WAWAKILISHI wa Tanzania kwenye anga la kimataifa katika Kombe la Shirikisho Afrika Simba wamekwea pipa kuwafuata wapinzani wao Al Ahly Tripoli mchezo unaotarajiwa kuchezwa Septemba 15. Chini ya Kocha Mkuu, Fadlu Davids wanatarajiwa kuwa Libya Septemba 12 kwa maandalizi ya mwisho.
Kuna nyota 22 ambao watakuwa nchini Libya kwenye maandalizi ya mchezo huo ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa na hapa ni rekodi zao ndani ya kikosi cha Simba itakayopeperusha bendera kwenye Kombe la Shirikisho huku Yanga inayodhaminiwa na SportPesa itakuwa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.
AISHI MANULA

Kwenye mechi mbili za ligi hakupata nafasi ya kuanza lakini katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Al Hilal ya Sudan alikomba dakika 45 Uwanja wa KMC, Mwenge.
Katika mchezo huo alionyesha uimara wake kwenye kuokoa michomo alifanya hivyo mara mbili kwa kuokoa hatari ambazo kama angekosa ubao ungebadilika namna ya kusoma ilikuwa dakika ya 32 kwa mkono wa kulia, 33 kwa mkono wa kushoto ilikuwa ni Agosti 31 mchezo huo ulichezwa Uwanja wa KMC, Mwenge.
MOUSSA CAMARA
Huyu kwenye mechi zote mbili za ligi alianza langoni katika mechi za ligi amekuwa na uwezo wa kutuliza mashambulizi na kuoka hatari ndani ya uwanja.
Katika dakika 180 hajaruhusu kufungwa ilikuwa Simba 3-0 Tabora United, Simba 4-0 Singida Fountain Gate. Ikumbukwe kwamba kwenye mechi zote mbili msako wa pointi tatu ulikuwa mali ya Simba baada ya dakika 90.
ALLY SALIM
Alikuwa na kazi kwenye timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars alipata nafasi ya kucheza mechi mbili ilikuwa Tanzania 0-0 Ethiopia na ule wa pili ilikuwa Guinea 1-2 Tanzania. Ndani ya dakika 180 anga la kimataifa alipata nafasi ya kuwa chaguo la kwanza akitunguliwa bao moja ugenini na Mohamed Bayo ilikuwa dakika ya 51.
WALINZI
SHOMARI KAPOMBE
Ni miongoni mwa wachezaji wenye uzoefu wa mechi za kitaifa na kimataifa. Jezi yake ni namba 12 mgongoni amecheza mechi mbili za ligi na kutoa pasi moja ya bao.
KELVIN KIJILI
Ni mechi mbili Kelvin Kijili amecheza za ligi ambapo zote alianzia benchi akikomba dakika 44 Uwanja wa KMC, Mwenge.
MOHAMED HUSSEN

Nahodha wa Simba chaguo la kwanza la Fadlu kacheza mechi zote mbili za ligi akikomba dakika 180 na kutoa pasi moja ya bao. Alikuwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania ambapo mechi zote mbili alipata nafasi ya kuanza kikosi cha kwanza.
VALENTIN NOUMA
Jezi namba 29 anaitumia beki huyu na alipata nafasi ya kuanza kikosi cha kwanza kwenye mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Al Hilal ya Sudan Agosti 31 walipotoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1 Uwanja wa KMC, Mwenge.
CHE MALONE
Beki wa kazi chaguo la kwanza la Fadlu amecheza mechi zote mbili za ligi akikomba dakika 180.Anaingia kwenye orodha ya mfungaji wa bao la kwanza ndani ya Simba kwa msimu wa 2024/25 ndani ya ligi.
Alipachika bao hilo kwenye mchezo dhidi ya Tabora United uliochezwa Uwanja wa KMC, Mwenge ilikuwa dakika ya 13 akiwa ndani ya 18 kwa pigo la kichwa.
KARABOU CHAMOU
Jezi yake ni namba mbili mgongoni iliwahi kuwa mikononi mwa beki wa kazi Gadiel Michael ambaye alikuwa hapo Simba kisha akaibukia Singida Fountain Gate. Mchezo aliopata nafasi ya kuanza kikosi cha kwanza Karabou ilikuwa Agosti 31 dhidi ya Al Hilal ya Sudan ambao ulikuwa ni wa kirafiki.
HAMZA
Katika mchezo wa kimataifa dhidi ya Al Hilal ya Sudan ambao ulikuwa wa kirafiki alianzia benchi lakini kwenye mechi za ligi alipata nafasi ya kuanza kikosi cha kwanza. Ameyeyusha dakika 180 kwenye mechi za ligi.
VIUNGO
OKEJAPHA
Agustino Okejapha nyota huyu alipata nafasi ya kucheza mchezo mmoja wa ligi dhidi ya Tabora United alikomba dakika 19.
DEBORAH
Deborah Fernadnes ni chaguo la kwanza la Fadlu alianza kikosi cha kwanza mechi zote mbili za ligi akikomba dakika 180.
AWESU AWESU
Kiungo rasta ameweka ni mechi mbili za ligi alipata nafasi ya kucheza na kafunga bao moja kwenye mchezo dhidi ya Tabora United uliochezwa Uwanja wa KMC, Mwenge.
YUSUPH KAGOMA

Kiungo huyu yupo kwenye msafara wa Simba ambao utakuwa na kazi ya kusaka ushindi dhidi ya Tripol ya Libya.
JOSHUA MUTALE
Alianza mchezo wa kwanza dhidi ya Tabora United na kupata maumivu katika mchezo huo alipokomba dakika 30 ila kwa sasa yupo fiti kuendelea na majukumu ndani ya Simba.
EDWIN BALUA
Mkali wa mapigo huru kwenye upande wa kona na faulo ni mechi mbili kacheza akifunga bao moja kwenye mchezo dhidi ya Fountain Gate, Uwanja wa KMC, Mwenge. Alikuwa kwenye majukumu ya timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars.
FABRINCE NGOMA
Hajapata nafasi ya kucheza mechi za Ligi Kuu Bara kutokana na sababu ambazo zilielezwa kuwa ni matatizo ya kifamilia lakini yupo kwenye msafara kiungo huyu.
JEAN AHOUA
Kinara wa pasi akiwa nazo tatu ndani ya ligi na katupia bao moja dhidi ya Singida Fountain Gate ilikuwa Agosti 25.
KIBU DENIS
Wanamuita mkandaji mtu wa kazi mwenye spidi na matumiz ya nguvu ndani ya uwanja yupo kwenye orodha ya wachezaji watakaokuwa na kibarua anga la kimataifa.
WASHAMBULIAJI
STEVEN MUKWALA

Mzee wa waa katupia bao moja ndani ya ligi ilikuwa kwenye mchezo dhidi ya Singida Fountain Gate alipotumia pasi ya Shomari Kapombe dakika ya 44.
MASHAKA
Valentino Mashaka ni mkali akitokea benchi kwenye mechi ambazo alipata nafasi ya kucheza ndani ya ligi alifunga mabao mawili dhidi ya Tabor United na Singida Fountain Gate zote alitupia bao mojamoja.
LEONEL ATEBA

Ingizo jipya ndani ya Simba kwenye mchezo wa kwanza kuvaa uzi wa Simba ilikuwa dhidi ya Al Hilal ambao ulikuwa wa kirafiki alitupia bao moja.
Mshambuliaji huyu ameweka wazi kwamba ukwamba wanatambua mchezo wao dhidi Libya utakuwa mgumu lakini watapambana kupata matokoe mazuri ugenini.
“Ni mchezo ambao utakuwa mgumu na ushindani mkubwa lakini sisi wachezaji tunahitaji kupata matokeo mazuri kwenye mchezo wetu.

