PAMOJA BINGWA AMEPATIKANA SEVILLA vs REAL MADRID NGOMA NZITO
Licha ya kwamba bingwa wa ligi ya Uhispania La Liga ameshapatikana, ambayo ni timu ya Barcelona, jambo moja la kusisimua lipo kwenye kinyang’anyiro cha kumalizia katika nafasi mbili zinazofuata. Utamu wa mechi kati ya Sevilla na Real Madrid unachagizwa zaidi na nafasi aliyopo Real madrid katika msimamo wa ligi ya La Liga.
Timu hizi zinakutana kesho katika mechi itakayochezwa kwenye uwanja wa nyumbani wa timu ya Sevilla Estadio Sanchez Pizjuan, Sevilla wakiwakaribisha Real Madrid, ambapo kama hatashinda basi nafasi ya yeye kubakia kwenye top three itayeyuka. Hii itakuwa hivyo kama Real sociedad atashinda mechi zake zilizosalia alafu Madrid akatoa hata sare moja.
Sevilla wapo nafasi ya 9 wakiwa na alama 48, wanahitaji alama 3 ili kukuzikimbia Osasuna yenye alama 47, Rayo Vallecano yenye alama 46, Real Mallorca yenye alama 44 na Valencia yenye alama 40 kwani wote hao wakishinda wanao uwezo wa kuwafikia.
Vilevile ushindi kwa Sevilla una maana kubwa kwani wataweza kusogea juu hadi nafasi ya 7 kwa kuwashusha Athletic Bilbao yenye alama 50 na Girona wenye alama 49.
Upande wa Real Madrid wapo nafasi ya 3 wakiwa na alama 71, wanataka alama 3 ili wamalize msimu wakiwa juu ya Atletico Madrid yenye alama 72 lakini pia wanahitaji alama hizo 3 ili wawakimbie Real Sociedad walio katika nafasi ya 4 wakiwa na alama 68 hivyo iwapo Los Blancos watatetereka wanaweza kumalizia msimu kwa aibu.
Real Madrid licha ya kuwa wapo katika nafasi ya 3, takwimu zao zinaonyesha hawakuwa na mwenendo mzuri sana wala mwenendo mbaya sana. Hii ndio timu ya pili kwa umiliki wa mchezo katika ligi kuu ya La Liga (59.1%). Sevilla ni ya 9 katika asilimia za kulimiliki mpira wakiwa na (54.3%).
Los Blancos ndio kinara kwa kufunga mabao katika La Liga hadi sasa, ambapo mpaka hivi tunapoandika Habari hii wana jumla ya magoli (70), wakati Sevilla imefunga mabao (44) wakishika nafasi ya 9.
Real Madrid ni hatari zaidi kwa kupiga mashuti yaliyolenga lango, wakiwa wamepiga takribani mashuti 216, ikiwa ni wastani wa mashuti (6.1 kwa kila mchezo). Wenyewe ndio vinara katika La Liga wakati Sevilla wao walipiga mashuti yaliyolenga lango 166 (1.6 kwa mchezo) na wanakamata nafasi ya 10.
Mabingwa wa zamani wa La Liga wameruhusu mabao 33 (wastani wa 0.96 kwa kila mchezo) na ndio timu ya nne kuruhusu mabao machache katika La Liga wakati Sevilla imeruhusu bao 49 ( wastani wa 1.4 kwa kila mchezo) na wanashika nafasi ya 13 kwa kuruhusu bao chache katika La Liga.
Timu hizi zimekutana mara 50 katika historia ya La Liga. Real Madrid imeshinda mechi 31, Sevilla wameshinda mara 16, wakiwa wametoa sare mara 3. Tukiangalia mechi 5 za mwisho ambazo timu hizi zimecheza, Real Madrid imeshinda mara 4, imetoa sare mara 1 na Sevilla haijashinda hata mchezo moja.
Katika mchezo wa mwisho waliyokutana baina yao, katika uwanja wa Santiago Bernabeu, Los Blancos ilishinda mabao 3-1, magoli yaliyofungwa na Luca Modric, Lucas Vasquez na Federico Valverde, huku Eric Lamela ndiye aliyewafungia bao la kufutia machozi Sevilla.
Kwa namna mwenendo wa matokeo ya hivi karibuni kwa timu ya Real Madrid, timu hii inahesabika haipo katika kiwango chake cha ubora uliozoeleka. Tayari Real Madrid wamepoteza mechi 2 mfululizo ikiwemo dhidi ya Manchester City, waliowatupa nje katika nusu fainali ya mashindano ya Klabu bingwa Ulaya.
Sevilla wao kwa upande wao wamekuwa tofauti katika mashindano ya kimataifa barani Ulaya. Wameshinda mechi 3, wametoa sare mechi 2 katika mechi 5 za mwisho ambazo wamecheza siku za karibuni.
Karim Benzema ambaye ni kinara wa mabao wa Real Madrid amefunga (mabao 17 na amepiga mashuti yaliyolenga lango 45). Vini Jr, yeye ana magoli 10 na amepiga mashuti 35 yaliyolenga lango.
Wachezaji hawa wote wawili, yaani Karim Benzema na Vini Jr ni washambuliaji wa kutazamwa zaidi. Kwa upande wa Sevilla, wana Youssef En Nesyr mwenye mabao 8 na mashuti 18, Rafa Mir mwenye mabao 5 na mashuti 12, bila kumsahau Eric Lamela mwenye mabao 4 na amepiga mashuti 19 yaliyolenga lango.
Swali ni je, rekodi ya kuwa na matokeo mazuri dhidi ya Sevilla itawapa faida Real Madrid au tutazame takwimu bora za Sevilla na kiwango kizuri walichonacho kwa sasa?
Mechi hii na nyinginezo nyngi zipo tayari kwenye tovuti yetu ya Sportpesa. Kubashiri tembelea sportpesa.co.tz au piga *150*87#.