TAMBO zimetawala kwa mabosi wa Fountain Gate baada ya kupata ushindi kwenye mechi mbili mfululizo ndani ya Ligi Kuu Bara msimu wa 2024/25 ndani ya dakika 180 wakikomba pointi sita kibindoni kuku vinara Simba wakishinda mehi mbili na pointi sita wakati Kagera Sugar kwenye mechi tatu dakika 270 wakiambulia vilio.
Ushindi wa mchezo wa Septemba 11 dhidi ya Ken Gold ambao waliupata Fountain Gate unawapa pointi tatu na wanafikisha pointi sita kibindoni baada ya kucheza mechi tatu ambazo ni dakika 270.
Ikumbukwe kwamba mchezo wa kwanza kwa Fountain Gate inayodhaminiwa na SportPesa iliambulia kichapo cha mabao 4-0 dhidi ya Simba mchezo uliochezwa Uwanja wa KMC, Mwenge. Mechi zote suka mkeka wako wakiwa uwanjani kisha unavuna mkwanja na SportPesa.

HAPA NDIPO WALIPO KWA SASA
Ushindi wao nyumbani Uwanja wa Tanzanite Kwaraa ukiwa ni mchezo wa kwanza wa ligi kuchezwa hapo kwa mara ya kwanza unawapeleka mpaka nafasi ya tatu kibindoni na pointi zao ni sita zimetulia.
Ken Gold iliyoanza kufunga kwenye mchezo huo ipo nafasi ya 14 kwenye msimamo baada ya kucheza mechi mbili ambazo ni dakika 180 haijapata ushindi zaidi ya kuyeyusha pointi tatu mazima na kete ya kwanza ilikuwa dhidi ya Singida Black Stars walikuwa nyumbani.
SEMAJI MBUZI KICHEZO TUPU
Ofisa Habari wa Fountain Gate, Issa Liponda maarufu kwa jina la Mbuzi ameangua kicheko huku akiweka wazi kuwa mwisho wao kufungwa ilikuwa mchezo dhidi ya Simba uliokuwa ni wa kwanza kwenye ligi.
“Tulishasema awali kwamba malengo yetu kwenye mechi za mwanzo kukusanya pointi nyingi na kufungwa mchezo wetu wa mwisho ulikuwa dhidi ya Simba hivyo tunaendelea pale ambapo tuliishia baada ya ushindi dhidi ya Namungo.
“Kazi yetu ni kuwapa burudani mashabiki na kikubwa ni kuona tunapata pointi tatu bila makelele na burudani inaonekana kwenye mechi ambayo tunacheza hiyo ni raha ya mpira na pongezi kwa wachezaji na benchi la ufundi kwani kila mmoja anatimiza majukumu yake.”
MWENDO WA FOUNTAIN GATE

Mechi tatu ambazo ni dakika 270 wameambulia ushindi kwenye mechi mbili safu ya ushambuliaji ikifunga mabao manne. Ilikuwa Namungo 0-2 Fountain Gate na Fountain Gate 2-1 Ken Gold. Mchezo waliopoteza ilikuwa Simba 4-0 Fountain Gate.
Ulinzi kwenye mechi tatu ni mabao matano imeruhusu huku safu ya ushambuliaji ikifunga jumla ya mabao manne kwenye mechi tatu.
KAGERA SUGAR NGOMA NZITO

Kagera Sugar inayotumia Uwanja wa Kaitaba mambo ni magumu katika mechi tatu mfululizo ambazo ni dakika 270 kwa kukwama kupata matokeo chanya. Mechi mbili ambazo ni dakika 180 walicheza Uwanja wa Kaitaba ilikuwa Kagera Sugar 0-1 Singida Black Stars, Kagera Sugar 0-2 Yanga huku mtupiaji wa bao la kwanza kwa mabingwa watetezi Yanga akiwa ni Maxi Nzengeli na kete ya tatu ilikuwa Tabora United 1-0 Kagera Sugar, Uwanja wa Ali
Kocha Mkuu wa Kagera Sugar, Paul Nkata ameweka wazi kuwa haikuwa rahisi kupata ushindi ugenini licha ya wachezaji wake kujitahidi kipindi cha pili.
“Mchezo wetu dhidi ya Tabora United tulikuwa tunahitaji ushindi bahati haikuwa upande wetu tukapoteza mchezo. Kipindi cha kwanza tulifanya makosa tukfangwa na kipindi cha pili tulijitahidi lakini tulikosa matokeo.”
MATOKEO YA MECHI ZA SEPTEMBA 11
Tabora United 1-0 Kagera Sugar, goal dakika ya 32 kwa mkwaju wa penalti mtupiaji Asiegbu Shedrack, Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi. Pointi tatu mali ya Tabora United.
Fountain Gate 2-1 Ken Gold kwa Ken Gold mtupiaji ni Joshua Ibrahim dakika ya 9 na Fountain Gate ni Kassim Suleiman dakika ya 42 na Seleman Mwalimu dakika ya 58 Uwanja wa Tanzanite Kwaraa, Babati.
RATIBA SEPTEMBA 12

Singida Black Stars v KMC, saa 10:00 jioni, Uwanja wa Liti. Singida Black Stars inayonolewa na Kocha Mkuu, Patrick Aussems imekuwa kwenye mwendo mzuri katika mechi za awali ikiwa nafasi ya pili kwenye msimamo na pointi sita baada ya kushinda mechi zake zote mbili.
KMC ilianza kwa sare mbele ya Coastal Union kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa KMC, Mwenge Dar leo wanatupa kete yao ya pili ugenini.
Dodoma Jiji v Namungo FC, saa 10:00 jioni, Uwanja wa Tanzanite Kwaraa, Babati saa 10:00 jioni. Namungo kwenye mechi zake mbili haijaambulia ushindi ndani ya dakika 180 huku Dodoma Jiji ikiwa imeambulia sare kwenye mchezo mmoja.
Septemba 13 2024

Azam FC v Pamba Jiji, Azam Complex saa 1;00 usiku
Septemba 14
Tabora United v Tanzania Prisons saa 10:00 jioni.
Septemba 15 2024
Pamba Jiji v Singida Black Stars, saa 8:00 mchana.
Fountain Gate v Dodoma Jiji, saa 10:15.

