skip to Main Content
YANGA Vs USM ALGER KESHO -Historia Iliyosubiriwa Kwa Miaka 30.
YangaUSM

YANGA vs USM ALGER KESHO -Historia iliyosubiriwa kwa miaka 30.

Kesho kwenye dimba la Benjamin Mkapa Jijini Dar es salaam, historia itaandikwa wakati Yanga ya Tanzania itakapowaalika miamba ya soka kutoka Algeria, USM Alger katika pambano la fainali mchezo wa mkondo wa kwanza wa Kombe la Shirikisho barani Afrika.

Hiyo itakuwa ni kwa mara ya pili katika historia ya timu hizo kukutana kwani mnamo August 19,2018 katika dimba la Mkapa timu hizi zilikutana kwenye mchezo wa marudiano hatua ya makundi Klabu bingwa Afrika na Yanga waliibuka na ushindi wa bao 2-1.

Katika mchezo wa mkondo wa marudiano uliopigwa nchini Algeria, mnamo Mei 6,2018, Yanga walichezea kipigo cha magoli 4-0.

Timu hizi zinakutana tena kwa mara nyingine, lakini safari hii ni kwenye fainali, zikiwa zimepitia njia tofauti, Yanga wao wakitokea kundi D na wao walimaliza vinara mbele ya US Monastir, Real Bamako na TP Mazembe.

USM Alger kwa upande wao wametokea kundi A lililokuwa na wapinzani wa Yanga kwenye nusu fainali Marumo Gallants, Al Akhdar na Saint Eloi Lupopo.

Rekodi nzuri waliyonayo Yanga ni kutokupoteza nyumbani mechi zote za michuano hii walizocheza. Wametoka sare mara mbili tu. Mara ya kwanza ni dhidi ya Club Africain, ya pili ni dhidi ya US Monastir na tatu ni dhidi ya Rivers United

Michezo mingine iliyosalia wameshinda, na wamepoteza mechi moja pekee katika michuano hii (dhidi ya US Monastir ya Tunisia ugenini).

Baada ya kumaliza hatua ya makundi, Yanga ilipangwa kucheza na Rivers United hatua ya robo fainali na Wananchi waliwazaba 2-0 na kulipa kisasi cha kuondolewa na wanaijeria hao kwenye hatua za awali kwenye michuano ya Klabu bingwa Afrika msimu uliopita.

Wananchi wakapangwa kukipiga na Marumo ambao ni wababe wa USM Algeria, na wao wakapigwa nyumbani na ugenini kwa jumla ya bao 4-1.

Wachezaji wa USM AlgerKwenye robo fainali, USM iliiondosha AS FAR ya Morocco kwa jumla ya bao 4-2 baada ya michezo miwili na snusu fainali wakaitandika Asec Mimosas ya Ivory Coast bao 2-0.

USMA ndio timu iliyoshinda mechi zote za nyumbani msimu huu huku ikiruhusu bao moja pekee kwenye dimba lake la nyumbani.

Kwa sasa USMA ambao ni mabingwa mara 8 wa Algeria wanakamata nafasi ya 3 kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya nchini mwao wakati Yanga ni mabingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania bara msimu huu.

Kinara wa kupachika mabao wa USMA ni Khaled Bousseilou kafunga mara 4 wakati Yanga wanaye kinara tena kwenye michuano kwa ujumla ana bao 6 na wote wanayo nafasi ya kufanya kitu kwenye mchezo wa fainali.

Macho na masikio ya watanzania yote yapo kwa Yanga ambayo imekuwa Klabu ya pili ya Tanzania kufuzu fainali baada ya takribani miaka 30 kupita ambapo Simba walicheza na kupoteza dhidi ya Stella Abidjan ya Ivory Coast.

Katika kuhamasisha, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan ametoa motisha kwa kuongeza donge nono la zawadi katika kila bao la ushindi litakalofungwa na sasa atalipa Milioni 20, huku akitoa ndege itakayowasafirisha wachezaji na mashabiki wa timu hiyo kwenye mchezo wa marudiano utakaopigwa June 3, 2023 huko Algeria.

Nassredine Nabi ambaye amekuwa na uwanja mpana wa kufanya mabadiliko kwenye kikosi cha Yanga anayo historia ya kucheza fainali ya michuano hii mwaka 2012, akiwa Kocha msaidizi wa AfC Leopards ya DR Congo ambapo walishinda 4-3 hivyo ni faida kwa Yanga juu ya uzoefu wake.

Kuhusu wapinzani kutoka Kaskazini mwa Afrika, Yanga inayo faida ya kucheza na wapinzani kutoka Tunisia mara 4 msimu huu na imepoteza mchezo mmoja tu,jambo ambalo ni ishara kwamba ubora wa kikosi na mbinu, uwepo wa wachezaji washindi kama, Djigui Diarra, Dickson job, Yannick Bangala, Bakari Mwamnyeto, Fiston Mayele n.k unawapa jeuri Yanga ya kushinda mechi zao.

Mashaka ya ugenini yamepotea kwani Yanga ilishinda dhidi ya Club Africain kwa bao 1-0 na kutinga makundi, kama haitoshi, Wananchi wameshinda mechi 4 mfululizo ugenini kwa kiwango cha daraja la juu. Vile vile kwa hapa nyumbani Yanga wamekuwa bora zaidi. Wana sifa zote za kutawazwa na kuwa  mabingwa wapya wa Kombe la Shirikisho barani Africa katika historia ya timu za Tanzania.

USM Alger sio timu ya kubeza abadan. Wanatoka katika ukanda uliojaaliwa mafanikio ya soka katika nyanja zote, kuanzia wachezaji, timu, wataalamu wa ufundi na vifaa. Pamoja na hili mechi hii ina umuhimu wa kipekee kwa Yanga, kwani rekodi wanayoipigania siku ya kesho imetafutwa kwa miaka 30 tangu mara ya mwisho Simba kucheza fainali 1993.

Tayari mechi hii ipo kwenye tovuti yetu. Unaweza kubashiria kwa kutembelea sportpesa.co.tz au kwa kupiga *150*87#.

 

 

 

Share this:
Back To Top