skip to Main Content
Manchester United Wanahitaji Points 1 Tu Kwa Chelsea.
ManchesterChelsea

Manchester United wanahitaji points 1 tu kwa Chelsea.

Usiku wa leo katika dimba la Old Trafford patapigwa mechi kali kati ya wenyeji Manchester United watakaowakaribisha timu ya Chelsea kutoka Magharibi mwa jiji la London.

Hii ni mechi ambayo ina umuhimu mkubwa kwa Manchester United ambayo inahitaji alama moja tu kujihakikishia wanapata tiketi ya kucheza Ligi ya mabingwa Ulaya msimu ujao, wakiungana na Manchester City, Arsenal na Newcastle ambao tayari wamekamilisha kazi ya kufuzu siku mbili zilizopita.

Manchester United ina alama 69, ikiwa katika nafasi ya 4 katika msimamo wa ligi kuu ya ya soka nchini Uingereza EPL. Alama walizonazo Manchester United zinaweza kufikiwa na Liverpool.

Majogoo hao wa Anfield wenyewe wana alama 66 hadi sasa. Na ikiwa watashinda mechi yao ya mwisho ya ligi dhidi ya Southampton, wanauwezo wa kufikisha alama 69, ingawa majogoo wa Jiji la Liverpoo wana wastani mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa kuliko Manchester United.

The Red Devil’s wamefunga mabao 52 na kuruhusu mabao 41, wakati Liverpool imefunga magoli 71 na kuruhusu magoli 43, hivyo ili vijana wa Kocha Eric Ten Haag wawaepuke vijana wa Jurgen Klopp, inawabidi waichukue alama moja au ushindi dhidi ya Chelsea na ikiwezekana wamalize juu ya Newcastle United yenye alama 70.

Upande wa Chelsea wao mwenendo wao ulisha fahamika. Hata kama watapata ushindi katika mechi mbili zilizosalia, hawataweza kuwashusha Brentford, walio katika nafasi ya 9 ya msimamo wa ligi, wakiwa na alama 56.

Fulham wao wapo nafasi ya 10, wakiwa na alama 52. Timu pekee ambayo inaweza kuishusha ni Crystal Palace walio juu yao kwa sasa, wakiwa na alama 44 wakati Chelsea ipo nafasi ya 12, huku wakiwa na alama zao 43.

Manchester United inaingia katika mchezo wa leo ikiwa bora kitakwimu katika maeneo mengi. Mpaka sasa The Red Devil’s wanashika nafasi ya 6 katika msimamo wa ligi ya EPL.

Manchester United pia wanaongoza kwa umiliki wa mchezo (54.4%) wakati Chelsea wapo nafasi ya 5 (57.9%) pia ni timu ya 9 msimamo wa EPL kwa kufunga mabao mengi (52).

Wachezaji wa ChelseaChelsea ipo nafasi ya 17 kwa timu zilizofunga mabao mengi (36). Manchester United imefunga mabao 23 kipindi cha kwanza, wakati Chelsea imefunga magoli 14 katika kipindi cha kwanza.

Manchester United imefunga mabao 29 kipindi cha pili, nayo Chelsea imefunga mabao 22 muda huo.

Manchester United inashika nafasi ya 5 katika timu zinazopiga mashuti mengi katika EPL, ikiwa wamepiga jumla ya mashuti (491). Tafsiri yake hapa ni  kwamba timu hii ina wastani wa kupiga mashuti 13 katika kila mechi.

Chelsea kwa upande wao wanashika nafasi ya 9 katika timu zinazopiga mashuti, wakiwa wamepiga jumla ya mashuti (145). Hapa tafsiri yake ni kwamba Chelsea wana wastani wa kupiga mashuti manne katika kila mchezo.

Manchester United inashika nafasi ya 3 kwa kuruhusu magoli mengi ya kufungwa(41). wakati Chelsea nayo ni timu ya 4 katika timu zinazoruhusu magoli mengi (42).

Nyota wa kuchungwa kwa Man United ni Marcus Rashford ambaye ndiye kinara wa kupachika mabao (16) na amepiga mashuti mengi (44), akifuatiwa na Bruno Fernandes mwenye magoli (9) na mashuti (29), wakati Chelsea tegemeo lao ni kwa mshambuliaji Kai Havertz mwenye magoli (7) na mashuti (28) wakati Raheem Sterling ana mabao (6) na mashuti (16).

Kinara wa pasi za mabao wa Manchester United ni Bruno Fernandes wakati kwa Chelsea ni Raheem Sterling mwenye pasi za mabao 3.

Manchester United itakosa huduma za Marcel Sabitzer, Lisandro Martinez, Dony Van De Beek ambao ni majeruhi. Chelsea kwa upande wao itaendelea kukosa huduma ya mchezaji Reece James, Ben Chilwell, Mason Mount na Ngolo Kante, ambao wote wanasumbuliwa na majeraha.

Kwa matokeo ya hivi karibuni Man U imeshinda mechi 3 na kupoteza 2 kati ya 5 za mwisho wakati Chelsea wamepoteza 3, sare 1 na ushindi 1 katika mechi 5 za mwisho.

Katika historia ya EPL timu hizi zimekutana mara 60,Man U imeshinda 17, Chelsea imeshinda 18 na sare zimejitokeza mara 25.

Kubwa zaidi ni kwamba katika mechi 5 za mwisho za EPL kukutana wababe hawa hakuna aliyeibuka mshindi,sare 5.

Je nani ataondoka na ushindi?au sare itaendelea kutawala?takwimu zinatosha kukupa taswira halisi namna ambavyo unaweza kuutabiri mchezo huu kupitia Sportpesa na odds nono zipo kwa ajili yako.

Kucheza na kubashiri tembelea sportpesa.co.tz au piga *150*87#

Share this:
Back To Top