. Romano alionyesha kuvutiwa na muonekano wa jezi hizo.
“Oh, waoh, waoh, waoh! Tazama hii (jezi nyeusi). Inapendeza, eh? Pia ipo ya manjano. Inashangaza!
Kisha… ah, hii ndiyo bora zaidi! (jezi ya kijani),” amesema Romano.
Dunia itajua

Yanga SC CAF Kit 2026/27 tayari zipo madukani. Mashabiki wamejitokeza kwa wingi kupata uzi huo mpya mapema kuanzia Septemba 3,2026. Ni makao makuu ya Yanga SC, Jangwani, Kariakoo uzi huo unauzwa kwa sasa.
Hitimisho
Yanga SC imetambulisha jezi ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambazo zinapatikana nchi nzima kwa sasa. Wawakilishi hawa wa Tanzania katika anga la kimataifa wataanza kucheza ugenini Septemba 5, 2026 nchini Botswana. Gaborone United vs Yanga SC ni mchezo wa hatua ya awali kisha watarejea Dar katika mchezo wa pili Uwanja wa Azam Complex.

